Breaking News

Majibu 4 yenye manufaa katika Maisha yako ya Mahusiano!

 


Na:HekimaI.Luvanda.

Kwa kila anayetazamia kuwa na maisha yenye furaha katika ndoa yake,au maisha ya uchumba hana budi kujifunza majibu manne yenye maaana kubwa katika maisha ya mapenzi!

Nakupendekezea mjibu manne;



JIFUNZE KUSEMA NDIYO

Ndiyo..yako iwe ni hakika katika kila utakalo lifanya.Hebu jifunze kusema ndiyo kama kweli unamaanisha hicho ukisemacho.
Usiogope kusema ndiyo kama kweli moyo wako na nafsi yako vinakuambia hivyo.
Dàima epuka unafiki katika maisha yako.
Kuna mtu amewahi kusema ...ikiwa unasema ndiyo basi iwe ni ndiyo kubwa.
Usione haya kumweleza mwenzi wako kilichopo moyoni mwako.


JIFUNZE KUSEMA HAPANA

Kwa hapana yako pia yaweza kubadili mwelekeo mbaya ambao huenda ungeathili maisha yako.
Hapana , hapana ...kwa kile nisichokitaka kwanini niumie kwasababu ya mtu fulani asiye na huruma na maisha yangu?
Tumia jibu la hapana pale inapobidi;
Ukikasirishwa sema hapana
Ukiumizwa sema hapana kwa hilo
Ukifanyiwa jambo lolote lisilokupendeza usione Shaka kusema hapana pale usipo pendezwa.
Mtu ambaye anakuwa wazi katika maisha yake ni bora kuliko shilingi.

JIFUNZE JIBU LA SIJUI

Hakuna atakaye kufunga au kukuadhibu kama utasema hujui.
Kama kitu au jamabo Fulani hulifahamu usipate shida ,kuleta ujuaji kitu usicho kifahamu.
Wapenzi wajuaji wanaongoza kuleta migogoro katika maisha yao ya mapenzi.Achana na tabia ya ujuaji.

JAWABU LA KIMYA

Watu wenye hekima wamekuwa washauri wakuu wakituasa ,juu ya upole na jawabu la kimya.
Mambo yanapoenda mlama katika maisha ya mapenzi , kuna wakati mwingine jibu la kuwa kimya laweza faa.
Ukikaa kimya utaponya ndoa yako ama uchumba wako kuliko ukifunua kinywa chako.
Chunga sana maneno yako.
Kupitia maneno yako waweza okoa na kuhuisha,  na kupitia maneno yako pia waweza kuharibu,Bali jibu lako la kimya laweza kuwa na nguvu zaidi.

Kitakacholeta furaha yenu katika mahusiano yenu ni mitazamo yenu ikibadilika.
Mungu awe nanyi katika mahusiano yenu mnapo amua kufata kanuni hizi hapa juu ,nilizo wapendekezea.


BARIKIWA.


MUNGU NI PENDO.

No comments