Breaking News

VITU VINAVYOTEKA HISIA ZA WANAUME KIMAPENZI KILA WAMWONAPO MWANAMKE

 

Linapokuja swala la wanaume kuvutiwa na mwanamke, mara nyingi sifa zinazowavutia na kuteka hisia zao kimapenzi hutofautiana, lakini zipo sifa ambazo wanaume wote hujikuta wakizizingatia hususan upande wa mavazi na mtindo wa maisha:
Hapa chini nitadadavua sifa tano ambazo wanaume huzipa kipaumbele linapokuja suala la kuvutiwa na mwanamke:
1. Mwanamke anaweza kuwa na vitu anavyopenda kufanya siku ya mapumziko ya kazi hususan kushiriki michezo au kuwa na mtoko na marafiki zake, lakini kama mwanamke anaye mpenzi ambaye ni mshabiki wa mpira au mchezo wowote inaleta mvuto zaidi iwapo mwanamke ataungana na mpenzi wake kwenda kuangalia mashindano hayo au kumuangalia anaposhiriki mashindano hayo. Kwa mfano wanaume wengi ni washabiki wa mpira wa miguu, kwa hiyo kama mwanamke anajua mpenzi wake ni mshabiki wa timu flani na siku hiyo ya mapumziko timu yake inacheza basi itamuweka mwanamke katika mazingira ya kuwa chaguo la mpenzi wake au uhusiano wake na mwenzi wake utakuwa na furaha na amani iwapo atatoka na mwenzi wake kwenda kuangalia mpira wakiwa pamoja, tena itapendeza zaidi iwapo atanunua Jezi ya timu anayoshabikia mwenzi wake. Jambo hilo litamfurahisha sana mwenzi wake na litaboresha mapenzi yao….
2. Wakati mwingine maumbile yanaweza kumfanya mwanamke akawa mvivu kutafuta vivazi vinavyokwenda na wakati kwa kuhofia kuonekana kituko, lakini jambo moja ambalo baadhi ya wanawake hawalijui ni kwamba kuna aina nyingi ya mavazi ambayo yanaweza kumfanya mwanamke kuwa na mvuto wa kipekee (Sexy) bila kujali ana umbo la namna gani. Pale ambapo mwanamke ataombwa mtoko na mwenzi wake kwenda kwenye Club ni vyema mwanamke akachagua aina ya mavazi yatakayomfanya awe na mvuto wa kipekee (Sexy). Kwa kuwa na mvuto wa kipekee kutamfanya mwenzi wake afurahiye kutoka naye na jambo hilo litaboresha uhusiano wake na mwenzi wake…..
3. Kwa kawaida wanaume huwa wanapenda wanawake wanaojua tofauti ya mavazi ya kanisani, kazini na kwenye club. Kwa bahati mbaya wapo baadhi ya wanawake hawajui kutofautisha mavazi na tukio, Wao vazi lolote litatumika popote, utakuta nguo ya ofisini, hiyo hiyo itatumika kwenye club, hiyo hiyo itatumika kanisani na hata ofisini. Mwanamke anayejua kupangilia mavazi kutokana na matukio anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwavutia wanaume au kuboresha penzi lake kwa mwenzi wake.
4. katika mambo ambayo yanawakera wanaume wengi ni kitendo cha wanawake kuchukua muda mrefu kujiandaa pale wanapokuwa na mtoko. Najua wanawake wanaweza kuja hapa na kujitetea, lakini hata pale ambapo mwanaume anamstukiza mwenzi wake mtoko wa ghafla lakini sio wa kwenda mbali bali kwenda baa au glossary ya karibu kupata moja moto moja baridi au nyama choma inashangaza kwamba wakati mwanaume anaweza kutumia dakika tano tu, lakini mwanamke akachukua nusu saa au dakika 45 kujiandaa. Usije ukadhani kwamba akitoka atakuwa amependeza sana, la hasha, anaweza kuwa na muonekanao wa kawaida mpaka ukashangaa kwamba muda wote alikuwa akifanya nini humo ndani…. Ni vyema wanawake wakajua kwamba wanaume wengi wanakerwa sana na tabia hii, na kama mwanamke ana mazoea ya kuchukua karne kujiandaa hata kwa mtoko mdogo, basi usishangae akiona mwenzi wake hampi mtoko, kwani atakuwa anakwepa kukwazika….
5. Msijidanganye ukweli ni kwamba mavazi ya kulalia yana mchango mkubwa sana katika kuwavutia wanaume, kama mwanamke atakuwa na mavazi ya kulallia yenye kum shape vizuri na kuacha mwili wake ukionekana vyema, hicho ni kichocheo sahihi cha kumchanganya mwanaume kimapenzi…

No comments