Breaking News

WALIOPENDANA KWA DHATI HAWAKUDUMU KWENYE UHUSIANO💯 NA WALIOKO KWENYE NDOA WENGI WAO WANALINDWA NA UVUMILIVU WALA SIO UPENDO 🤭


Mara zote Kwenye PENZI LA KWELI Wivu husitawi kila hatua mnayopiga, ndiyo Maana nikasema WALIOPENDANA KWA DHATI 💘 huwa hawadumu Sana na wakidumu sio Kwenye NDOA😂😂
Uhusiano ni DARAJA LA NDOA hivyo wengi hukomea ng'ambo ya UHUSIANO wala wasifikie ng'ambo ya NDOA.
Kwenye UHUSIANO ndiko mashaka huishi, Kuchunguzana na magomvi ya kila Mara kwa sababu UPENDO WA DHATI 💘 huishi huko, na waliopendana kwa dhati huachana kwa sababu ya WIVU💯
Lakini mioyoni mwao huishi pamoja kwa sababu ya zile nyakati nzuri waliziishi Kwenye uhusiano wao, ndo Maana nikasema:-
👉 NDOA NYINGI ZINALINDWA NA UVUMILIVU WALA SIO UPENDO WA DHATI 💘 KAMA ILIVYO MAANA HALISI YA NDOA.
Kwa sababu Wana ndoa wengi hawaishi na watu waliowapenda kwa dhati, Hasira ama kukata tamaa ya Mahusiano hiyo ndiyo hupelekea NDOA ZISIZO RASMI KUZALIWA😂😂😂
Unafikiri ni kwa nini:-
👉 WALIO KWENYE MAHUSIANO NI NADRA KUSALITI PENZI KULIKO WALIOKO KWENYE NDOA?
Sababu ni ndogo sana, Kwa sababu WENGI WALIOPO KWENYE NDOA HAWAZIFURAHII NDOA ZAO💯
Kuolewa ama kuoa Mtu ambaye hukuwa na malengo nae hii ndiyo sumu mbaya zaidi Kwenye NDOA.
Maana NDOA sio kitu kwamba unaweza kushika na kukiacha, iweje uingie Kwenye NDOA na mtu mwingine ambaye hukuwa na malengo nae etiiii tu Kwa sababu uliyempenda amekuumiza?
Mwiba uliochomwa Kwenye Mahusiano uchomoe, chechemea kuelekea Mahusiano mapya wala sio kuelekea moja kwa moja Kwenye NDOA
Maliza MATATIZO yako Kwenye uwanja wa MAHUSIANO ili ukiamua kuingia Kwenye NDOA uwe smart 🧠
#Elista_kasema_ila_sio_Sheria 🔨
UTAMU KITANDANI


No comments