Breaking News

Sms Tamu Za Kumtumia Mpenzi Wako Asubuhi

Uko wapi wangu malkia, mwenzio hamu nasikia nawe ndiye ujuwaye hamu kunitoa, 
tafadhali dear upatapo msg hii tambua nyumbani nakusubiria! Luv u

 Nisamehe la azizi ukweli mbona uko wazi, yule si wangu mpenzi ila ni rafiki yangu 
kipenzi, yangu mapenzi ni wewe pekee nayekupa mpenzi, katika hii dunia ni wewe 
pekee penzi nayekupatia!

. Jamani msg huwezi kunitumia, hata bipu nipate jua rohoni nimekuingia, ila ukata 
umekuingia. U hali gani dia?

. Hakika nakuhurumia kwa msiba uliokukumba, lakini kumbuka mwenzetu ametangulia 
nasi tutafuatia, hakuna haja ya kulia bali ahitaji kuombewa. Mungu akutie nguvu!

. Mpenzi mbona mapenzi yetu kama yanapoteza dira, kila siku huishi hila, kitu 
kidogo wafura hasira. Wanichanganya dia!

 Nina huzuni moyoni sijui kwa kuwa siku hizi sikuoni, naishia kukuota ndotoni, 
hivi kweli nipo kwako moyoni? Nakupenda

 Mahaba unayonipa natamani niwe nawe mpaka kufa, kila siku zinavyozidi kupita 
najuta kwanini nilichelewa penzi kukupa, nakupenda na nitakupenda hadi kufa!

Asubuhi imefika ni muda wa kujiandaa na pilika, lakini kazini ukifika isisahau 
kutumia japo nusu dakika rafiki zako salamu kuwapa, swawabu utapata! Asubuhi 
njema.

 Najua una majonzi kwa kuwa uliyempenda kakumwaga machozi kwa kukuacha ungali 
walihitaji penzi lake, nimekuja mwokozi kukufuta machozi kwakukupa la dhati 
penzi. Nakupenda mpenzi amini sitalimwaga lako chozi, na daima nitakuenzi.

No comments