Breaking News

WANAWAKE WENGI WAKISHAOLEWA HUDHANI MAISHA YAMEISHA, WANAJISAHAU.

utamuzaidiapp

Wanawake wengi wakishaolewa hudhani kuwa maisha yameisha, wanajisahau kwa namna flani, ile dhana kuwa mwanaume yupo basi inawachanganya sana, inawaondolea ule mzuka wa kutafuta, ile hamu ya mafanikio, hasa wale wanawake ambao waume zao wanajali, wanahudumia kila kitu. Wanawake kama hawa wanajisahau sana katika suala la kutafuta, hawa ndiyo utasikia;
(1) Nasubiri kwanza nimalize kuzaa ndiyo nitafute kazi au nifanye Biashara; Ukweli ni kuwa mume anahudumia sina haja ya kubeba mimba huku nikifanya kazi!
(2) Mimba yangu inanisumbua siwezi kufanya chochote; Nikweli wakati mwingine mimba sinasumbua, lakini wanaacha kazi kwakua kuna anayehudumia, single mother angekomaa na bosi na maruhusa, angehangaika na mabarua mpaka basi, single mother asingefunga Biashara, angeajiri mtu lakini kila siku angefuatilia, simu zingepigwa mpaka basi.
(3) Nasubiri mpaka mtoto akue, wanangu hawawezi kulelewa na Dada wa kazi! Wadada wa kazi siku hizi kupata shida; Hapo unakuta mtoto ana mwaka mmoja, sijui anasubiri akue mpaka awe daktari au, hakuna kasi sana ya kutafuta dada wa kazi kwakua hana haraka ya kutafuta kazi, angekua single mother mtoto angebeba hata mgongoni afanye kazi.
Dada yangu, acha kujisahau, anza sasa, anza na kitu kidogo ambacho kinawezekana kwako.

No comments