Breaking News

KWANINI MAHUSIANO AMA NDOA ZA SASA ZIMEKOSA MAANA HALISI YA UPENDO WA DHATI🎁


Swali hili pengine na wewe ni miongoni mwa wengi wanaojiuliza🤔
Kuzuka 🔥 Kama tabia fulani miongoni mwa jamii ya sasa, Mahusiano ama ndoa nyingi zinapatikana kwa SABABU💯
Kwa ulimwengu wa sasa wengi wanajitazama wao katika malengo yao na ndipo wachague anayeendana na matakwa yake NJE YA UPENDO kwamba uwe na sura ya nyani ama sura ya bin adam kama una kitu umepata mwenza😂
Wazuri wanatumika kusababisha starehe ya Mtu, iwe wakike beautifully girl 👧 na huna kitu utabakia kwa matumizi ya bin adam, Uwe wakiume handsome boy 👦 na six pack yako ila huna hela wewe bwana wasaidie wenye pesa zao kumaliza kilanga cha Mama huyo📍
Mbaya wa sura mwili wallah kama una pesa wewe YOU SO NICE 👍
Na hapo ndipo utanielewa wazi kwa sasa;
👉🏼 USIJIVUNIE UZURI WAKO ILA TAFUTA PESA IKUPE UTAKACHO💉
Mwanamke mzuri unampataje huna hela?
Mwanaume Mzuri unampataje huna hela?
Ukimpata ujue wewe ni kwa sababu wala sio kwa mwenendo wa sasa, Wengi wanaingia kwenye ndoa kwa ajili ya kusimama ki maisha kwamba mke ama Mme atafanikisha ndoto zake, Kwa nguvu na akili zake amekata tamaa ndo maana akatafuta atakayempandisha atakapo, Mara zote ndoa za aina hiyo WANAKUSANYA MALI TU ila hawawezi kuwa kwenye mfumo halisi wa UPENDO
Waliofurahia na kuwa na AMANI kwenye ndoa zao ni wale hata hawana kitu lakini wanapata japo mahitaji yao na kupanga kutengeneza MOMENTS "nyakati"
Ndoa nyingi zinapoingia migogoro mada kuu ni KUGAWANA WALIVYOCHUMA💯
Ni nani aliwekeza zaidi ya Mwingine na je nguvu kazi ni ya nani?
Hizo ni zile ndoa zinazotawaliwa na SABABU lakini kwa wale wenye NDOA ZA UPENDO WA DHATI wakiingia migogoro mara zote hujadiri kuhusiana na MOMENT walijenga UPENDO.
Na ndoa hizi huwa hazifi mioyoni ila huleta utenganifu peke yake.
Mpe mtu MOYO wako ikiwa nae MOYO wake ni dhaifu kwako huyo mtaweza kutimiza maana halisi ya UPENDO WA DHATI 💪🏼
Mali zinaweza kupitwa na wakati ukatamani kuwa na matoleo mapya, Shamba laweza lisilete mazao, Gari litapitwa na fashion lakini kamwe UPENDO WA KWELI HAUNA UCHAKAVU ni wewe na mwenza wako kuhakikisha mnailinda DHAMANA YA PENDO LENU🎁
Hata ukiwa mbali nae hataacha kukukumbuka, ila hawa watu wanakuja kwa sababu zao za ki maslahi hao hata ukimpa kisogo tu ANAKUZOMEAAAAA🗣
#Elista_kasema_ila_sio_Sheria 🔨
Image may contain: one or more people


No comments