MTOTO MIAKA 15 ALIYEHUKUMIWA KUUAWA
AKIWA na umri wa miaka 15, Magai Matiop Ngong hakuwa na msaada wowote wa kisheria wakati wa mashtaka yake kabla ya kuhukumiwa kifo.
Kijana huyu Raia wa Sudan Kusini, hivi sasa anakabiliwa na adhabu ya kunyongwa kwa kumuua binamu yake, pamoja na yeye kudai kwamba tukio hilo lilikuwa bahati mbaya. Imemchukua Magai miaka miwili akipigania rufaa yake isikilizwe.Shirika la haki za Binadamu Duniani (Amnesty International) wamepinga adhabu hiyo na kuwaomba wadau wa haki za binadamu kupinga ukatili huo.
No comments