DADA ZANGU MSIWE VIPOFU
Kama mtu anakupenda na anakujali lazima atafanya jitihada ya kutengeneza muda wa kuwa karibu na wewe bila kujali ubize au umbali uliopo kati yenu,,,atakuwa karibu na wewe kwa namna yoyote,,atajivunia kuwa na wewe na ataonesha wazi namna anavyofurahia uwepo wako kwake,,,
Hivyo kuwa makini...usihadaiwe na hizo nakupenda sana au nimekumiss sana,,,lazima kuwepo na jitihada za kumaanisha hayo maneno,,,,kumbuka muda ni mali adimu,, usikubali kuchezewa michezo ya kitoto ukapoteza muda wako,,,,,okoa moyo wako na muda wako kwa watu wasio serious na mahusiano yasiyokujenga na zaidi kukumaliza kiuchumi na kifikra.

No comments