Mapenzi ya Mitandaoni. Soma Ukweli Huu
Katika mitandao ya kijamii unatakiwa kujua kuwa hakuna mwanaume hata mmoja aliyeoa na kama yupo basi lazima atakuambia kuwa mke wake ana matatizo na anakaribia kumuacha. Ninachotaka kusema hapa nikuwa, kama ulikutana na mwanaume katika mitandao ya kijamii, hembu jaribu kumjua nnje ya mitandao, asilimia kubwa ni waume za watu na anapokuambia yupo bize na kazi,a kakutajia likazi flani ambalo linamfanya kuwa bize baada ya kutembea na wewe ili asikuone tena basi jua kuwa unadanganywa.
Niwanaume wachache sana katika mitando watakuambia nina mke au mpenzi wangu, hivyo ukikubali uongo wake wakati Mungu alikubariki na kusoma hapa basi jua kuwa na wewe una matatizo. N
arudia hata kama mshaonana na huyo mwanaume na akakupeleka kwake, lakini kama kila kitu unachokijua kuhusu yeye ni yeye kakuambia, hakuna hata kitu kimoja ulichokijua wewe bila kuambiwa na yeye basi jua kuwa unadanganywa, acha kuahirisha maisha yako kwaajili ya huyu mtu.
No comments