MAMBO 5 UNAYOTAKIWA KUJUA KUHUSIANA NA HEDHI
Je unafahamu inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake? Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni "period", neno hili lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 1822 likimaanisha tukio linalotokea ndani ya muda fulani au linalojirudia baada ya muda fulani. Leo hii tuangalie mambo mengine 5 muhimu kuyajua kuhusiana na hedhi.
1. Kwa wastani, mwanamke huanza kupata hedhi yake ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 12.
2. Mzunguko wa siku za hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Ingawa wengi huwa na mzunguko wa siku 28, lakini kuzidi wiki moja au kuwahi kwa wiki moja ni kitu cha kawaida.
3. Mwanamke huzaliwa na mayai milioni 1 hadi 2. Mayai haya, mengi hufa jinsi mwanamke anavyoendelea kuishi na ni mayai 400 tu ndiyo hukadiriwa kufika hatua ya ukomavu tayari kwa uchavushwaji.
4. Msichana anaweza kupata ujauzito kabla ya kuanza hedhi yake ya kwanza. Hii ni kwa sababu, yai huanza kukomaa kabla ya kuona hedhi yake ya kwanza, hivyo kama atashiriki tendo bila kinga, kuna uwezekano wa kupata ujauzito.
5. Wanawake wengi hufikia ukomo wa kupoata hedhi (menopause) wakiwa na umri wa miaka 48 hadi 55.
No comments