Breaking News

WALI NAZI….2

Nilipiga hatua mpaka kuingia ndani ya chumba cha bafu lile na kuanza kujimwagia maji nilinyanyua makopo kadhaa kabla ya kusikia ngoo! ngoo! Iliyonifanya nigune, kuashiria kuwa mahali pale tayari kumechukuliwa nafasi. Hizi ndio tamaduni mpya nilizokuwa nimezianza kuzielewa baada ya kuishi ndani ya nyumba ile ya kupanga. Mguno ule ulinyamazisha mgongaji na mimi nikaendelea kufanya yangu. Japo kwa safari hii sikuwa nimejiachia kama awali maana yule mgongaji alikuwa kama amenitoa kwenye starehe.
Dakika kadhaa nilimaliza kuoga na kutoka bafuni mule, kutoka kule sura yangu iliendana sambamba na mama Aisha moja kati ya mpangaji mwenzangu . Lakini mtazamo wake ulikuwa tofauti sana nikiwa nimeshika yangu ndoo niliona macho yake yakiwa yameganda chini ya kitovu changu yani maeneo yangu yale ya ikuru ambapo kulikuwa kumetuna kinamna kutokana tu na mzigo nilikuwa nimejaliwa. Nilimpa salamu ambayo ilijibiwa na sauti ya kitemeshi ya mama Aisha lakini mimi sikujali nilipiga hatua kuelekea kilipo chumba changu.
Nilijianda na kuanza kuitafuta njia ya kuelekea kazini, muda mfupi baada ya kuchukua boda boda kwa mara nyingine huku saa yangu ya mkononi ikinionesha saa moja na kamili. Sikuwa nimechelewa ndio ulikuwa muda muafaka wa kuingia ndani ya ofisi. Nilifika kwenye meza ya kusaini kama taratibu ya ofisi yetu ilivyo. Nikiwa pale nilikaribishwa na tabasamu mwanaa la Rose.Nilisaini kabla ya kuanza kuniingizia maneno ya kichokozi kama kawaida yake, nilikuwa nikitabasamu huku nikiwa na mjengea picha kama siku akiingia kwenye kumi na nane zangu basi nimpoteze kabisa . Sijui kinanisukumaga nini? Pindi ni muonapo Rose huwa na waza, waza ngono tu. Nilikuwa nikimvua nguo Rose ilihali yu na zake nguo, maana namna alivyo tu mawazo yangu yote yanaamia kwenye injini yake. Nikijenga picha ukubwa wa injini yake yote kutokana na namna kaumbo chake kilivyo.
Hakika lazima utakuwa unawaza mambo kama hayo kwa mwanaume yoyote mtoto anakiuno kama dondola vile, ukija maeneo yake ya kifuani ndio kabisa chuchu mchongoma , midomo yake utafikiri kama anachinja kuku kutokana tu na maudabwi dabwi yake aliyokuwa anayaweka na kibaya zaidi harufu yake ya marashi ndio ilikuwa ikinimaliza sana.Huyo ndio alikuwa Rose mtoto wa kimanyema kutoka huku Kigoma . Moja kati ya wafanyakazi wa kampuni nilikuwa nikifanya kazi, pindi utokapo uingiapo lazima uonane naye kabla ujaona na watu wengine wote.
Hiyo ndio ilikuwa taratibu zilizowekwa na bosi wa kampuni yetu bwana Aziz Mshongoma , kifupi mwite Mr kama apendavyo
Tuliendelea kuchombezana kwa dakika kadhaa kabla ya kunyanyua mguu na kutoka eneo lile. Hofu yangu ndio ilinitoa pale kwa muda ule nikihofia kukutwa na wafanyakazi ambao walikuwa wakinigia ofisi kwa muda ule, la sivyo nilitamani kuendelea kukaa eneo lile kujalibu hata bahati yangu. Kwa vyovyote ile ingeweza kuleta vijimaneno maneno ambavyo vingeweza kuniharibia kazi na kama si kumuhalibia yeye. Maana mke wa bosi alikuwa tayari kashazama kwangu na kitendo cha kuhisi vyovyote vile juu ya Rose ingeleta tatizo kidogo.
Nilipiga hatua kadhaa kabla ya kuelelekea mahali ilipo kiofisi cha staff yani ya wafanyakazi wa chini ndani ya ofisi ile. Wakati nikipiga hatua nilihisi kama mtu ananiita nilipunguza mwendo kidogo kabla sijageuka.
Nakumbuka vyema siku ile George alipokuja kuniambia habari za yule mama wakati tukiwa tunaendelea na kazi pale kazini kuwa eti muonekeno wake tu yule mama ambaye ndio alikuwa mke wa bosi wa kampuni yetu alikuwa akinihitaji. Huku akiniibia siri kuwa mumewe alikuwa si ridhiki mwazoni sikuwa na amini mpaka pale mama mwenyewe alipojileta wazi kwangu. Dah!… kweli Dar kuna vituko sana mama kama lile la kutembea na mimi nilijisemea kimoyo moyo kabla ya kujipa ushindi tena kwa mara nyingine.
Jambo liliofatia ni kwenda kuoga tu nilitoka na kidoo changu cha maji , nikapokewa na mwanga kwenye macho yangu uliokuwa ukirifukuza giza kuikaribisha siku mpya, vindege navyo havikuwa nyuma kupigana miluzi sijui ndio hivyo au la maana vikawa vinanikumbusha mbali sana yani kila ifikapo asabuhi ya muda ule nilikuwa nikihisi kama nipo nyumbani Dundo ndani ya mkoa wa Tanga. Nikiwa na Babu akinifundisha kuwinda ndege ambaye nilikuwa nikimpenda yule ndege yule nani? yule ahhh!.. Kisie esie. Hapo na kanyimbo nilikuwa na mwimbia kakanipitia kana sema… yakuwa baba yake ndio mie kisiesie usilie ahh!… kanyimbo chenyewe kanitoka muda kweli.
ITAENDELEA..

No comments