UNAPOINGIA KWENYE MAHUSIANO KUWA MTU AMBAYE HAJAWAHI KUWA NA HISTORIA YA MAUMIVU YA MAPENZI
*Kila siku tunajadili kuhusu mahusiano lakini cha ajabu ni kwamba bado tuna-fail. Sasa cha msingi mtu unapoingia kwenye mahusiano kuwa kama mtu ambaye huna historia ya maumivu ya mapenzi, ujue kuna watu tunaingia kwenye mahusiano mapya wakati bado tumetunza gunia la maumivu ya mapenzi ya nyuma, ukiingia kwenye mahusiano ukiwa mpya mambo yataenda vyema, lakini ukiingia na maumivu kila chema utakiona kibaya coz moyo wako unakumbuka mabaya aliyofanya fulani mtu ambaye Kwa muda huo hujui hata yuko sayari gani na shida nyingine watu wengine tunaingia kwenye mahusiano kulipiza visasi Kwa hawa ambao hata si wao waliotuumiza, Jambo ambalo tunakosea kikubwa ni kubadilika na kufuta dhana ya wanawake/wanaume wako Sawa. Waliozaliwa tumbo moja wenyewe hawako Sawa sasa utamfananishaje fulani na fulani?? Wewe umeumizwa na Happy kwanini uamini hata Joyce anakuumiza??? Wewe umeumizwa na Godwin kwanini uamini hata Freddy atakuumiza?? Hizo ni dhana potofu ambazo zinatakiwa kufutika kwenye Akili zetu, ili tuweze kufurahia mahusiano*
No comments