Breaking News

ZIFAHAMU SIFA KUU ZA MWANAMKE WA KUOA

 


Kuna vitu vingi sana mwanamke anapaswa kujua kabla hajakuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume anaefikiri kuwa atakuwa mume wake.Wanaume wanatabia ya kupima baadhi ya vitu kutoka kwa mwanamke, na baada ya hapo huamua kama mwanamke aliyenae anaweza kuwa mkewe.
Kuna wakati utashangaa kwanini mwanaume uliyekaa nae kwa muda mrefu lakini kaenda kuoa mwanamke mwingine, inawezekana kabisa alikuwa anakupima kwa muda mrefu na akagundua  una vingi anavyopenda lakini hauna vichache ambavyo ni muhimu kwake.Zifahamu sifa hizi ziznazoweka kuwa  ni muhimu zaidi kwa mwanaume
  • Wanaume wengi hufarahia sana wanapopata mwanamke anaeweza kuishi vizuri na ndugu zake tena hasa mama yake mzazi, mwanaume huwa ana upendo  sana na mama yake kwaio ili kuweza ku-win maisha  ya mapenzi kwa mwanaume anaetarajiwa kuwa mumeo basi ni vyema ukawa na upendo na ndugu zake, mtunze vyema mama yake, kuwa karibu nae, sikilza shida zake na jenga mahusiano mazuri hata kama huko  mbali na mama mkwe.
  • Hakuna mtu asiependa kunyeyekewa  hasa mwanaume, mwanamke anapokuwa na heshima kwa  mwanaume itakufanya akuhitaji sana katika maisha yake, kuwa mtu wa kusikiliza na kutoa majibu yenye heshima, mfanye mwanaume wako ajue kuwa unamuheshimu.Hapa siongelei kumuogopa mwanaume bali kuwa msikivu, mnyenyekevu na mwenye heshima . Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mwanamke ni kichwa cha familia, basi na wewe muoneshe mwenzi wako kuwa hata kama unampita au mko sawa kiuchumi bado yeye atabaki kuwa mwanaume katika mahusiano na ndoa yenu.
  • Wanaume hupendelea  mwanamke hasiependa kujipodoa sana , mwanamke mwenye uhalisia wake, hata kama unataka kubadilisha muonekano  na kuwa tofauti jitahiid kutokuvaa make-up yenye kukufanya uonekane tofauti.Kwa mfano unakuta mwanamke kajipodoa  na marangi mengi mdomoni, kaweka kope, kapaka wanja mwanzo mpaka mwisho , hii inaharibu uhalisia wako.mara nyingine unaweza kuona mwanamke kuanzi asubuhi mpaka jioni kajipodoa wanja na lipstick hazikauki usoni, mwanamke hana asubuhi wala jioni. Dada jitahidi kuwa  na muonekano wako wa uhalisia ili kama anaamua kukupenda basi akupende kama ulivyo

No comments