BARUA YA MSALITI. (Black valentine).
Isome barua yangu ukiwa ni mwenye furaha japo maandishi ni yenye maumivu, ikumbuke siku ya faraja niliyokupa mateso mpaka ukasahau jina la upendo nakukumbuka machungu ya mapenzi.
Kuhifadhi maumivu ni udhaifu wa binaadamu mwenye kuujali upendo, ni heri niwe katili kuliko kuwa mfariji mwenye maumivu.
Upokee moyo wako wenye mateso, nirejeshee wenye upendo, sitamani kupendwa tena, walionipenda wanatosha.
Upokee moyo wako wenye mateso, nirejeshee wenye upendo, sitamani kupendwa tena, walionipenda wanatosha.
Nimekuwa mfariji kwenye maumivu yako, ukanitumia kama kilaka wa majeraha yako, nilihatarisha maisha yangu pasipo kujali ukatili wa mpenzi wako. Yote nitimize furaha yako, mbona yangu hukuitimiza?.
Umenifanya msaliti kwa aliyenipenda, ukaisaliti pete yako, ukamuumiza mwenzako, hukujua kuwa anastahili kupendwa?
Unapofurahia mapenzi yangu jua yupo anayeumia kwa kuukosa upendo wangu.
Unapofurahia mapenzi yangu jua yupo anayeumia kwa kuukosa upendo wangu.
Nimepoteza sifa ya kuwa baba bora na mwenye upendo kwa familia yangu kwasababu yako, huruma yangu ilinifanya niingie mapenzini pasi kujua ni hatarini.
Mwanangu nitamfunza nini kuhusu upendo ikiwa baba yake nimepoteza sifa ya mapenzi bora? kizazi cha usaliti kinaanzia kwenye malezi, uwongo na kutokupenda, siitaki sifa hii imuingie mwanangu.
Mapenzi bora yaanze nami, niwe mfano wa kudumu mbele yake kwamba yapo mapenzi ya kweli kwa kumpenda mama yake,
Najua barua yangu itakuumiza nakuniona nisiye naupendo kwako, kabla ya kunihukumu jiulize kama nawe unaupendo kwa mwenza wako?
Kama nawe unaupendo kwa mwanamke mwenzio?
Kama nawe unaupendo kwa mwanamke mwenzio?
Mapenzi hayana mwalimu bali yanawafunzi wasioelewa kuhusu upendo, nami ni miongoni mwao, ni heri nisikupende ili nijifunze kumpenda mke wangu aliyekuwa na roho ya uvumilivu kwa mateso yangu.
Hakuwahi kunisaliti japo nimewahi kumsaliti, hakuwahi kukusaliti japo umewahi kumsaliti, tutasemaje tunapendana ikiwa wote ni wasaliti? Tutasemaje tuna upendo ikiwa tunawaumiza wanaotupenda?
Barua hii ni ya usaliti wa mapenzi yangu kwako, barua hii ni mwanzo wa mapenzi yangu kwa mke wangu.Nampenda.
THIS IS THE BLACK VALENTINE.
(0658247651)
No comments