Breaking News

Yafahamu Madhara 9 ya Kuchora Tattoo Mwilini

 

Tattoo ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu huitwa dermis na kubadilisha rangi kabisa inaweza kuwa maisha yako yote au kwa muda tu, itategemea na uwekaji.

kwa dunia ya sasa kujichora tattoo ni kama fasheni kwenye jamii, kuna uwezekano mkubwa sana tatto iliyochorwa kwenye ngozi isitoke maisha yote hivyo kwa usalama ni vizuri kumuona mtaalamu wa tattoo ambaye ni maarufu na ana sifa kubwa katika shughuli hiyo, anaweza kuwa na gharama kubwa lakini itasaidia.

Nchi ya Marekani ndiyo inaongoza duniani kote kwa kuwa na watu wengi wenye tattoo, hivyo kabla hujaamua kuchora tattoo ni vyema kutambua madhara yake kama ambavyo imeainishwa hapa chini.

Kansa ya ngozi;
Hapo mwanzoni wataalamu walikua wanasema hakuna mahusiano kati ya kansa ya ngozi na na tabia ya kujichora tattoo lakini hivi karibuni tafiti kutoka uingereza zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha kansa zikitumika kuchora tattoo.

2. Allergy ya ngozi;

Haijalishi unaweka tattoo kwa muda au ya moja kwa moja kumetokea kesi nyingi za watu wanaopata allergy baada ya kupakwa tattoo, utafiti unaonyesha rangi nyekundu ndio inaongoza kwa kusababisha allergy hizo huku rangi zingine kama nyeusi, purple na zingine hazisababishi. mara nyingi allergy hizi huonekana mtu akikaa juani.

3. Makovu;

Mwili unataambua tattoo kama adui wake hivyo hujaribu kuiondoa kwa njia mbalimbali na kwa kufanya hivyo husababisha makovu ya muda mrefu ambayo yanaweza kuleta magonjwa mengine ya ngozi.

4. Maambukizi ya ukimwi na ugonjwa wa hepatitis;

Tabia ya kurudia sindano zilezile wakati wa kuchora tattoo kunaweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ini kitaalamu kama hepatitis b. ugonjwa huu wa hepatitis b husababisha kansa ya ini ambayo haitibiki. ni vizuri kua makini ili uone kama sindano inayotumika kwako ni mpya.

5. Matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI;

Hichi kipimo ni cha mionzi na kirefu chake ni magnetic resonance imaging, hutumika kupima viungo vya mwili ambavyo havionekani kwa macho ndani ya mwili wa binadamu kama x ray inavyofanya. tatizo ni kwamba kipimo hiki kina sumaku kali kiasi kwamba mtu hatakiwi kuingia kwenye mtambo huo akiwa amevaa chuma chochote na hata kama kiko ndani ya mwili kitavutwa nje, sasa mara nyingi tattoo nyeusi hua imetengenezwa na compound kitaalamu kama iron oxide ambayo ina chembechembe za chuma. hii inaweza ikaleta changamoto kubwa kwenye vipimo.

6. Unaweza kukosa fursa mbalimbali;

Kuna kampuni mbalimbali duniani haziwapi watu kazi kwasababu wamechora tattoo kulingana na imani za kampuni husika lakini pia kazi yeyote ya jeshi duniani hairuhusu tattoo hivyo kama wewe unayesoma hapa umeshachora tattoo ujue kazi ya jeshi huna tena.

7. Tattoo huingiliana na matumizi ya dawa fulani;

Kama wewe unatumia dawa za kuzuia damu isingane mwilini ukichora tattoo inaweza kufanya utoke damu nyingi sana kwani dawa hizo huzuia uwezo wa mwili kukausha damu na kuponyesha vidonda.

8. Magonjwa ya ngozi;

Wakati mwingine bacteria huweza kuvamia sehemu zenye vidonda vya tattoo na kusababisha kutopona haraka, dalili huweza kua homa kali, maunivu makali na sehemu ya tattoo kuvimba.

9. Damu kuganda juu ya ngozi [haematoma];

Hii husababishwa na kuvuja kwa damu nyingi chini ya ngozi, huonekana sana pembeni pembeni ya sehemu ambapo rangi ya tatoo imepita na huchelewesha kupona kwa kidonda.

Aidha watalaamu wa hizi kazi wanasema ni ngumu sana kufuta tattoo japokuwa kuna kifaa kinachoitwa laser ambacho kinaweza kutumika kufuta tattoo yote au sehemu ndogo tu ya tattoo. Na mara nyingi rangi nyeusi zinafutika kirahusu kulinganisha rangi nyingine.

Japokuwa wanasema maumivu yanayotumiaka kufuta tattoo ni makali kuliko maumivu ya kuchora.

No comments