NILAMBE TENA….1
Ashh!!! OOhhpss!! Bado buana. Kidogo tu hata mizuka haijanipanda ushanilalia kifuani.
“Nilambe tena buana”
“Sina tena muda huo kwanza sitaki tena”
Hiyo ilikuwa ni katika nyumba ya kupanga. Maisha yangu ya hali ya chini mno. Kuishi chini ya elfu moja na mia tano. Chumba nilichokipanga hakikuweza kuzuia sauti za chumba cha jirani yangu. Hivyo ikawa ni suluba
mno kwa upande wangu kutokana na sauti ile ya mwanamke jinsi alivyoonekana kulalama kimahaba lakini mpenzi wake akamjibu vibaya. Cha kunishangaza baada ya jibu lile, sauti ya mwanamke ikasikika akilia kilio cha chinichini. Alionekana kukatishwa mbio ghafla. Mbio za raha. Nikamuonea huruma sana. Lakini mwisho nikapitiwa na usingizi wala sikujua kilichoendelea. Kama alilambwa tena au iliishia pale. Swali nililojiuliza ni kwanini alie? Lazima kuna kitu.
Kesho yake nilikuwa wa kwanza kuamka. Nilikuwa mgeni katika nyumba ile hivyo sikuwa nawafahamu wenyeji. Lengo langu kuamka mapema, ni ili nipate kumuona yule mwanamke aliyelia usiku kisa kunyimwa kulambwa. Usishangae hili, sikuwa na uhakika kama ni mpenzi wake wa moja kwa moja. Maana wahuni wengi kuchukua dada zetu kuwatumia kwa usiku mmoja na kuwaacha. Basi nilichokifanya nilitoa nguo zangu nje ili kufua. Usicheke! Hazikuwa chafu lakini hivyo tu ili niweze kumuona mwanamke yule. Ni kweli fikra zangu zilikuwa sahihi. Asubuhi ileile na mapema, nikamuona mwanamama mkubwa tu akitoka katika chumba kilichomtoa machozi usiku uliopita. Nikashangaa sana mama mkubwa vile eti analilia kulambwa. Alaa!! Nikawaza sana wakati huo akizidi kutembea kwa mbwembwe. Ewalaa!!! Ni vile nilikuwa mwenyewe pale nje, vinginevyo ningekuwa kichekesho kwa watu. Sijui nilianza na mguu gani kupiga hatua, lakini nilijikuta tu nikiwa namfuatilia kujua ni wapi anaishi. Taratibu kama sitaki. Duh!! Si akasimamisha daladala? Nami haraka nikaingia ndani. Mradi tu nifanikiwe kufahamu. Kwa bahati mbaya, muda wa kudai nauli ndipo nakumbuka sikuwa nimechukua fedha. Katika kumuelewesha konda, ndipo mama yule akajitolea kunilipia. Wote tulikuwa tumesimama baada ya kuingia ndani na kukosa sehemu ya kukakaa. Niwe muwazi kwamba aliniokoa na kuzabwa makofi. Maana asubuhi ile daladala nd’o limeingia barabarani halafu umzingue konda na nauli. Wee!! Kutoka kituo tulichopana, akaomba kuteremka kinachofuatia. Nami alipoteremka nikateremka. Sikutaka kupoteza pointi, nikamshukuru kwa kunisaidia.
“Bila wewe sidhani kama muda huu ningekuwa na nguo mwilini maana hawa makonda wana hasira kwelikweli”
“Usijali, kawaida tu huenda hata wewe uliwahi kumsaidia mwingine katika njia nyingine hivyo hayo ndiyo malipo yako.” Hapo ndipo akanichanganya kwa sauti yake ya kubembeleza. Sauti itokayo puani kana kwamba hataki kuongea au akiongea anapata maumivu. Mama mweupe. Weupe wa wastani. Wenye kung’arang’ara. Kalio la wastani. Kiuno kilichokatika haswaa. Ebahana mi sisemi sana maana doh!! Nilimkubali.
“nashukuru” tukaishia hapo kimaongezi lakini nikabaki na kazi moja ya kuhakikisha napafahamu anapoishi. Nikafanikiwa kumuona akiingia ndani ya nyumba moja ya maana. Nasema hivyo kumaanisha nyumba ya gharama. Siyo kinyumba chako hicho cha elfu mbili na miamoja halafu kelele kila kukicha mtaani. Oohh nimejenga. Oohh nina nyumba. Nyumba?? Watu wana viberiti vimepanda tu huko hewani lakini wala hawaongeiongei. Haya utajua mwenyewe na mbwembwe zako za nyumba topetope kutunyima usingizi.
Baada ya kutimiza lengo langu, nikaanza safari ya kurudi nyumbani kwa mguu. Adhabu hiyo. Kisa tu kusikia nilambe tena. Pamoja na kuchoka lakini nilifika. Nikasuuza nguo zangu vyema na kuzianika. Hiyo ilikuwa ni siku yangu ya pili kuwapo ndani ya nyumba ile, huku ikiwa ya kwanza kufahamiana na wapangaji wenzangu. Nyumba ilikuwa na vyumba nane. Hatukuwa tukiishi pale na mwenye nyumba lakini aliweka msimamizi wake ambaye naye alikuwa mpangaji kama mimi. Alikuwa na mwanamke. Labda kwa kukadiria kama miaka thelathini na tano. Kadri siku zilivyokuwa zikisogea, ndivyo nilizidi kuwafahamu wapangaji maana wengi walikuwa na shughuli zao kurudi ni majira ya usiku. Kazi yangu ilikuwa ni ufundi seremara. Si hiyo tu. Kujenga, kutembeza urembo wa wanawake. Nilijishughulisha na shughuli mbalimbali ili mojawapo ikidorola katika mapato, basi nahamia nyingine. Mjini kujituma. Sikuogopa kazi. Watu walinipenda kwasababu ya uchapakazi wangu. Nafsi yangu ikalifurahia hilo kwasabubabu ramani za kazi nilipewa nyingi. Na jinsi ramani zilivyoongezeka, ndivyo mfuko wangu ulituna fedha japokuwa za kubadilisha mbonga na nguo. Sikuwa nimeoa wala sikuwa katika mahusiano kwa kipindi kirefu mno. Nathubutu kusema kipindi kirefu kwasababu ilikuwa yapata miaka mine pasipo kuwa na mpenzi hata wa kusingizia. Si kwamba si kwamba sikuwa na hisia. Lah! Lakini kila nilipokumbuka jinsi mpenzi wangu alivyoniacha kwa dharau kubwa kwasababu ya ufakara wangu, nilikuwa nikiumia nafsi yangu kwa kiasi kikubwa. Akasahau kwamba ipo siku ningefanikiwa kimaisha kwasababu sikuwa mvivu lilipokuja suala la kazi. Ni wengi mno walioonwa na mboni za macho yangu na kuuruhusu moyo wangu kutamani lakini niliishia kujisemea kimoyomoyo. “Labda unipe bila kukutongoza” kauli ya kipuuzi. Kabla ya kupanga ndani ya nyumba ile ya Mzee Mbwana, nilikuwa nimepanga mahali ambapo hapakuwa na wanawake kabisa lakini nikapashindwa kwasababu ya sharia za kubadilikabadilika na kusababisha kero. Sikuwa nikipata usumbufu wa kupishana na wanawake hata kwa bahati mbaya. Lakini sasa niliangukia katika nyumba ya wanawake wengi kuliko wanaume. Ndani ya vyumba nane, vitano vilimilikiwa na wanawake na viwili wanaume. Huku kimoja kilichosalia, wakiishi waliooana. Naamini sasa nimekupatia mwanga mfinyu wa kunifahamu na kufahamu mazingira ya kazi zangu. Twende katika songombigo kali na lenye kusisimua. Nilambe tena.
Ni katika pilikapilika zangu za useremara, ndipo nilikutana tena na mwanamama yule aliyesababisha nitoe nguo zangu safi na kuziloweka kwenye maji. Alikuwa akihitaji thamani za nyumba yake. Yeye pia alistaajabu kukutana na mimi tena. Lakini ule msemo wa wahenga ulikamilika. Siku hiyo kuja kazini kwangu, alikuwa na gari lake. Tx. Kwa wapenzi wa muziki nikitaja Tx basi wamemkumbuka Tx M.William. Tukaelewana bei ya thamani zake. Mwisho akaniaga lakini akaniomba siku ya kuchukua mzigo wake niandamane naye ili niweze kumpangia ndani kwake. Akaondoka nami nikaianza kazi ile maana ilikuwa na ujira mzuri. Ilivyoonekana alikuwa ni mwenye fedha japo hadi wakati huo, sikuwa nimemfahamu kiundani. Kama alikuwa ameolewa au lah!
itaendelea..
No comments