PENZI LA GIZA SEHEMU YA 10 MWISHO
PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 10 KATI YA 10
*******
*******
Maji ya mto huo yalizidi kuwapeleka Donald na Hassan baada ya Landrover kupinduka na wao
kutokea nje ya vioo na kutua ndani ya maji yaendayo kasi sana, yaliwapeleka na kufanya wagote kwenye gogo kubwa huku wakipigwa na Maji hayo,
wakiwa wameumia sehemu tofauti tofauti za miili yao, hakika Mungu alikua bado akiwatetea alikua bado akiwalinda kutoka mikononi mwa Wachawi wale wabaya, walijaribu kuvuta kumbu kumbu zao na haraka kutoka nje ya Mto huo ambapo ilionekana walitokea mbali sana,
Nguvu ziliwaishia kutokana na kupigwa na maji hayo pia kutokuweka chakula kwa kipindi kirefu sana tumboni mwao.,
kulisha kucha tayari na jua kuonekana walianza kutembea bila kujua wanapoelekea kwa wakati huo, walimkumbuka Mchungaji Mlaki na kutokuelewa atakua na hali gani kwa wakati huo.
Safari ilizidi kusonga mbele kuelekea wasipo pajua, kila mtu aliye waona kupitia sura zao ilionesha tosha kuwa ni wendawezamu kabisa,
walikua na manywele marefu na kucha za kutisha, walingiia ndani ya msitu na kutafuta mti wenye matunda na kuanza kula, ivyo ndivyo ilivyo kua kila siku, kulivyo kucha kesho yake waliomba msaada wa gari la mkaa linaloenda Morogoro na kupewa msaada huo wakiwa wenye furaha sana.
****
SIKU YA NNE SASA mama Donald hakuonekana nyumbani wala sehemu yoyote Maria alishaanza kuingiwa na hofu alimuulizia kila sehemu mpaka kwa majirani, akimtafuta dada yake kipenzi, ilibidi tu wanyooshe moja kwa moja mpaka kituo cha polisi kutoa taarifa ya upotevu wa dada yake, alimuomba sana mungu amlinde,
bila kujua dada yake Imani yake ilimponza na sasa hivi yupo kuzimu akiteseka sana, hakua na la kufanya Zaidi ya kufunga na kumuomba MUNGU BABA WA MAJESHI aliye juu mbinguni aweze kumuonesha dada yake alipo,
siku iliyo fuata alienda kutoa taarifa kwa mchungaji Nathaniel ivyo waumini wote walitangaziwa ili waweze kumuombea Mama Donald aweze kupatikana waliamini jambo hilo kwa Mungu litawezekana,
kwa sababu hakuna lishindikanalo chini ya jua akiwemo yeye, waumini wote baada ya kupewa neno kutoka kwa mchungaji Nathaniel siku hiyo ya jumapili asubuhi misa ya kwanza saa moja na nusu.
“fungua yeremia 33;3-4”
Kila muumini alishika biblia yake na kuanza kutafuta mistari hiyo
“NIITEE, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua, Maana bwana Mungu wa Israel asema hivi, katika habari za nyumba za mji huu,na katika habari za nyumba za wafalme wa Yuda,zilibomolewa ili kuyapinga maboma na upanga. BWANA YESU ASIFIWE SANA”
“Ameen”
Waumini wote waliitikia kisha Mchungaji Nathaniel kuanza kutafsiri neno lile alilolisoma ki undani Zaidi huku akitembea tembea madhabauni, pembeni yake aliketi mke wake mama mchungaji huku yeye akizidi kushusha neno la Mungu, mmoja wa watu walikuwepo ndani ya kanisa hilo siku hiyo alikua ni Pamela ilikua ni kama kitu kilimvuta kwenda katika kanisa hilo asubuhi hiyo na kujumuika na waumini wenzake na yeye kusali pia.
Baada ya hapo waliimba nyimbo za kusifu na kuabudu kisha maombi yalianza kushushwa pale pale kwa sauti kubwa sana., huku wakizidi kutaja jina la Donald na MAMA YAKE.
****
Donald na Hassan walisha fika mkoani Morogoro na kuanza kutembea huku na kule wakiomba misaada mbali mbali, ghafla mbele yao ilipaki NISSAN PATROL na mwanamke mzuri wa kisasa kufungua kioo cha mbele na kuwaomba waweze kuingia ndani ya gari, kwa kuwa walihitaji msaada hawakuwa na kipingamizi chochote kile.
“naitwa Queen, sijui ninyi wenzangu”?
“mimi naitwa Donald huyu Hassan”
“nimeamua kuwa saidia sababu nimewaona tangu kule mnavyohangaika”
“tunashukuru Sanaa dada ila sisi tulikua tuna omba tufike Dar es saalam”
“hilo ondoeni shaka kabisa, mimi mwenyewe nilikua na safari hiyo baadae, twendeni kwanza kwangu na baadae nitawapeleka, ina bidi mpate kwanza chakula muoge sawa”
Shukrani waliyo mpa mwana mke huyo hakika haikuelezeka kabisa, walijawa na furaha sana mioyoni mwao, gari liliondoka na baadae kufika mpaka kwenye jumba kubwa la kifahari ambapo nje kulikua kuna magari mengi ya kifahari waliingia na kupewa nguo nyingine kisha baadae walipelekwa saluni kupunguza nywele na kucha zao, na kurudi katika hali yao ya kawaida,
Wakiwa seblen wana kula chakula cha mchana ghafla walihisi upepo mkali sana una vuma na kuanza kuingiwa na hofu nyingi, mbele yao walimuona Queen akibadilika sura na kuwa na sura ya Roshban ilionesha dhahiri kabisa walishanasa kwenye mtego wake.
“ha ha ha ha ha ha ha ha ha, kamwe hamuwezi kuni kimbia mimi ndiye Malkia wa kuzimu ha ha ha ha”
Alicheka malkia Roshban na kuwanyooshea vidole, kilicho fuata hapo Hassan na Donald walidondoka chini na kiza kinene kutawala ndani ya macho yao,
****
Kilicho washtua zilikua ni ngoma zilizokua zikipigwa na wachawi wakisherekea kuwapata watu walio watafuta kwa siku nyingi sasa, na kupanga siku hiyo hiyo wakatwe ndimi zao,
“MAMA”!
Donald aliita baada ya kumuona mama yake mbele yake amefungwa kwenye mti mkubwa, pembni alikua amesimama mzee Deuji baba yake mzazi na pamela,
japo kua ilikua mchana lakini waliweza kufanya mambo yao baada ya kuomba kibali kwa mkubwa wao aliye kuzimu waliye muita Mungu au Lusifa, ivyo aliwapa nguvu za kutosha kabisa,
Wote walifungwa kwenye miti mikubwa na ngoma kuendelea kupigwa huku wachawi wengine wakiwa wenye furaha sana,
Kisu kikali kilitolewa na malkia Roshban kutoa agizo moja tu wamuanze mama Donald kumkata ulimi wake, alipakwa dawa ya pumbazo kisha baadae ulimi wake kutolewa nje, ila kila mtu huyo alivyotaka kumkata ulimi alihisi kuishiwa nguvu na kudondoka chini,
alisimama tena na kujaribu ila alidondoka chini tena bila kuelewa nini kilichosababisha aishiwe nguvu.
“nini wewe fanya haraka”
Aliamuru Malkia Roshban, na kukichukua kisu kile ila kabla ya kufika aliona mwanga mweupe sana ukiwamulika,na tetemeko kubwa la ajabu sana na kushindwa kuelewa nini kinatokea,
huku kwa mbali wakisikia jina kuu la YESU KRISTO na kuwafanya waanze kuungua na moto, wote walidondoka chini,
Mwanga ule mkali uliwafanya Donald, MAMA YAKE pamoja na Hassan wayafumbue macho yao kwa mbali sana,, kwa macho yao waliweza kuona watu wawili wakiwa na mabawa yanayong’aa mithili ya dhahabu huku katikati yao akiwemo Mtu mmoja ambaye haraka haraka walimtambua alikua ni Yesu kristo wa Nazareth, na kushindwa kuelewa nini kinachoendelea.
MAOMBI NDANI YA KANISA LA MCHUNGAJI Nathaniel yalizidi kupamba moto sasa, alizidi kunena kwa lugha huku waumini wengine wakilitaja jina la yesu kristo na kulia machozi, ilionekana kabisa ndani ya kanisa hilo roho mtakatifu alishuka,
katika hali ya kushangaza watu tisa walidondoka mbele ya madhabau na kufanya wale wasiokua na Imani kuanza kukimbia mbio ndefu,
Ila Mchungaji Nathaniel alisimama imara na kuzidi kutoa maombi.
“ha ha ha ha ha ha”
Alicheka Roshban kwa sauti kubwa baada ya kutokea kanisani na kumnyooshea kidole cha kushoto mchungaji Nathaniel na kutoa kama radi ambalo ili mrusha upande wa pili,
malkia Roshban aliwageukia waumini na kutoa meno yake yaliyokua marefu sana, na kufanya waumini waanze kukimbia na wengine kudondoka chini pale pale.
Mchungaji Nathaniel alisimama tena lakini Roshban alirusha radi na kufanya idunde baada ya kuweka biblia mbele yake, radi lile iligonga biblia na kumrudia Roshban na kumtupa pembeni.
“katika jina la Yesu, huna mamlaka juu yangu, shindwaa katika jina la yesu,”
Mchungaji Nathaniel alizidi kulitaja jina la yesu wake hapo alipo sababu alijua huyo ndiyo ngao yake dhidi ya mwanamke yule aliyekua mbele yake akirusha radi kali sana…
Upepo ulizidi kuwa mkali sana mithili ya kimbunga maombi yalizidi kupamba moto ndani ya kanisa la mchungaji Nathaniel Gabriel aliyejawa na roho mtakatifu ndani yake,bado alizidi kulitaja jina la yesu kristo wa Nazareth na kumuomba Mungu Baba wa majeshi aliye juu mbinguni ili aweze kutenda miujiza mahali pale,.
Mke wake nayeye alisimama sasa imara na kuanza kusaidiana na mume wake kukemea na kumuomba Mungu,taratibu malkia Roshban alianza kuishiwa nguvu na kuanza kuwashwa huku akijibadili vitu vya ajabu, alikua akijibadili sura tofauti za watu na wanyama mbali mbali, baada ya muda mchache alitulia chini kimnya bila kuongea chochote kile.
Mchungaji Nathaniel alichukulia kama huo ni ushindi alimshukuru sana Mungu kisha kuanza kuomba tena.
“Da.a…d”
Pamela aliye kua ndani kanisani alionesha kustaajabu sana hakuamini alichokiona mbele yake, hakuamini baada ya kumuona baba yake mzazi akiwa amevalia kibwaya huku akiwa na irizi kiunoni mwake,
hiyo ilionesha tosha kuwa baba yake ni mchawi hakuelewa wenda anaota au kile anachokiona ni cha ukweli, alimtizama mwana ume mmoja ki umakini sana, moyo wake uli mlipuka na kupigwa na ganzi, hii ni baada ya kumuona Donald mpenzi wake ambaye aliamini amekufa siku nyingi zilizo pita leo hii ana muona mbele ya madhabau, hakuelewa ni kitu gani kimetokea mpaka watu wale kutokea mbele, alisimama na kuji pangusa kisha kuanza kutembea kwenda mbele ili ahakikishe kama ni kweli kwa kitu ana chokiona.
*****
“unasemaje gari limepata ajali, kivipi, nani alikua ana endesha, subiri nakuja”
Ilikua ni sauti ya Erick Deuji akiwa ofisini kwake baada ya kupokea taarifa kuwa gari ya baba yake hammer III imepata ajali na imekua light off haiwezi kurudi katika hali yake tena,
kabla ya kupiga hatua alipokea simu nyingine kutoka kwa mama yake, kuwa nyumba yao ya oysterbay inaungua moto na kumfanya azidi kuchanganyikiwa kabisa, hakuelewa ni kitu gani kina tokea.
Aliingia ndani ya gari na kulitoa mbio, baada ya kufika nyumbani kwao oysterbay hakuamini baada ya kukutana na moto mkubwa sana ulikua ukiteketea na kuunguza kila kitu,.
Mama yake alilia sana kwa uchungu hakuelewa kuwa mali zile za kichawi zinateketea na muda mfupi watarudi katika hali ya umaskini wa kutupa sababu mpaka dakika hiyo walisha pokea simu nyingi kuwa vitega uchumi karibia vyote vimeteketea moto kabisa,
Hii ni baada ya tu ya Mzee Deuji kupokea maombi, ki ukweli hawakuelewa kuwa wakati huo yupo kanisani ana pokea maombi na kuunguzwa na moto wa yesu.
“yes naongea na nani”?
“mimi hapa pascal bosi, ile kampuni ya mafuta imelipuka yote,”
“unasemaje pascal”?
“kampuni ya mafuta imelipuka yote na pesa zote zilikua ndani bosi, chanzo cha moto hakijajulikana bado”
Erick alikua ni kama amechanganyikiwa sasa hakuelewa ni kitu gani akifanye kwa wakati huo, mpaka jioni inafika hawakubakiza kitu chochote kile,
pesa zilizokua kwenye account zilipotea na vitega uchumi vyote vilikua vimeungua moto.
Katika akili zao walijua mzee Deuji yupo nje ya nchi na ndivyo alivyo waaga lakini haikuwa ivyo,
Baada ya nyimbo za kuabudu kuisha wainjiristi walianza kujisogeza mbele wengine walitoa kanga zao ili kuwafunika wachawi waliokua uchi wa mnyama, kila kitu kilikua shwari Pamela na Maria walisha fika mbele kumtizama Donald,
“Daaa….d”!
Alimtizama baba yake kwa macho yaliyojawa na upole ndani yake,
Mzee Deuji aliona aibu sana mbele ya binti yake hakuelewa ni kitu gani afanye, ukweli wa mambo ulisha onekana sasa, hakua na namna ya kufanya zaidi ya kuomba msamaha mbele ya binti yake huku akilia machozi,
Ki ukweli aliona aibu sana kuliko siku zote za maisha yake. Watu waliomjua walishika midomo yao, watu waliomuheshimu walistaajabu sana kumuona mtu tajiri kama Yule na mwenye heshima zake kujishirikisha kwenye ushirikina.
Walisali sara ya toba kanisani mule,na kila muumini kumshukuru Mungu.
“Donald nakupenda sana”
Aliongea Pamela na kumkombatia mwanaume huyo na kufanya kanisa lianze kupiga makofi na kushangilia ushindi.
BAADA YA siku kadhaa Donald alisharudi katika hali yake ya kawaida, alimshukuru sana Mungu na kuamua kuokoka kabisa, walirudi katika mahusiano yao na Pamela kama kawaida,
Hakukua na haja ya kuweka tena siri kuhusu swala la mimba kwa PHD Grayson ilibidi tu amwambie ukweli, bila kinyongo alikubaliana na hali na kuamua kurudi ENGLAND hakua na hila sababu ya kisomo chake, hakua na sababu ya kulazimisha mapenzi.
Mzee Deuji alifirisika vibaya sana laiti ungemuona usingethubutu kusema kuwa huyu ndiye aliyekua bilionea wa miaka ya nyuma , hali yake ilikua mbaya sana kila aliye muona alimnyooshea kidole, lakini sasa hivi alishaamua kumpokea yesu kristo awe kiongozi wa maisha yake akihudhuria semina mbalimbali na kutoa ushuhuda wake .
Donald alirudi katika masomo yake kama kawaida na baada ya kufudhu, alifaulu vizuri na kuchaguliwa na kupewa udhamini wa kusomea nchini INDIA. kama kanisa walimshukuru Mungu na kumpa mchango, Mtoto wao mdogo Samson alishaanza kutambaa sasa,
Ilikua furaha sana kwa wawili hawa.,
“Pamela mpenzi wangu nina kuhaidi nikimaliza tu masomo yangu, nakuja kukuoa”
Alizungumza Donald wakiwa uwanja wa ndege wanaagana siku hiyo, kwa pamela ilikua ni kama pigo kutenganishwa na Donald japo aliamini kuwa ipo siku atarudi na wata funga ndoa, yote alimuachia Mungu, Mama Donald na Maria na marafiki wengine wa karibu walimuaga kisha baadae kila mtu kurudi makwao hii ni baada tu kuona ndege tayari imeshapaa angani.
Mtoto Samson alilelewa sasa katika misingi imara ya kidini ya kumuogopa Mungu, alishaanza kujua kuita Mama waliishi vizuri kwa upendo na mama yake Donald hapo sinza , ilikua kila siku ipitayo kwa Mungu ni lazima aongee na Donald,
Siku hiyo alikua mwenye furaha sana baada ya kupokea simu kuwa Donald anarudi, aliweka kila kitu sawa na kuvaa nguo zake haraka haraka,
jioni ilipofika alinyoosha mpaka uwanja wa ndege,
Moyo wake ulilipuka kwa Furaha na kumrukia Donald na wote kudondoka chini na kuwafanya watu waliokua maeneo hayo wawashangae pengine walionekana kama ni wenda wazimu kabisa,
Furaha ili zidi kutawala nyumbani hapo,Donald alikua teyari kashamaliza masters ya ukandarasi, baada ya siku chache aliajiriwa katika kampuni kubwa hapo Dar es salaam,alipokea pesa nyingi sana baada ya kulimaliza jengo la MUNGANGA entreprises kampuni ya wazulu, cha kwanza kukifanya ni kumjengea mama yake mzazi nyumba kubwa ya kifahari maeneo ya mbezi beach, na kumnunulia gari la kutembelea,
Na baadae zilianza taratibu za ndoa walifanya mambo yao taratibu sana aliwachukua wazazi wa Pamela pamoja na Erick na kuwatafutia nyumba nyingine nzuri, hakua na kinyongo kabisa juu ya watu hawa, ilikua ni lazima asahau yaliyopita kama maandiko ya kwenye biblia yanavyosema, alisahau mabaya yote waliyo mfanyia hapo nyuma,
Siku za ndoa sasa zilikua zina nukia mambo yalipelekwa haraka haraka ni baada tu ya kununua nyumba kubwa ya kifahari Kimara, alimshukuru sana Mungu, na kuongeza upendo kwa Pamela na mtoto wao samson .
***
Watu walizidi kufurika ndani ya kanisa la assemblez of God lililokua Mwenge ili kushuhudia harusi hiyo kubwa sana, mamia na maelfu ya watu walikua kanisani hapo,
Waumini wote walisimama baada ya kuwaona Donald akiwa ndani ya suti nyeusi na Pamela akiwa ndani ya shella kubwa wakiwa wana pita kuelekea madhabauni,
walitembea taratibu sana wakiwa wenye nyuso zenye furaha muda wote,
Pamela alitokwa na machozi ya furaha, alikua aamini kama leo anafunga ndoa na wapo kanisani hakutaka kabisa iwe ndoto,
“Donald nakupenda sana”
Alinong’ona Pamela masikioni mwa Donald bila mtu yoyote kusikia.
“Mimi zaidi yako mke wangu mtarajiwa”
Walitembea taratibu huku wakiwa wameshikana mikono yao tayari kuwa bibi na bwana saa chache zijazo, tarumbeta zilisikika kila kona. kanisa lilijawa na furaha sana.
Mchungaji Nathaniel alisoma neno kisha baadae pete zililetwa na kuvalishana.
“hivi sasa mmekua mwili mmoja kama maandiko yanavyosema nendeni mka…Paaaaaa paaaaa”
Ulikua ni mlio wa bastola uliosikika kwa sauti kubwa sana na kufanya hofu kutanda ndani yakanisa hilo, watu wanne waliojificha nyuso zao waliingia ndani ya kanisa huku wakiwa na silaha mikononi.
Ilipigwa risasi nyingine juu na kufanya waumini wote walale chini, hata kwa mchungaji Nathaniel ilimbidi alale chini.
“wote ivyo ivyo kama mlivyo,Pamela kuja hapa”!
Kauli hiyo ilimshtua Donald, na kufanya apigwe na butwaa hakuelewa ni kwanini siku yake ya furaha ina katishwa,
Donald alipigwa na kitako cha bunduki na kudondoka chini alivyojaribu kusimama alitandikwa risasi ya beganina kudondoka chini huku akiwa na maumivu mengi sana. kisha watu waliojivika matambala usoni, kutokomea na Pamela nje, waliingia ndani ya gari na kuondoka zao mbio.
Akili yake ilicheza kama umeme japo alikua na jeraha la risasi mkononi mwake alisimama kiume na kumpokonya funguo mpambe wake Everest Mfugale na kuanza kukimbia kutoka nje ya kanisa,
Waumini walishaanza kuzagaa huku na kule kila mtu akitafuta mlango wa kutokea ili wanusuru nafsi zao,mambo yalishaharibika tayari,!
Ilibidi Donald afanye jambo ili mke wake kipenzi arudi mikononi mwake na wala sio vinginevyo, alitembea taratibu mpaka ndani ya gari lake RANGE rover sport na kuingia ndani huku bado mkono wake ukiwa unavuja damu nyingi,
Maumivu aliyosikia mkononi hakuweza kuya fananisha nayale anayo yapata ndani ya moyo wake, kama kungekua kuna kipimo basi moyo wake ndio ulikua ukimuuma sana baada ya Pamela kuchukuliwa na watu asio wafahamu,
Tayari Alisha piga gia na kutoka mbio kuelekea upande wa chuo kikuu akizidi kufukuzia gari aina ya CHASER nyeusi ambapo ndani yake alikuwepo Pamela ametekwa,
alizidi kuyapita magari mengine na sasa kuwa na gari hilo nyuma yake, akijaribu kulipita lakini majambazi hao ilibidi wakae kati kati ya barabara ili wasimruhusu Donald apitishe gari lake mbele yao,
Alizidi kutembeza gari na kukunja kulia na kutoka kwenye bara bara ya lami sasa kuingia ya vumbi bado Donald alikua makini kula nao sahani moja,
mpaka mmoja wa majambazi alipofungua kioo cha gari na kuanza kurusha risasi na kupasua kioo chambele cha gari la Donald kilicho msaidia, niyeye baada ya kulaza kichwa chake chini nakufanya chenga chenga za vioo kumdondokea,
Kilicho sikika baadae ni mlio wa tairi kupasuka baada ya jambazi huyo kupiga tairi la mbele la range rover spot na kufanya lipoteze uelekeo wake na kuhama kisha kuingia kwenye miti mingi,
Kwa mbali sana aliweza kuliona gari la majambazi lina tokomea na kushindwa kuelewa nini afanye, hakuelewa ni nani aliyekatisha ndoa yake, bado alikua na maswali ya kujiuliza ndani ya mtima wake, ambayo hakuweza kuyapatia ufumbuzi.
***
Msako ulizidi kuendelea bado wakimtafuta Pamela kila kona ya mji bila mafanikio yoyote yale Donald alishachaganyikiwa alizidi kuwa sumbua polisi juu ya wapi walipo fikia.
“kijana una uhakika hauna ugomvi na mtu yoyote Yule”?
“hapana sina ugomvi na mtu yoyote Yule”
“haiwezekani jaribu kufikiria tena”
“nimesema sina..lakini nime kumbuka kitu, kabla ya huyu mwanamke kurudi kwangu alikua na mwanaume mmoja ana mahusiano nae….”
“ndio ndio enhee”
“baada ya hapo tukarudiana, nina mashaka nae naweza nika sema ivyo”
“tutajie jina lake na anapoishi”
“anaishi nchini England anaitwa Grayson Mallewo”
Meja Kabogoza alizidi kuchukua maelezo ya Donald huku akiyaandika juu ya karatasi maalumu katika kituo cha polisi Relini Mwananchi,
maelezo yale yalikua yana umuhimu sana kwake, aliunga unga matukio kisha kumruhusu Donald akapumzike sasa ili yeye aanze kufanya uchunguzi wa kina!.
“napenda kukuhakikishia kuwa mkeo atarudi, nenda kakae na amani”
“sawa afande”
Donald alirudi ndani ya gari akiwa bado na ogo mkononi mwake lililosababishwa na kupigwa risasi siku yake ya harusi.
Mtoto wake mdogo Samson alikua akilia kila siku ya Mungu, japokua alikua mdogo alijua tu kuna kitu hakipo, nacho ni Mama,!
Baada ya siku chache PHD Grayson aliitwa Tanzania na kutiwa nguvuni mara moja ili ajibu mashtaka yaliyokua yakimkabili, walijua ni kwa njia moja au nyingine ndiye aliye husika na utekaji nyara!.
“mbona siwaelewi, siwezi kufanya kitu kama hiko mimi”
“hapa hatujaja kuigiza sawa kijana, tunataka kujua Pamela yuko wapi, usitupotezee muda wetu”
“sijui mnaongelea nini, ki ukweli siwezi mimi kufanya kitu kama hiko, ili iweje labda, ?your wrong, you have got a wrong person oh My God! why would I kidnap her. If there is someone out there who is real trying to kill Pamela you need to stop wasting your time here with me and find them (haupo sahihi,mmemkamata mtu asiyehusika oh Mungu wangu kwanini nimteke Pamela, kama kuna mtu mwingine huko anayetaka kujaribu kumuuwa Pamela mnatakiwa msipoteze muda wenu na mimi muwatafute “
Aliongea Grayson kwa sauti ya chini kabisa kwa upole.
“anasemaje huyu, wewe ume muelewa,ana tutukana huyu kidinapa ndiyo nini, analeta dharau hapa, sasa subiri”
Maaskari wale walisemezana bila kuelewa alichokua akiongea PHD Grayson sababu ya kiingereza chake cha kuyang’ata maneno kama mzungu, ivyo maaskari wale walichukulia kama dharau,
Hakuna kilicho fuata hapo zaidi ya kumpiga Grayson nakuanza kumtesa ili aseme wanacho taka kujua kutoka kwa mwanaume huyo, ndani ya dakika kadhaa alikua teyari keshalowa damu mwili mzima,
Lakini bado aliendelea kuongea kile kile na kufanya kipondo kizidi kuendelea tena kuzidi, yalikua ni mateso ambayo hakuwahi hata kuyafikiria na kumfanya apige kelele nyingi za maumivu anayo yapata hapo.
***
Kwa Mbali sana aliweza kuhisi kuna muungurumo wa gari na kisha mlango wa gari kufungwa, ndani ya chumba alicho wekwa kulikua kuna giza totoro na kufanya asiweze kuona hata kilichokua mbele yake
Aliweza kusikia minong’ono ya watu, lakini sauti ya mmoja wa watu waliokuwa wakiongea aliweza kuitambua japo hakuwa na uhakika nayo kama ndiye yeye.
Alimkumbuka Donald wake wakiwa kanisani wana funga ndoa na kutokuelewa kama wenda atakua hai au wapi alipo,
Parakacha za watu zilisikika na mwishowe mlango aliokua amefungiwa yeye ndani kufunguliwa, aliwaangalia watu waliosimama mbele yake,
bado hakuweza kumtambua hata mmoja wa watu waliokua mbele yake.
“mna taka nini na nyie ni akina nani”?
Alihoji Pamela akiwa chini amefungwa kamba kwa nyuma,hakika hata yeye hakuelewa kwanini yupo mahali pale, ki ukweli hakuwahi kumkosea hata mtu mmoja jambo hilo lili mshangaza sana.
“sisi tuna fuata maagizo tu,”
Walimvuta Pamela na kuanza kumpeleka mbele huku wao wakiwa nyuma yake,bado alikua mwenye hofu nyingi akizidi kulishangaa jumba hilo lililokua kubwa sana,
hakuelewa ni wapi alipo.
“Pamela”
Sauti hiyo ilimshtua sana na kugeuka kuangalia juu ya ngazi hakuamini mtu aliye muona, hakuamini kuwa mtu anaye muona hapo ndiyo amesuka mipango yote,
na kumfanya hofu izdi kumtanda.
**
Bado Donald anazidi kulisumbua jeshi a polisi juu ya walipo fikia mpaka dakika hiyo, alionekana ni mtu aliye changanyikiwa sana, dalili zilionesha kabisa uwezekano wa kumpata Pamela ulikua ni asilimia arobaini tu, sababu mtu waliye mtia nguvuni PHD Grayson bado hakuelewa kile kina choendelea, licha ya kusema maneno hayo yote lakini haikufanya aachiwe huru, ilikua ni lazima alisaidie jeshi la polisi kwa sababu huyo ndiye mtu pekee waliye mshuku,
Walizidi kumpa mateso maabusu huku wakizidi kumuhoji maswali mengi tofauti, Donlad alitoa pesa nyingi sana ili tu jeshi la polisi waweze kumtafuta Pamela, mwanamke wa maisha yake.
Hata yeye pia alihisi ni lazima atakua PHD Grayson na wala siye mtu mwingine, siku hiyo asubuhi na mapema aliwasha gari mpaka kituoni Relini Mwananchi kisha kushuka,
Aliingia kituoni na kutaka kujua kuwa walifikia wapi juu ya msako wao huo. Ila majibu waliyo mpa bado hayakumridhisha kabisa.
“kwani Grayson yeye hajaongea mpaka sasa hivi”?
“hapana bado ana kanusha”
“embu naomba niongee nae anaweza akaniambia”
“sawa hakuna tabu nifuate”
Askari huyo aliongoza mbele na Donald nyuma yake mpaka ndani ya chumba kidogo chenye harufu nzito na giza hafifu, kilichoitwa maabusu kisha kuingia,
“Grayson, ngoja nisipoteze muda, Pamela yuko wapi, naomba uniambie haina haja ya kuwekeana ligi Yule mwanamkeni mke wangu, sikatai una mpenda lakini haina haja ya wewe kufikia huko”
“Donald siwezi mimi kufika huko, siwezi kufanya kitu kama hiko, siwezi, nilikua England sasanitawezaje kufanya kitu kama hiko?”
“ngoja nikwambie kitu kimoja, Pamela akipata matatizo, au akiuwawa huko alipo ni lazima utaenda jela, unadhani ni nani ninaweza kumshuku kama sio wewe”
“sidhani kama upo sahihi kwanini nifanye kitu kama hiko kwa mtu ninae mpenda”?
“sasa sikiliza nikwambie, utaendelea kukaa humu mpaka pale utakapo sema alipo Pamela”
Donald alisimama na kuongea akionyesha hasira za waziwazi na kufanya macho yake yawe mekundu tayari, haikuwa rahisi kwake kuyaamini maneno ya Grayson MALLEWO hata kidogo, alitoka nje ya maabusu na kuwaambia maaskari wazidi kumtesa Grayson mpaka pale atakapo sema ukweli wa mambo.
***
Mzee Deuji pamoja na mke wake ilikua kila siku ya Mungu lazima wamtafute Donald kumuulizia juu ya wapi alipo fikia ila ilikua ni kama wana mtonesha kidonda, wote walimdondokea yeye na kumuona ndiyo kila kitu kwao, sasa alishakua tajiri mwenye jina kubwa sana,
“mwanangu ume fikia wapi”?
Alihoji mzee Deuji siku hiyo baada ya Donald kufika kwa mzee huyo seblen.
“bado sina cha kusema Baba, ila kama nilivyokwambia wame mtia nguvuni Grayson”
“mimi nina mashaka nae vile vile, hakuna mtu mwingine atakae weza kufanya tukio kama hilo, niyeye tu,”
“hata mimi pia nilisha waza sana juu ya hilo”
“lakini mwanangu una uhakika kuwa haukuwahi kuwa na ugomvi wowote ule na mtu mwingine, ukiachilia Grayson maana isije ikawa tuna msingizia tu”
Alihoji Mama Pamela akiwa amevalia tenge lake kubwa baada ya kuyasikilizia mazungumzo hayo.
“sidhani Mama, sikua na ugomvi wowote ule”
****
“Okaka”
Aliita Pamela baada ya kuona sura ya mwanaume mweusi kiasi, mrefu, kumbu kumbu zake zilirudi haraka sana nyuma na kukumbuka huyu mwana ume alikua ni raisi wa chuo kikuu cha UDSM na ndiye huyo aliye sababiasha ugomvi mkubwa sana kati yake na Donald kipindi wana soma miaka mingi iliyopita,
na ndiye huyu aliye mwingilia kimwili baada ya kumuwekea madawa ya kulevya kwenye juice kisha kumpiga picha za utupu wakiwa wamelala chumbani, na kufanya picha zile zizue ugomvi mkubwa sana na Donald.
“nashukuru umelikumbuka jina langu mpenzi wangu”
“nani mpenzi wako”?
“mimi hapa Okaka, bado nakupenda nataka nifunge ndoa nawewe”
“mpuuzi wewe, si nilisha kwambia siku taki tena, nampenda Donald wangu, niache niende zangu”
“ha ha ha ha ha, huendi popote pale, kwanza hongera alafu na pole vile vile, nilimuona baba yako kwenye magazeti, tuachane na hayo hongera kwa kupata mtoto, najua anaitwa Samson nisingependa awe mbali na sisi, nataka nitume vijana wangu wamlete hapa tuje tuishi kama familia”
“okaka, naomba usimguse mwanangu”
Pamelaaliongea kwa hasira sana kitendo kwa kutekwa nyara, kumbu kumbu zake alizirudisha tena kanisani na kumuona DONALD akiwa chini amelala amepigwa risasi mwenye maumivu makali sana.
“alafu pia kitu kingine, hivi kwanini tusimuuwe na Donald ili maisha yawe murua, sababu Yule ni kama mzuka amefufuka alikua kasha kufa, sasa nataka tumuuwe ki ukweli ukweli akapumzike ahera”
Alizumgumza okaka akiwa mwenye maneno yenye kumaanisha kinywani mwake kabisa, sababu alitoa simu yake na kuanza kuwaeleza watu wake ni jinsi gani ya kumpata Donald ili wamvamie kisha wamuuwe na wamchukue mtoto mdogo Samson.
“yaaa mumuuwe na pia muniletee mtoto wake”
“sawa mkuu hatutofanya makosa hata kidogo”
Sauti ya upande wa pili ilisikika ikiwa loudspika na kufanya ipenye ndani ya masikio ya Pamela na moja moja kuufanya moyo wake ulipuke, aliangua kilio na kuzidi kumsihi okaka asifanye jambo hilo,
lakini kwa okaka aliona kama ni kituko sababu alicheka kwa dharau tena kwa sauti kubwa sana
***
Donald alizidi kutoa maagizo kwa askari hapo kituoni wazidi kumshushia kipondo kikali Grayson Mallewo tena safari hii alizidi kutoa vitisho vikali akiwapa askari wale masaa machache tu ili mwana mke wake apatikane, bila kujua alikua ndani ya giza nene, kauli hiyo iliwafanya askari wazidi kushusha kipondo cha mbwa mwitu kwa mwanaume huyu mpole asiye kuwa na hatia hata kidogo,
laiti kungekua na uwezo wa kuufungua moyo wake wajue kilicho kua ndani yake wala wasinge thubutu kuendelea kumpiga vilivyo.
Kipigo kiliendelea lakini bado hakikuzaa matunda, na kufanya wamuamishe kituo na kumpakiza ndani ya defender mpaka kituo cha kati urafiki kilicho fahamika kwa kuwa na maaskari magwiji waliobobea kutesa binadamu wenzao bila huruma.
**
GARI aina ya rav 4 nyeusi ilikua nje maeneo ya mbezi beach Msakuzi, nje ya geti kubwa lenye rangi nyekundu, ndani ya gari alishuka mwanamke mrefu kidogo mwembamba na kijana mmoja na kulisogelea geti hilo, mwanamke huyo alibonyeza kengele baada ya muda kidogo alikuja mwana mke mtu mzima.
“wewee ndiye Mama Donald”?
“ndiye mimi karibuni”
“ahsante sana”
Watu wale waliingia ndani kiurahisi kabisa na kunyoosha mpaka ndani ambapo baada ya kutupa jicho chini walimuoma mtoto mdogo anatambaa huku akishika hiki na kuacha kile.
“nyie ni akina nani”?
“ni wafanya kazi wenzake na Donald, siku nyingi sana tulikua mkoani sasa, akatuambia tuje hapa ndipo mwanae Samson anaishi, kutokana na matatizo aliyokua nayo sasa hivi hatukuweza kuonana nae. Ametuambia tuje japo kumsalimia mtoto wake”
“karibuni sana, karibuni mimi ndiye mama yake huyu ndiye mjukuu wangu, anaitwa Samson ndiye mtoto wa Donald”
Kama hesabu, walikua teyari wameshapata jibu kichwani kitendo cha Mama Donald kufunguka ilikua ni kosa la jinai, tena kitendo cha kuwakabidhi Samson nayeye kuelekea jikoni, ilikua ni kama kumuachia fisi bucha.
Haraka haraka walitoka na mtoto wa Donald Samson na kunyoosha mpaka nje kisha kuingia nae ndani ya gari lao na kulitoa mbio.
“Bosi tunae mtoto hatua ya kwanza teyari, sasa usiku tutaenda kwa Donald kum-mmaliza”
Aliongea kwenye simu mwanamke huyo jambazi huku akiwa na Samson mkononi akilia kwa sauti.
Close
KAY-STALLION
· May 29, 2015 ·
PENZI LA GIZA…(39)
MTUNZI…EMMANUEL F. KWAY
Contact..+256756 322432
ILIPOISHIA
Haraka haraka walitoka na mtoto wa Donald Samson na kunyoosha mpaka nje kisha kuingia nae ndani ya gari lao na kulitoa mbio.
“Bosi tunae mtoto hatua ya kwanza teyari, sasa usiku tutaenda kwa Donald kum-mmaliza”
Aliongea kwenye simu mwanamke huyo jambazi huku akiwa na Samson mkononi akilia kwa sauti.
SONGA NAYO.
“mnanitesa bure, mimi sielewi chochote”
Alizungumza PHD Grayson huku akiwa analia machozi na kuonekana mateso aliyo yapata yamemchakaza vilivyo,
hakua na namna ya kuongea kingine ili jeshi la polisi liweze kumuamini kuwa yale maneno anayoongea kutoka ndani ya moyo wake yana ukweli.
Bado walizidi kumtesa sana sasa mpaka kuchoka unge bahatika kumuona usingedhani kama ndiye huyu aliyetoka ng’ambo siku chache zilizopita,
usinge weza kuamini kua huyu ni daktari mwenye PHD kichwani mwake,
Damu zilimvuja kila mahali,
“mimi naona huyu ni kiburi sana, akakalie chupa osterbay polisi”
“embu tuendelee kumpa kipondo kesho asubuhi tumpeleke tumkabidhi kwa Sirgent Msumai, nina uhakika ataongea kila kitu, kule sio pa kuchezea kabisa”
Walisemezana maaskari hao huku mikononi mwao wakiwa na virungu,
baada ya mazungumzo hayo kuisha tu, walianza tena kumshambulia vibaya sana, hawakuwa na huruma juu ya binadamu mwenzao,
ilimradi wamesha kula pesa nyingi kutoka kwa Donald kuwa mpaka atakapo sema ukweli ndipo aachiwe huru, ivyo hawakuangalia utu waliangalia pesa tu,
hawakujua kuwa wapo kwenye giza nene, hawakujua kuwa wana mtesa mtu asiye na hatia kabisa.
Walichukua pasi yenye moto mkali na kumuwekea mgongoni mwake, PHD Grayson alipiga kelele nyingi sana za maumivu huku akiwa mwenye kutia huruma, lakini kwao waliona kitendo kile ni kama kichekesho sababu walicheka na kuzidi kuikandamiza pasi ile yenye makaa ya moto ndani yake,
na kufanya mgongo wa Grayson kujichora pembe tatu yenye alama nyekundu,
Mateso yalizidi kuwa makali mno mpaka jioni hiyo PHD Grayson Alisha poteza fahamu zake kutokana na watu hao waliomtesa sana!.
Baadae saa moja jioni Donald alipaki gari pembeni kituo cha polisinakushuka akitaka kujua tu jeshi la polisi lime fikia wapi, juu ya msako wao.
“bado hataki kusema”
“au mnacheka nae, subiri basi nimchukue mimi nimpeleke kule jeshini akapewe mateso, mpaka atataja huyu”
“atasema tu haina haja ya kumpeleka huko kambini”
“naona hamfanyi kazi, siku nyingi zime pita hamjanipa jibu la kueleweka”
Alizidi kuwapa vitisho askari hao, ila kabla hajakaa vizuri simu yake ya mkononi iliita baada ya kugundua ni mama yake mzazi aliipokea na kuiweka sikioni,
hakuamini baada ya kusikia taarifa mbaya za kupotelewa na mtoto wake Samson, haraka haraka aliwasha gari na kutoka mbio mpaka mbezi ili akahakikishe kama kuna ukweli juu ya taarifa zile alizozipata,
Alivyo fika tu nyumbani kwa mama yake bila kusalimia alitaka kujua ilikuaje,
Taratibu kiupole mama yakealianza kumuhadithia mchana wa siku hiyo, walivyokuja watu wawili wakidai kuwa ni wafanya kazi wenzake kisha baadae kuondoka na Samson,
Donald alihisi kuchoka sana alikaa mzima mzima kitini na kuweka mikono yake kichwani akiwa amejawa na mawazo.
“ni lazima hawa watakuwa watu wa Grayson, laikni nime mkosea nini huyu mwanaume, lazima atakua yeye”
Aliwaza Donald na kuinuka kitini bila kusema chochote kile, hisia zake zilimpeleka moja kwa moja kwa Grayson tu,
hakuweza kuwaza tena nje ya boxi alijua ni lazima atakua anamtaka Pamela na mtoto mdogo Samson,
Histroria aliyohadithiwa na Pamela kuhusu kumsingizia Grayson mimba aliyobeba, vilianza kupita ndani ya medulla oblongata yake na kuanza kuunga unga matukio na kupata jibu kamili,
Aliwasha gari usiku huo huo na kunyoosha mpaka urafiki kituo kidogo cha polisi na kutaka tena kuongea na Grayson Malewo,
bila kipingamizi aliingia kwa hasira zote na kumkata jicho kali lenye hasira nyingi sana.
“naona umeamua kutuma watu sasa,”
“Do…na..ld sikuelew… kabi..sa”
“usinifanyie maigizo mimi, nipo siriazi, nirudishie familia yangu ili niishi kwa amani na furaha,”
“na..omba.. niach…ie huru mimi.. sihusi..ki na lolote li…le, unanite..sa tu bure”
Bado Grayson alijitetea na kuongea ukweli wakewa mambo tena kwa taabu nyingi, ila licha ya kuongea hayo yote ya moyoni haikumuingia akilini Donald.
“askari nigee bastola yako”
“yanini Donald”?
“nipe bastola yako”
“hapana siwezi kukupa, nitaenda kinyume na sheria”
Donald alikabwa na hasira na kufanya aheme juu juu, akimkazia macho yake Grayson Mallewo aliyekua mbele yake amejawa na damu nyingi, mwili ume mvimba kila sehemu,
Alimtizama Donald kwa shida sana na maumivu mengi sana, moyoni mwake hakuelewa atumie njia gani ili aweze kumueleza ukweli juu ya kile alichokua nacho moyoni.
“mwanangu ametekwa, wewe ndiye ume mteka mtoto wangu,ametekwa nyumbani kwa mama yangu, niambie sasa hivi Gray, niambie ni wapi familia yangu ilipo?”
Ilibidi Grayson akae kimnya anyamaze sababu aliamini kuwa hata angesema chochote asingeaminika kabisa, ukweli aliouongea sasa haukuaminika tena, ilimbidi tu amuangalie Donald aliyekua akifoka mbele yake huku akipiga piga meza.
Alitoka nje kwa jazba na kuingia ndani ya gari lake na kuegemea usukani huku akilia kwa uchungu sana,
**
Alistaajabu sana kumuona mtoto wake mdogo mbele yake aliyeitwa Samson, hakuelewa walimpataje, alibaki tu akilia huku akimkimbilia mwanae aliyeletwa na watu asiowajua,
Pembeni yake alisimama Okaka akiwa anatabasamu sana baada ya kuletwa mtoto, alimtizama Pamela kwa macho yaliyoonekana yana jambo Fulani ndani yake.
“sasa bado Donald kufa, mpigie simu Thomas, muulize ni wapi alipofikia”
Simu pale pale ilipigwa na kuweka loudspika na upande wa pili wa simu kusikika vizuri kabisa iliyokua yenyemkwaruzo wa hali ya juu.
Sauti ile ilipenya masikioni mwa Pamela na kusikia kila kitu.
“usijali tupo nyuma yake hapa, yupo hapa Urafiki Big blazza karibu na manzese, kituo cha polisi, wewe unatakaje tumuuwe au tukuletee umuuwe mwenyewe?”
“ha ha ha ha ha, subiri atoke hapo kituoni haina haja ya kuniletea , mumuuwe kabisa huko huko”
Kauli hiyo kutoka kwa Okaka ilimfanya Pamela aangue kilio na kudondoka chini kwa magoti akimuendea okaka alipo kua amekaa kitini amekunja nne,
“As…kari naomba si,,mu.. yako”!
Alizungumza Grayson akiwa kwenye hali ya mateso mengi sana aliongea kwa shida alihisi maumivu mengi mwilini mwake, aliamini kuwa matesohayo hayatoisha na wangeendelea kumtesa pengine hata kuupoteza uhai wake.
“wewe simu ya nini”?
“si mn..ata.ka.ku…jua ukw..eli”?
“ndio, wewe simu ya nini”?
“na..taka nimpigie mtu ali..yemteka Pamela”
“kumbe kweli, shika simu hii”
Phd Grayson alipokea simu na kubonyeza namba kwenye simu ile, na kuanza kuongea kireno, hakuna hata askari mmoja aliyeelewa nini anachozungumza hawakuelewa kuwa simu hiyo iliruka mpaka barani Ulaya nchini England na kumfikia wakili wake, nia na madhumuni ilikua aje nchini Tanzania ili aweze kumtetea,
aliamini kabisa askari hao wanaenda kinyume na sheria hakua na jinsi zaidi ya kupiga nchini kwao simu ili aweze kupata msaada alituma anuani wapi alipo kisha kukata simu.
SIMU ZILIANZA kugongana simu ya kwanza moja kwa mojailiruka mpaka ubalozi wa uingereza nchini Tanzania na kumfikia Mr.Arron ALEXANDER ofisini kwake kuwa kuna raia wao anateswa sana, kitendo hiko kili mchukiza sana na kupiga simu kwa kamishna wa kikosi cha haki za binadamu .
kitendo cha Grayson kuchukua uraia wa uingereza na kufanya awe kabisa mtu wa nchi yao tena akiwa daktari mkubwa kiliwauma sana baada ya kusikia anapokea mateso makali nchini Tanzania,
ilikua ni lazima wachukue hatua kali za kisheria.
“Unaongea na Arron Alexander, kutoka ubalozini naomba nisipoteze muda wangu, kuna raia wetu yupo mahabusu anapata mateso, naomba mara moja aachiwe”
“ndio kwanza nasikia hizo habari kutoka kwako Mr. Alexander, jina lake nani”?
“anaitwa Graysson Mallewo ni raia wa uingereza”
“sawa subiri simu yangu”
Baada ya kukata simu Mr,ARON aliona haitoshi alimpigia simu dereva wakeaweze kuandaa gari ili safari ya kwendakituo cha polisi urafiki ianze mara moja.
Ndani ya dakika tano alipigiwa simu kuwa gari ipo tayari. Ford yenye namba ya ubalozi na bendera ya uingereza mbele yake ilianza safari yake, huku bado wakiendelea kufanya mawasiliano na watu wa Uingereza kitengo cha usalama,
Baada ya dakika ishirini Gari kubwa yenye nembo ya ubalozini ilifika kituo hiko kidogo cha urafiki na mzee mwenye mvi kiasi na kitambi aliyevalia suti nyeusi kushuka ndani ya gari na kunyoosha moja kwa moja mpaka ndani kituoni.
Askari walianza kuhaha tayari wakianza kuogopa walisha pokea fununu juu ya ujio wa mtu huyo mzito kutokea ubalozini.
“habari zenu”!?
“nzuri meheshimiwa”
“naomba nionane na IGP wa hapa”
Askari mmoja wapo alinyoosha mpaka ofisini kwa IGP na kumkuta hata yeye amechanganyikiwa.
“mkuu unaitwa”
“sikia mwambie sipo, mwambie sipo”
“sawa mkuu”
Alitoka nje na kumpa ujumbe aliopewa na IGP, kwa Alexander aliamua kupiga tena simu kwa kamishna mkubwa wa mkoa wa Dar es salaam aliyeitwa Kailembo na kumueleza kila kitu kinachotokea hapo kituoni.
“yupo ndani ila amemwambia huyu kijana wake aseme kuwa yeye hayupo, sasa mimi ombi langu naomba umpigie simu mwambie nataka kuonana nae sasa hivi”
Mambo yalikua yasha haribika tayari kama kitumbua kilisha ingia mchanga hakikulika tena, Graysonalikua teyari yupo oysterbay polisi akila mateso makali ivyo ndivyo aliyoambiwa na IGP baada ya tu kutoka ndani ofisini mwake akiwa mwenye haya usoni mwake.
“mna kesi ya kujibu nataka nifungue jalada, mimi nataka hii kesi niisimamie, nataka nimjue aliyeifungua mara moja nikirudi hapa jioni ya leo”
Gari iliwashwa mpaka Oysterbay polisi na Grayson kutolewa akiwa amechakaa sana kutokana na mateso aliyokua akiyapata na kumfanya Alexander apandwe na hasira.
***
“shuka ndani ya gari, husikii toka ndani ya gari”
Sauti hiyo nzito ilisikika kutoka kwa pande la mtu huku mkononi akiwa na bastola na kidole chake kipo kwenye kitufe kinachoitwa Trigga,
Donald hakua na ujanja zaidi ya kushuka ndani ya gari taratibu kama mwanakondoo, ilikua ni lazima asalimu amri aliyopewa na mtu mweusi aliyepanda hewani asubuhi baada ya kutoa gari lake nje.
Alinyoosha mwenyewe mpaka kwenye Pick up nyeusi na kukuta wanaume wengine watatu,
alifunikwa na kitambaa cheusi na gari hilo kuondoka, bado kichwani mwake alimfikiria Grayson ndiye ana fanya mambo hayo.
Ila ilimbidi akae kimnya na kutulia kuhofia maisha yake, gari lilitembea na kusimama, walimvuta na kumtoa nje ya gari na kumsukumiza mpaka ndani.
Baada ya kufunguliwa kitambaa hakuamini baada ya kumuona Mke wake Pamela akiwa amemshika mtoto wao mdogo Samson,
Huku watu wengi wakiwa wamemzunguka, macho yake yaligongana namwanaume mweusi mrefu kiasi alimtambua vizuri,
alimtambua sana kuwa ndiye huyo aliye sababisha ugomvi mkubwa kati yake na Pamela hakua mwingine bali ni Okaka.
Hapo ndipo alipoanza kuilaumu nafsi yake kwa kitendo cha kumtesa Grayson Mallewo akidhani ndiye aliyeiteka familia yake, alijiona ni mkosaji sana, alivyotaka kumkimbilia Pamela alishikwa na kupigwa ngumi tumboni.
“Tulia bwana mdogo, acha kukimbilia wake za watu, una kumbuka kipindi tupo chuo nilikwambia nini, nitakuja kukuua kisa huyu mwanamke, sasa leo ndiyo siku ile imetimia”
Alizungumza Okaka akitega mkono wake ili apewe bastola, Pamela alilia sana machozi huku akitembea kwa magoti mpaka kwa okaka akimuomba asifanye kitendo hiko ila haikumfanya Okaka ashindwe kuikoki bastola aliyoishika mkononi mwake na kumuelekezea Donaldaliyekua chini ana subiri siku iyo ya kufa kwake,
Alisali sala ya mwisho na kumuomba Mungu ampokee ahera au aweze kufanya miujiza ya kuitetea nafsi yake.
“okay sitaki kuukua mimi kwakua umesali sala yako ya mwisho, shika bastola hiyo hapo jiue mwenyewe,”
Okaka alimkabidhi bastola ile Donald akijiamini sana, kila mtu alikaa kimnya akiangalia kitendo kitakacho fuata hapo, Donald alijiwekea bastola ile kichwani.
“Donald.. M..me wangu usifanye i…vyo.. naom..ba tuna mtoto mdogo”
Alilia Pamela huku akisema maneno hayo
Badala ya kufyatua ile risasi aligeuza na kumuelekezea Okaka kisha kuvuta kitufe kinachoitwa triga nyuma ili kuruhusu risasi itoke ndani ya chemba na kumfikia mlengwa lakini nguvu zilimuisha baada ya kusikika mlio ulioashiria kuwa hakuna risasi ndani ya bastola.
“ha ha ha ha ha mimi sio mpuuzi nikupe bastola yenye risasi hahahaha kacha kacha”
Okaka alitoa bastola yake kiunoni na kuikoki na kumuelekezea Donald aliyekua chini amelala huku analia sana, picha ilionesha kulikua kuna kila aina ya viashirio kuwILIPOTOKA
Furaha ya Donald na Pamela ina katika ghafla wakiwa kanisani Assemblez of god wana funga ndoa yao, ni baada ya kuvamiwa na majambazi na Pamela kuchukuliwa na watu asio wajua na kumuacha Donald akiwa katika hali ya mshangao, hisia za Donald zina mtuma moja kwa moja kuwa PHD Grayson ndiye muhusika aliye fanya uvamizi huo sababu tu walishawahi kuwa na mapenzi na pemela, hali ina kua tete kabisa, anazidi kuchanganyikiwa baada ya mtoto wake kutekwa pia, bado ana muwekea mashaka PHD Grayson na wala sio mtu mwingine.
Baadaye ana kuja kujuta na kugundua kuwa aliye mdhania siye kabisa, lakini alikua teyari kasha chelewa sababu mdomo wa bastola ulikua kichwani mwake tayari kwa kuuliwa na OKAKA tena mbeleya mke wake na Mtoto wao Samson
SONGA NAYO.
Phd Grayson tayari alikua yupo hospitali ana patiwa matibabu baada ya kutolewa maabusu na kuteswa kwa kosa ambalo alijua hakulifanya yeye, ndani ya nafsi yake aliumia sana kusingiziwa kitendo hiko cha ujambazi lakini hakumlaumu mtu yoyote Yule,
ili bidi asahau tu kwa yaliyo tokea, licha ya hayo yote bado alitaka kudhihilisha kuwa yeye hakufanya utekaji, wazo lililo mjia kwa wakati huo ni moja tu, kumtafuta Pamela na wala sio vinginevyo.
“lazima nimtafute Pamela”
aliwaza na kuinuka kitandani
“Mr, Grayson tafadhali unatakiwa usubiri kidogo”
“hapana siwezi”
Alitoka mpaka nje na kupiga simu moja kwa moja kwa Detective Charles ambaye alitoka Ng’ambo kwa nia moja tu ya kufanya upelelezi juu ya kesi yake, kwa njia ya simu ili bidi amuelezee vizuri kile kilicho tokea kuhusu Pamela, hakua na haja ya kuweka kipingamiza sababu bosi wake ndiye alimtaka afanye ivyo,
waliaungana na kwendamoja kwa moja nyumbani kwa Mama Donald ili kumuhoji juu ya upotevu wa mtoto mdogo Samson, wakiamini kuwa ni watu hao watakua wame mteka pia na pamela, taarifa mbaya tena alizozipata ni za Donald kutekwa nyara vile vile!,
“kuna watu walikuja hapa ndio”
Aliongea Mama Donald kwa sauti ya chini, kila alichoongea Mama huyo Grayson alikua na kazi ya kumtafsilia Charles kila kitu kwa lugha ya kiingereza
“enheee”
“wakasema ni wafanya kazi wenzake na Donald ndo ivyo tu mwanangu”
Maelezo hayo yalimfanya Detective Charles mpepelezi wa kizungu atoe vifaa maalumu na kuanza kupuliza juu ya kiti na ukutani walipo hisi kuwa watekaji hao waligusa, baada ya hapo walichukua alama za vidole, baada ya zoezi hilo alitoa kompyuta ndogo mashine ya kuscan akitumia kumjua ni wahusika gani, haikuchukua hata dakika tano zilikuja sura tano juu ya kioo cha kompyuta ikiwemo ya Donald.
“huyo hapo!”
Mama Donald aliruka na kupiga kelele baada ya kuona sura ya mwanamke mweusi aliyekuja siku za nyuma kisha kutokomea na Samson, hapo ndipo walianza kutafuta makazi yake pamoja na namba zake za simu,
ilikua ni mitambo ya kisasa sana, ndani ya sekunde mbili walisha jua kila kitu kuhusu mwanamke huyo mpaka wapi alipo.
Hawa kutaka kufanya papala ilibidi walishirikishe jeshi la polisi na kwenda makao makuu ya mtandao wa TIGO.
“mimi ni hafsa wa polisi kutoka kituo cha kati, tuna muhitaji huyu dada ni muhalifu”
alijitambulisha askari huyo na kuingia mpaka ndani ya chumba kidogo kisha dada huyo kuingia kwenye mitambo yake, haraka haraka alipiga simu.
“Hilder Mpila hongera sana dada umejishindia pesa taslimu milioni Tano kutoka TIGO hongera kwa kushiriki mashindano yetu, kwaio una takiwa uje mara moja katika ofisi zetu hapa Postaleo hii ili uweze kujipatia zawadi yako”
“hiii jamani, siamini, uwiii jamani, nakuja sasa hivi nipo hapa Kariakoo asanteni sana jamani”
Sauti ya upande wa pili ilisikika bila kujua kuwa ana enda kwenye mdomo wa mamba, hakuelewa kuwa anasikiwa na kila mtu na kitendo cha kwenda ilikua ni lazima aingie kwenye mkono wa sheria , alikua katika giza nene hata yeye.
Baada ya dakika kumi kwa mbali walimuona anatembea na mwanamke huyo mfanya kazi wa mtandao wa TIgo alivalia tishirt yake ili kwenda kumpokea, hapo ndipo jeshi la polisi walipo mnasa kiurahisi kabisa.
“jamani kuna nini?”
Kitendo cha kuuliza swali hilo alipokea kofi kutoka kwa PhdGrayson
“Mtoto mdogo Samson yuko wapi?”
“sijui mna ongelea nini?”
“usini potezee muda”
“jamani niacheni nikachukue pesa zangu nimeshinda”
“huja shinda twende ukachukue pesa zako kituoni”
Alidakia Askari mmoja wao mweusi sana na Hilder kuingizwa ndani ya gofu.
Virungu viwili tu vili mtosha na kumfanya ataje kila kitu akiwa ndani ya defender hapo ndipo maaskari walianza kufanya mawasiliano ili waweze kwenda kinondoni kwa MANYANYA.
**
Akiwa amelala chini sakafuni alizidi kumuomba Mungu wake aliye juu mbinguni japo atende miujiza na aweze kuinusuru roho yake, hakua na ujanja mwingine, Okaka Alisha dhamiria kumuua Alisha ikoki bastola teyari.,
alimtizama Pamela aliyekua akilia machozi mengi kama mtoto akimsihi Okaka asiweze kufanya kile anachotaka kukifanya,
lakini machozi yake haya kuweza kubadili msimamo wa mwanaume huyo, hakutaka Donald aishi duniani ilikua bora wakose wote,aliweka bastola kichwani mwa Donald na kuanza kuhesabu
“Moja , mbil ta…”
Kabla ya kumalizia tatu ili avute kitu kinachoitwa Triga na risasi itoke ndani ya chemba alisikia kishindo cha mlango ukipigwa teke kwa nguvu hapo ndipo maaskari waliingia wakiwa na mitutu mikononi mwao na kuwaweka wote chini ya ulinzi,
Hawa kuwa na ujanja tena zaidi kusalimu Amri mikoni yao ikiwa juu. Pamela alimkimbilia Donald na kumrukia kwa nguvu zote huku akilia kwa furaha sana walivyogeuka pembeni walimuona PHD Grayson amesimama ana tabasamu, hakuonesha hali yoyote ya wivu!,
“Grayson naomba unisamehe, hakika nilikua katika giza nene sana, naomba unisamehe ”
Aliongea Donald kwa sauti ya chini.
“usijali Donald hata mimi ningekua wewe, ninge fanya kile ulichokua una kifanya nina imani ulikua hujui kitu, Pamela na Donald hakika mna mapenzi ya kweli,”
“sina cha kukupa Grayson ila Mungu akubariki sana”
“ahsante sana”
Wote walikombatiana kwa furaha sana. Ilibidi Grayson apige simu na kufuta kesi iliyokua ina mkabili Donald mahakamani,
Baada ya siku mbili walikua uwanja wa ndege wakimsindikiza Grayson ili aweze kundoka walikua wenye nyuso za furaha muda wote wakiwa na mtoto wao samson,
huku nyuma akiacha Okaka na wenzake wame hukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano jela kwa kosa la utekaji nyara.
“Mtoto akifikisha mwaka mmoja nataka mimi nimfanyie sherehe kubwa sana, mumlete England”
Aliongea PHD Grayson na kuagana aliwapungia mikono huku wakimsindikiza kwa macho mpaka alipo ingia ndani ya mlango wa abiria,
“unajua nini Donald mume wangu?”
Pamela aliongea na kumgeukia mume wake
“Nakupenda sana, nakupenda mno!”
Bila aibu alimvuta mume wake na kuanza kumpiga mabusu ya mdomoni huku wakiwa wenye furaha sana.
MWISHO
No comments