TEGEMEA MATUKIO HAYA 5 IWAPO MWANAMKE WAKO ATAKUFUMANIA NA KICHECHEDE
Mahusiano yana raha yake lakini karaha na majeraha nayo hugubika kedekede.
Hivi umewahi kujiuliza ukimfumania mpenzi yaani ile ndi! Utafanya kitu gani?
Wanawake wao huwa na maamuzi ya tofauti zaidi yanayo tofautiana kwa kiasi kikubwa na wanaume.
Watupipo.com imezungumza na warembo kadhaa katika jiji la Dar es salaam ambao wameeleza mambo watayofanya ikitokea wamewafumania wapenzi wao.
Kufuta mawasiliano.
Baadhi ya wanawake niliozungumza nao, nimegundua kuwa mwanamke ni kiumbe mwenye uvumilivu wa hali ya juu inapokuja suala la maumivu. Hii kauli isipotoshe ukweli kwamba mwanamke ni “mlaini sana”.
Unaweza kumuumiza mwanamke hapa akaku-dump huku anakutazama kama vile anachinja kuku, lakini akiingia tu chumbani kwake anaanza kuangua kilio cha uchungu. Trust me, mwanamke akifikia hapa ni vigumu kurudi.
Mwanadada Ashura Musa kutoka Mikocheni anasema kuwa inataka kuwa na ujasiri unamfumania mtu unayempenda. Lakini mimi nitamfungia vioo.
“Mimi nakaa kimya tu wala sifanyi chochote, lakini nita-mblock kwenye mitandao yote maana atawatuma marafiki zake wamwombee msamaha” anasema Ashura.
Kuachana naye
Kitu kikubwa kinachotokea pindi linapotokea fumanizi ni kuachana. Kama ikitokea umefumaniwa halafu hujaachwa basi ujue umebarikiwa na usirudie tena.
Mwanadada Asia Mbelwa ameniambia yeye akifumania, hasemi chochote zaidi ya ‘IT’S OVER’
“Yaani haina haja ya kupigana maana ameshafanya, nitachokifanya naachana naye hapo hapo yani na-delete kila sehemu” anasema mrembo huyu.
Kuondoka.
Ukipoteza uaminifu wa mtu ukabakia kuchovya chovya tegemea kuachwa. Lakini Josephine yeye anasema ikitokea yeye amekufumania ataondoka tu bila hata kuzungumza lakini huo ndio mwisho wa penzi.
“Naondoka lakini ndio mapenzi basi tena, yani nam-block kila mahali na asinitafute tena, lakini sijui ntapigana au yani hata sijui” Josephine anasema.
Kupigana nao
Hili ndio tukio ambalo hutakiwi kukutana nalo mvulana. Unapofumaniwa halafu mabinti wanaamua kuzichapa kavukavu. Mbaya zaidi ni pale wanapoamua kutumia na silaha na kuumizana zaidi au hata ku-uana.
Ni afadhali wanawake wote waliofunguka kwenye stori hii lakini Rahma yeye anasema akimfumania mpenzi wake anazichapa.
“Nitapigana na huyo mwanamke, mabwana wote kawakosa kaona bwana wangu ndio wakutembea nae?”
“Hata nikipigwa na yeye nimempiga, hee! Tunagawana majengo” alisema.
Sitaki kukushauri kitu cha kufanya wakati ukimfumania mtu kwa sababu wewe ndio utakuwa muamuzi wa mwisho, na wewe ndio utakuwa unajiskia maumivu… So una uhuru wa kuchukua uamuzi wowote. Lakini kama unajipenda ni afadhali ufikirie.
Je wewe una thamani yoyote? Je wewe ni msaliti? Je wewe unastahili kusalitiwa?
Mtu anapoamua kukusaliti ina maana amekukosea heshima kwa kiasi kikubwa mpaka amefikia kuchanganya tamu yako na tamu ya mtu mwingine. Ikiwe wewe hujamsaliti mtu na yeye amekusaliti ina maana yeye ndio mkosaji.
Ikitokea kwa bahati mbaya umefumania, nadhani ni vizuri ukachukua uamuzi ambao hautakufanya ujutie baadae. Ni vizuri ukakumbuka thamani yako kwanza na kujipanga kwa uamuzi sahihi.
Kuachana ni kitu cha kawaida sana hasa kama mtu sio mume wako, lakini inategemea mnaachana vipi?
Karibu tena watupipo nitakuletea mbinu za kufuata ili ikitokea siku umefumania uweze kuhimili pigo hilo na kuchukua uamuzi sahihi.
No comments