MAZINGIRA YASIYOEPUKIKA KWA MWANAMKE KUTOA MAAMUZI
una mambo ambayo wataalamu wengi wamekuwa wakiongelea katika maisha hasa yanayohusiana na hisia, tunapokuja kwenye swala la kutaka kufanya maamuzi tunashauriwa sana kuepuka kufanya maamuzi unapokuwa na hisia fulani, hii inaweza kukuletea matokeo chanya au hasi lakini mara nyingi unakuwa haujategemea kupata matokeo hayo kulingana na hali uliyokuwa nayo.
Kwa wanawake, hii huwa ngumu kwao kwa sababu kuna hali ambazo aidha kwa kupenda au kutokupenda anaweza kujikuta tu akifanya maamuzi bila kujali yataleta matokeo gani baadae.
Kwa kumsikiliza pia moja ya wataalamu wa mahusiano kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salam , Chris Mauki anasema kuwa kuna hali ambazo mwanamke hata ufanye nini inakuwa ngumu kwake kuacha kufanya maamuzi pengine apate mtu wa karibu sana kuweza kuzipinga hatua zake.
Baadhi ya hali hizo zinazoweza kumfanya ashindwe kuacha kufanya maamuzi ni pamoja na :-
- Akiwa mpweke – akiwa na kiu ya kuliwazwa kwenye upweke wake haangalii huyu ni mume wa mtu, mchumba wa mtu, mzazi wa mtu. Yeye anachotaka upweke wake uishe
- Akiwa desparate (mwenye kiu ya kuolewa) – mwanamke akiwa kwenye hali hii, basi mwanaume yoyote kwake ni potential husband, awe mume wa mtu au la, akifikia hapa hajali mambo ya kupima afya, mambo ya dini au imani, vigezo na masharti vyote vinafukiwa ardhini.
- Akiwa na kiu ya mtoto – Hapa hajaliwi mtu inajaliwa mbegu tu. Kila akiona mwanaume anamwona kama baba mtoto wake, hapa haliangaliwi penzi tena bali mbegu za mtoto. Hapa hata kama ana imani ya kuhamisha milima atakuwa tayari kwenda kwa mganga pale anapoona maombi hayafanyi kazi. Mtoto atatafutwa come what may, come sun come rain
Hali yako na mapito yako yasikufanye ushushe standards zako. Ndio maana taji hata siku moja haitolewi mwanzoni bali mwishoni. Yeye avumiliaye atavikwa taji –
No comments