Breaking News

Fashion & Style Tips: MAMBO HAYA YANAKWAMISHA WENGI KATIKA KUBORESHA MUONEKANO WAO (Sehemu ya 1)



Image may contain: 2 people


1. Uzazi
Kuna baadhi ya wanawake wakishazaa huanza kujikataa wao wenyewe wakiona kwamba miili yao imepoteza ule muonekano mzuri waliokua nao kabla ya uzazi. Hata hivyo, mwanamke ukijiamini na kufanya yanayostahili mwili wako utakaa vizuri.
Pia kuna maarifa ya uvaaji hata kama umejifungua au upo mjamzito na bado ukawa na muonekano mzuri sana.
-Pichani nipo na binti yangu wa miezi sita, Camilla.
2.Kuiga
Ukiangalia mwenzako alivyopendeza nawe ukaiga mtindo wa nguo , nywele au viatu si mara zote utakua sahihi. Nguo , nywele na hata viatu wakati mwingine humpendeza mtu kuendana na aina ya umbile la mwili wake, umbile la sura yake , kimo chake , rangi ya ngozi yake, ukubwa au udogo wa miguu yake, na bila kusahau namna alivyo mix vitu vyote alivyovaa.
Hivyo basi, unaweza ona nguo fulani imempendeza mtu fulani, wewe ukaenda kuitafuta kama hiyo na usipendeze na hata wewe mwenyewe usijikubali.


Ndio maana ninatoa huduma ya personal styling, yaani kukuwezesha wewe uwe na muonekano mzuri wewe kama wewe bila kuiga wengine. Na hata kama utapenda uvaaji wa mtu fulani, nitakushauri namna bora ya kufanya muonekano huo uendane na wewe.
3.Mahusiano/Ndoa
Mwingine eti kwakua tayari ameolewa au anae mpenzi haoni tena haja ya kupendeza kwakua eti apendeze kwa ajili ya nani wakati tayari ana mwenyewe. Kumbuka haupendezi tuu ili uonekane na watu. Kupendeza kuna mchango kubwa katika kujiamini kwako na kujitambua. Kupendeza kutakufungulia milango mingine kama utajenga muonekano unaendana na malengo yako ya kimaisha.
4.Mazingira na watu wako wa karibu
Kuna mazingira yanaweza kukuchangia usiwe na muonekano mzuri kama utafuatisha kila wazo na maneno ya wale wanaokuzunguka. Kuna wanaoogopa kuwa na muonekano mzuri kisa atatafsirika kuwa hajatulia au anatafuta wanaume.
Kuna wanaoogopa kupendeza kisa eti wataonekana wamefanikiwa kiuchumi hivyo watapata maadui na hata kuandamwa na watu watakaotaka kuwakopa au kuomba msaada. Epuka watu wanaokujaza Imani zisizokuboresha. Jiamini na tambua kupendeza huanza kwa ajili yako, na kupendeza sio lazima uwe na mpenzi, au uwe unafanya mtoko Fulani . Na pia sio lazima utumie pesa nyingi kupendeza.m
Ufanye nini basi ?
Unaweza kuanza kuboresha muonekano wako leo, kwa kutilia maanani mambo ambayo unahitaji kubadili na kuongeza.



No comments