Kabla ya kumuuliza Mungu kwanini hajakupatia mtoto,,Soma hapa
Kabla ya kumuuliza Mungu kwanini hajakupatia mtoto hembu anza kwa kumuuliza kwanini amekupatia miguu? Wewe ni nani hata uweze kutembea wakati kuna wengi hawawezi! Kabla ya kumuambia Mungu kwanini hajakupatia kazi hembu muulize kwanza kwanini alikupatia macho, mbona kuna vipofu wengi tu mtaani? Wewe ulimfanyia nini Mungu mpaka akakupa macho na hao wengine kuwanyima!
Kabla ya kulia kwa Mungu kwanini hajakupatia mume au mke mpaka sasa hivi hembu jaribu kulia na kumuuliza Mungu kwanini umenipatia hivi viungo vya uzazi, mimi ni nani? Mbona kuna wanaozaliwa kila siku wanalazimika kutobolewa mashimo kwenye matumbo yao ili kuweza tu kutoa mkojo na haja kubwa na si kama wewe ambaye unavyo mpaka unatafuta mume au mke, wao walikosea nini na wewe ulifanya nini mpaka kupata ulichonacho.
Najua hutafanya hivyo wala sikuambii usimuombe Mungu kwa hitaji lako, yeye ndiyo mwenye nguvu na anaweza kukupa vyote hivyo. Lakini nakukumbusha tu hembu kabla hujaanza kulalamika na kuomba kile unachodhani kuwa ni kikubwa, angalia vile Mungu alivyokubariki bila hata kumuomba, angalia ukubwa wake na anza kumshukuru Mungu kwa hivyo ulivyonavyo.
Furahia baraka ulizonazo sasa kwani ingawa Mungu hafanyi kama sisi acha kuwa kama yule mtu anayepewa msaada wa milioni na kuanza kulalamika kuwa aliyempa msaada ana roho mbaya kwani hakumpa na elfu kumi yakutolea! Huwezi kuwa na furaha katika maisha yako kama kila siku wewe ni kuangalia vitu ambavyo huna wakati una vingi vyenye thamani kuliko hivyo unavyoviomba!
Comment “AHSANTE MUNGU” kama kuna kitu angalau kimoja cha thamani alichokupa bila wewe kumuomba.
No comments