UNAACHWA KWASABABU UNALALAMIKA SANA KUHUSU KUUMIZWA;
Umeshaumizwa mara ya kwanza, ya pili na ya tatu, unabeba maumivu yako kila sehemu. Wanawake wengi walioumizwa wanadhani kua wanaume wana huruma, wanadhani wakimuambia mwanaume “Sitaki tena mtu wa kiniumiza kama X wangu” ndiyo mwanaume hatamuumiza. Hiki ni kitu cha kwanza ambacho ukimuambia mwanaume kuhusu wewe basi kuna uwezekano mkubwa akakuacha kwasababu kuu mbili.
Kwanza kabisa nikuwa, kama wewe si msichana wake wa kwanza basi kuna sehemu nayeye ameshaumiza, kwamba ili awe na wewe alishakua na mwanamke mwingine, akamuacha na kumuumiza kama ulivyoumizwa. Mara nyingi unakuta tabia nyingi za X wako naye anazo, kwakulalamika humfanyi akuonee huruma bali akuone kuwa wewe ni mwanamke wa kulalamika lalamika sana hivyo kuboreka hata kuwa nawe kwani anaona pia hujiamini.
Pili nikama unamuambia kua wewe ni mtu wa kukataliwa, kwamba wewe ni takataka ya mtu na hakuna mtu anayependa takataka. Tuchukulie mfano chakula kingeweza kuongea, wewe ufike hotelini halafu kabla ya kuanza kula chakula kinakuambia “Nawewe usije kunionja na kunaicha kama flani, yeye alinishikashika akala na kunichafua kisha akaniacha!” Hivi ndiyo ungekula kile chakula au ungeachana nacho. Mimi ningeacha na kama ningekua na njaa sana ningekula kidogo kisha kuacha.
Wanawake wanaolalamika lalamika sana kuhusu kuachwa kwanza wanaboa, pili wanajishushia hadhi, wanajionyesha kama ni watu wa kuachwa achwa. Anajua umeachwa lakini huna haja ya kulia, huna haja ya kujionyesha mnyonge, acha kuonyesha kua kuna mwanaume alishakukataa ndiyo ukamkubali yeye. Hembu muambie kua umeachana na X wako, mlishindwana tabia basi, muambie alikua anakusumbua ukaona kila mtu aishi kivyake basi.
Asikuone makombo, uonyeshe kuwa angalau unajiamini, kwamba wewe si chakula kilichokataliwa bali ulimkataa mlaji. Wanaume wanapenda wanwake wanaojiamini, wanaojua thamani zao na ambao hawalalamiki lalamiki. Kama ni mtu wa kulalamika lalamika, kila saa unakua na huzuni basi jua unawakimbiza wanaume, unawafanya wakuchezee wakuache kwani hakuna mwanaume anayetaka wanawake wenye huzuni, kila mtu anataka furaha, anataka kuwa na mtua mbaye hajakataliwa.
No comments