Breaking News

USHAWAHI KUKUTANA NA WALE WADADA WANAOUZA BIRIANI PEPONI?


Hakuna wanawake ambao wanajisikia raha kama wale wanawake ambao anatembea na mume wa mtu, halafu mwanaume anamshirikisha kila kitu. Mwanaume hawezi kufanya kitu cha maendeleo, iwe ni Biashara au kujenga bila kumuambia na kutaka maoni yake.
Wanajiona sana aisee, yaani ukiwasikia wanavyojisifia kuwa, ananipenda kuliko mke wake, mke wake hana akili,a lifunguliwa duka akalila lote. Basi unaweza udhani ni wale wadada wa peponi amabo wanapika Biriani kila Jumanna (Biriani la kule ni Jumanne).
Hasa ukute mke wa jamaa ni Mama wa nyumbani aisee watasumbua mpaka basi. Lakini ukweli nikuwa hakuna wanawake VIAZI kama hawa. Yaani tena ni vile viazi ambavyo unakuta vimetobolewa, ukikipika unakuta ni kichungu. Wako vizuri na wana akili ya kutafuta, wana mawazo mazuri lakini ni viazi kwenye mapenzi. Najua washaanza kutoa povu kuwa Kaka iddi anatukana hivyo ngoja niwakumbushe tu kidogo.
(1) Anakuambia anakupenda na una akili kuliko mke wake. Mawazo yote ya baishara unatoa wewe, lakini biashara zake na nyumba zake zote zina majija yake. Akifa mke wake mliyekua mnamuona mjinga ndiyo anarithi na wewe unarudi kulia ndani na akili zako.
(2) Mwenzako kaoa, anakuambia anakupenda hampendi mke wake, lakini hamuachi,a nabaki naye hivyo hivyo. Anakubana hataki uwe na mtu, watu wa kikutongoza wanasikia unetembea na flani wanaondoka, ukija kushtuka umri umeenda unaanza sasa kufunga, kusali kila siku,ili kutafuta mume wakati mwenzako anamaisha yake yanaendelea.
(3) Nishamaliza kama hizo sababu hazijakutosha, basi nunua Kitabu changu, nipigie nikupe appointment uongee na mimi, uje nikuambie acha ukinga. Nikuambie namna atakavyokutapeli. Ila kama huniamini hembu fanya hivi, sasa hivia kija kukuomba mawazo ya baishara muambie unataka muwe shea majina yenu wawili na kama ni nyumba muambie kiwanja aandike jina lako uone kama hatakimbia!
utamuzaidiapp


No comments