Breaking News

DADA ZANGU;MUEPUKE SANA MWANAUME ALIYEKUACHA KWA MBWEMBWE AKITAKA MRUDIANE

 



Mwanaume yeyote aliyekuacha kwa dharau,,dhihaka,,matusi au hata kukuonyesha uchafu aliokuwa anaufanya na wanawake wengine,,akikuomba mrudiane Nate usikubali
Nakusisitizia tena USIKUBALI,,kama alishindwa kutambua thamani yako wakati mpo pamoja hadi mkaachana,,hawezi kuitambua hata mkirudiana,,furaha ya mwanaume kama huyo ni kumuona mwanamke aliye achana nae akipata tabu,akilia na kuhuzunika katika maisha yake.
Mwanaume hujihisi fala pale anapokuona unaendelea na maisha yako kama kawaida,,una furaha na amani katika moyo wako,,humtegemei wala kumlilia kama ulivyo kuwa unafanya hapo awali juu yake,,,,Hivyo atafanya kila liwezekanalo mrudiane then akurudishe kwenye vikwazo ulivyovivuka.
Endelea kumuomba Mungu ili akusaidie uweze kusimama mwenyewe katika maisha yako,,Muombe sana Mungu aendelee kuyalinda mahusiano yako mapya,,ampe imani ya kukujalia huyo mwenza wako mpya,,akupende na kuyafanya mahusiano yenu kuwa yenye tija,,
Muepuke sana mwanaume aliyekuacha kwa mbwembwe kisha anakuja kwa hekima akitaka mrudiane baada ya kuona umefanikiwa kuyashinda majaribu yake na FURAHA YAKO KUIMARIKA.

No comments