NGUVU YA MUNGU KWENYE NDOA ZETU
MUME wangu kumbuka mimi ni MWANAMKE kama walivyo WANAWAKE wengine kuna muda nahitaji TENDO LA NDOA...
Sauti ya kwikwi ilisikika nyumbani kwa jilani yangu, Nikatamani kuendelea kuaikiliza lakini kadri alivyoendelea kulia Mwanamke huyo nilisikia uchungu sana, Sina uwezo wa kusogea mlangoni kwao nikagonga ili nitoe mchango wangu wa mawazo, Wakati nikiendelea kutafakari ghafla Jilani yangu wa kiume akasikika akisema "NIKUSAIDIEJE KWA MFANO?" .
Hapo ndipo Mwanamke huyo alipandwa hasira na kuanza kugaa gaa sakafuni huku akitupa miguu na kutoa kilio kikali huku akisema maneno mengi, neno ambalo lilinipa simanzi ndani ya moyo wangu ni pale aliposema "NIMESUBIRI SANA MUME WANGU MIAKA SABA LEO HUJAWAHI NIPATIA HAKI YANGU YA NDOA NA WALA HUSUMBUKI HATA KUNIPA TUMAINI JAPO NIHISI UNAUMWA SIKU MOJA MUNGU ATAKUPONYA UNIHUDUMIE.
UNASUMBUKA NA WANAWAKE WENGINE UKINIACHA MPWEKE KAMA VILE SINA THAMANI TENA DUNIANI NIAMBIE NIENDE WAPI NIKAPATE HAKI YANGU?"
Nusu nilie kwa maneno hayo, uchungu mwingi umemjaa dada huyo na kama amevumilia miaka 7, kwanini leo ndipo ashindwe kuendelea kuvumilia?.
Swali hili ndilo lililonitesa sana kiasi nikampigia simu jilani yangu wa kiume alipokea simu na nikamuomba azungumze na mkewe kwa upole Kwani sauti inasambaa na sio majilani wote wanao uwezo wa kustahamili hayo badala yake ndo itakuwa stori ya mtaani.
Jilani akaniomba niende nyumbani kwake ili tuzungumze kama familia, Nilifurahi maana niliona amenipa heshima katika mambo mazito kama ya NDOA mara nyingi hayanaga mshenga ila wahusika kuweka kipaumbele katika maridhiano.
Nikatoka nyumbani kwangu na kuelekea kwa jilani yangu Bwana Stanley, Jamani Habari za hapa? Karibu jilani Karibu sana, Mama yule ndo kwanza analia kwa uchungu nikamsogelea na kumuomba anyamaze ili tuzungumze.
Bahati nzuri niliishi na familia hii kama ndugu hata mama huyo alipoona namuomba anisikie Basi alinyamaza na kumuomba atulie ili tujadili tatizo lililopo katika familia yao.
Stanley nimesikia shemeji akilia sana naomba maelezo yako kwa ufupi sana ili tujue tunafanyaje,
Kwanza kabisa kaka Asante kwa kufika binafsi nilishachanganyikiwa maana nikawa natamani niite ndugu yangu lakini kama ujuavyo binaadam, basi nikaishia kuumia peke yangu.
Jilani wewe ni mtu mzima najuwa umesikia kila kitu Kwani mke wangu amelia kwa uchungu sana kiasi sauti ilisikika mbali, Kuna tatizo katika NDOA yangu yapata miaka saba sasa, yaani kila niliporudi nyumbani nilikosa kabisa hamu ya kushiriki TENDO LA NDOA na mke wangu.
Mwanzoni ilinitesa sana maana tulipopanga kusafiri na mke wangu alijikuta anaingia katika siku zake na kusababisha kutoshiriki TENDO LA NDOA tukiwa safarini, siku moja mke wangu akataka kujuwa Kwanini iwe hivyo?.
Nakumbuka ilikuwa asubuhi yapata kama saa 10 alfajiri mke wangu akaniamsha kutoka usingizini wakati huo nashituka nikamkuta mke wangu akihangaika kutaka tufanye TENDO LA NDOA maana tayari alishanidandia, lakini ghafla mwili wangu ukasinyaa na kusikia mke wangu akilalamika nimechelewa kuamka Kwani nilikuwa "NIME-STIMULATE" kusema ukweli kama binaadam mwenye moyo wa nyama nilimuonea huruma sana mke wangu.
Nikamwambia tutafute mganga ili tujue, tatizo mke wangu alikuwa na IMANI sana akasema atazidi kuomba Mungu tu.
Kuna wakati alipotezea mawazo hayo na siku zikasonga, aliponihitaji alilalamika sana lakini aliniambia neno moja tu HATANISALITI MPAKA KUFA KWAKE... Siku moja alimshirikisha Binam yake na wakapanga namna ya kutaka kubaini kama tatizo lipo kiafya ama Kuna uchawi ndipo yule Binam alijilengesha kwangu na Shetani alivyo mbaya nikajikuta namtamani na niliweza kumhudumia Binam yake mke wangu na Dada yule alifurahia sana TENDO LA NDOA kutoka kwangu.
Baada ya Binam kurudisha majibu kwa mke wangu ndipo mke wangu akataka kujaribu, lakini sikuweza kabisa, na nikwambie tu jilani yangu baada ya kujaribisha kwa Binam yake Mke wangu nilianza tabia mbaya nje ya ndoa yangu.
Niliweza ila ndani sikuweza, Mke wangu akarudi kanisani kama umjuavyo ni mtu wa IBADA na hilo ndilo limeilinda NDOA yangu.
Jilani mpaka kufikia hatua mke wangu kupatwa na hali hii ukweli najisikia vibaya, kwake tu ndo siwezi kumtimizia haki ya ndoa ila kwingine naweza, Mke wangu amenishika na MESSAGE kibao za wanawake lakini kila alipokumbuka tatizo letu alivumilia na kunifichia aibu hii.
Sio kama Mimi ni MWANAUME SURUALI laa hasha brother ni tatizo ambalo sijui chanzo chake, nafikiri kwa maelezo hayo nimemaliza na kama Kuna ambalo sijasema mke wangu atanisaidia kusema ila kwanza kabisa naomba niseme mbele yako NAMPENDA SANA MKE WANGU Yaani pamoja na yote lakini sijawahi mlinganisha na mwanamke mwingine.
Nilishusha pumzi kwa sababu historia hii imegusa UTU WA MTU na kwa hakika katika lile swali ambalo MUNGU ALIULIZA KUWA JE NI NANI AWEZAYE KUMPATA MKE MWEMA? Mimi naomba nijibu kuwa STANLEY UMEMPATA MKE MWEMA maana kwa DUNIA tuliyopo mwanamke sio mtu wa kubembeleza tena Mapenzi maana ukimuona wa nini wenzio wanawaza namna gani watampata.
kwa SENSA wanawake ni wengi kuliko wanaume ila MKE KUMPATA KATIKA KUNDI LA WANAWAKE HAO inakubidi kumshirikisha sana MUNGU vinginevyo leo shemeji yangu asingelia kilio ambacho hata Mimi kimenigusa.
Stanley sihitaji kutafuta majibu katika kesi hii ila napenda niwashirikishe jambo moja nalo ni KUNA TATIZO KATIKA NDOA YENU MNATAKIWA MPATE MTU WA MUNGU ALIYE NA MUNGU NDANI YAKE aweze kuikomboa ndoa yenu.
Naona wazi kabisa mko katika hatari ni vile mkeo analo pendo la dhati kwako, Naomba nimpigie mchungaji aje kuwasaidia vinginevyo sina msaada katika hili maana linahitaji NGUVU YA MUNGU kulitatua.
Muda wote huo mke wa Stanley amejikunyata Dada wa watu akisikiliza tu, Kumkuta mwanamke analilia MAPENZI ujue huyo ni mwenye HEKIMA, mheshimu mwanamke huyo, Kwani hakuna mwanamke humaliza siku bila kuitwa na mwanaume haijarishi ni mzuri au mbaya Kwani kila Mwanamke ana mtu wake na ndivyo ilivyo kwa mwanaume.
Nilipiga simu kwa Mchungaji na kwakuwa alikuwa ni mtumishi kweli kweli Yaani ameitwa na BWANA kuwasaidia wana wa adam, Mchungaji alikuja mahala pale na kwanza kabisa aliwaongoza SARA YA TOBA wana ndoa hawa.
Maombi yalikuwa ya nguvu ya ajabu, Bwana Stanley alianza kupandwa na mapepo yaliongea mambo mengi sana na hata kufikia Mchungaji kuijuwa sababu ya tatizo la Stanley.
Stanley alikuwa analo jini MAHABA ambalo lilimfunga kushiriki TENDO LA NDOA na mkewe ila mwanamke mwingine ilikuwa haina shida, Stanley alilia sana kiasi mkewe akawa na kazi ya kumnyamazisha mumewe.
Ilikuwa simanzi kubwa Kwani mama alilia kujuwa Kuna pepo alikuwa anadhurumu haki yake ya ndoa, Mchungaji aliendelea na kukanyaga nguvu za Shetani na mawakara wake hata jini yule alipokimbia.
Stanley aliingiwa hamu ya ajabu juu ya mkewe, Tayari uwezo wa MUNGU ukajidhihilisha...
Ndugu zangu ULINZI WA NDOA NI WA MUNGU TU maana kwenye furaha ndipo ambapo Shetani hujiinua ili kuharibu.
UPENDO wa Stanley kwa mkewe ndo ulisababisha mwanamke akaendelea kusubiri, Kama sio upendo pamoja na maombi ya Dada huyu ndoa hii isingekuwepo kitambo.
Kwa akili ya kawaida tu MWANAMKE YUPI AJUE HUWEZI KUMPA HAKI YAKE YA NDOA halafu agande tu? Laa Kama ana kidumu nje na abaki kulinda heshima yake tu vinginevyo UTAISOMA NAMBA!
Kama unaamini kwa MUNGU lipo TUMAINI sema AMEN.

No comments