Breaking News

PENZI LA GIZA SEHEMU YA 9/10



PENZI LA GIZA
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 9 KATI YA 10
*******
 *******


Grayson na taarifa izo kumfikia, alifurahi sana kupewa taarifa hizo ndani ya mtima wake, alitamani
siku hiyo hiyo achukue ndege na kuruka mpaka Tanzania,
Kwa masikio yake alimsikia Pamela kuwa amekubali baaada ya kuongea kwenye simu na kukubali kua awe mume wake wa ndoa tena bila kuwekewa kisu shingoni mwenyewe alikiri ndani ya moyo wake,
Lakini siku iyo akiwa anafua nguo zake bafuni alihisi hali ya ajabu sana mwilini mwake kichefu chefu kili mbana na kukimbia mbio kwenye sink na kuanza kutapika hakuelewa ni nini mara ya kwanza, ila kadri siku zilivyo zidi kwenda hali yake ili zidi kumtisha,
Kimnya kimnya aliiingia ndani ya gari siku iyo asubuhi sana na kwenda mpaka hospitali hakuamini majibu aliyo pewa kutoka kwa Dakatra kuwa ni mjamzito,
“Mungu wangu!”
“nini?! , ndio wewe ni mjamzito”
Picha ya Donald ilianza kuji jenga kichwani na kuanza kulia machozi alielewa fika kuwa ni lazima ita kua ni mimba ya Donald na wala si vinginevyo sababu mara ya mwisho walifanya tendo la ndoa na alikua katika siku za hatari, katika ndani ya akili yake aliweza kuwaza vitu vingi sana , alielewa fika nini maana ya kuwaambia wazazi wake juu ya uja uzito wa Donald alijua wange mchukia kabisa, hakua na jinsi ya kufanya zaidi ya kutaka kuitoa mimba ile tumboni mwake, ili asiwaudhi tena wazazi wake, sasa alishaamua kuwa upande wa wazazi wake,.
“kuna uwezekano wa kuitoa hii mimba”?
“una semaje”!?
“nasema ivi, sipo tayari kuzaa, itoe”
“una uhakika”?
“ndio”
“sawa, subiri kidogo”
Daktari yule alitoka nje kisha baadae kurudi na vifaa na kumwambia Pamela apande juu ya kitanda ili waende kwenye chumba maalumu ili aweze kutoa mimba ile ambayo hakutaka kukaa nayo, hakujua roho ile kaitoa wapi , alibaki akilia machozi huku kitanda kile kikizidi kusukumizwa.

********

“Baada ya hapo, nika muona Mchungaji Nathaniel akiwa pembeni na watu wana ong’aa kama malaika, kisha baadae nika jikuta nipo hapa, sija elewa nime fika fikaje hapa,”
“enhee huko kukoje”?
“kuna tisha mchungaji, nime ona vitu vya ajabu sana, wanyama wa ajabu, huwezi amini nime muona ndugu yangu mtoto wa dada yangu Donald,ambae huku duniani tunajua kuwa amekufa. Nilivyo mwambia twondoke yeye alikataa na kukimbia, nimewaona watu maarufu wengi waliokufa wakipata mateso makali sana, ”
“kwa jina la yesu nasema kwamba huyo Donald, atashinda kuzimu nawatuma malaika wa bwana huko alipo, waweze kumkomboa, natuma Jeshi, natuma moto uweze kuwaangamiza huko , watu wana oteseka waweze kuachiwa sasa,!”
Mchungaji aliongea huku akitembea tembea juu ya madhabau, hakika alijazwa na roho mtakatifu , jina la Mchungaji huyo kweli lili ogopeka kuzimu na wachawi wote walimshindwa na kumuogopa kama ukoma, hakuna aliye thubutu hata kumsogelea, alikua na upako wa kipekee
Maria aliilia machozi juu ya madhabau hapo huku waumini wakiwa kimnya sana wakiguswa na ushuhuda ule, wengine walibaki midomo wazi, waumini walishangilia sana na kupiga makofi huku wakimshukuru baba wa Mbinguni kwa kutenda miujiza,
Wachawi wengine waliokua pale mbele waliombewa na mmoja baada ya mmoja kukubali kuokoka na kumpokea Yesu awe mwokozi wa maisha yao, huku wakitoa siri nyingi juu ya kuwa chukua watu misukule, ivyo Mchungaji Nathaniel alikua na kibarua kingine cha kuwa fufua watu ambao waliaminika wame kufa Duniani,
Waliendelea kumsifu Mungu na kusali sana siku hiyo kwa nguvu zote,

*****

“Nooo sitaki , nimeghairi daktari sitaki”
Baada ya kitanda kile kufika mlangoni Pamela alishuka na kughairi kwa kitendo alicho kua anataka kuitoa mimba ya Donald, aliamini kuwa kufanya vile ange mkosea Mungu, aliamini ange fanya vile ange mkosea Donald, aliamini kuwa mtoto atakae zaliwa ita kua kumbukumbu tosha ya kumkumbuka na kumuenzi Donald, alichomoka na kuingia ndani ya gari na kuegemea usukani wa gari akitafakari cha kufanya.
“Lazima hii mimba ailee Grayson, nisha pata wazo! Nitatunza siri hii mpaka mwisho wa maisha yangu. Ila kuhusu mtoto huyu itabaki kuwa siri yangu! ”
Aliwaza Pamela na kuwasha gari kisha kuliondoa akiwa kichwani na mahesabu ya kumsingizia mimba ile Grayson japo kua hakuelewa atumie njia gani.



WACHAWI walizidi kushuka wengi wao wakiwa juu ya nyungo huku wengine juu ya migongo ya fisi, ili kua ni kama sherehe kwao, siku ya arobaini ya kukatwa ndimi kwa watu walioaminika wame kufa duniani sasa ili wadia, kati ya watu walio takiwa kukatwa ulimi alikua ni Donalad alikua ni kama zezeta hakuelewa kinachoendelea, sababu ya dawa aina ya pumbazo aliyo nyunyiziwa, mbele yake kulikua kuna mti mkubwa wa mbuyu ambao mmoja baada ya mwingine hufungwa hapo,

kisha mwana mke aliye kua maalumu kuja kufanya kazi yake ya kukata ulimi bina damu wenzake hupita kwa kila mmoja wao na kufanya kazi hiyo. Ngoma zilizidi kupigwa huku baadhi ya misukule ikiwa jikoni wakipika nyama za watu au binadamu wenzao!, mzee Deuji muda wote alikua kayaacha meno yake nje akifurahi sana kwa kitendo kile cha Donald kutaka kukatwa ulimi wake, walifanya mambo yao haraka haraka na tayari ilikua zamu ya Donald kuwekwa kwenye mti ule ili apewe dawa kisha ulimi wake ukatwe, mijitu yenye misuli ili kwenda mbele yake na kumbeba mpaka kwenye m-buyu huo na kumfunga kamba kisha wao kukaa pembeni wakipokezana kibakuli cha damu za watu.
Mtoto wa mkubwa wa wachawi waliye muita MALKIA alikua tayari na kisu mkononi kilicho kua na makali sana na kumuendea Donald ambae muda wote alikua akitema udenda, alikua sio yeye tena nywele nyingi na makucha marefu vili yeyusha kabisa uzuri wake asilia, hakuelewa lolote lile, hakuwa na kumbu kumbu yoyote ile juu ya Pamela mpenzi

wake ambae huko Duniani anajua keshakufa tayari.
Mwana mke Yule alizidi kumsogelea kisha kumpaka dawa ila alisita kidogo baada ya kuona Sura ya Donald na kusitisha zoezi la kukata ulimi huo, hakika alionesha ni kama mtu anaye mfahamu,
Donald akiwa hajui hili wala lile Alisha utoa kabisa ulimi wake nje,
“Doooonaaa..ld”!
Mwana mke huyo aliita na kuanza kumfungua kamba, wachawi waliokua pale walianza kumshangaa na kushindwa kuelewa nini kinaendelea., mmoja wao alisimama kutoka juu ya kiti na kuweka kibuyu cha damu pembeni.
“kazi ime kushinda”?
“hapana, huyu tusubiri muda wake bado!”
“hapana, mkate ulimi”
“nimesema hivi! Muda wake bado”
Mchawi Yule alikuja pale na kukichukua kisu kile na kumsukumiza Malkia pembeni
“mshirika”!
“naam mkuu”
“mwache”
Sauti iyo nzito kutoka kwa mkuu wake ilisikika baada ya kumuona mtoto wake wa kike amkataa kitendo kile japo hakujua ni kwanini aliji kuta nayeye ana muunga mkono.
Baada ya kuwekwa pembeni misukule mingine ilifuata na zoezi lile likiendelea kama kawaida la kuwaka taka ulimi, Msukule aliye wekwa maalumu kwa ajili ya kupika ndimi alisogea karibu kisha kuchukua ndimi zilizokatwa na kuzipeleka jikoni na kuanza kuzipika, ulikua ni usiku wa kutisha sana wakati huo.!

Vigele gele vilizidi sana ila kwa Mzee Deuji alionesha dhahiri hali ya chuki, kitendo cha Donald kutokatwa ulimi kili mkera sana lakini hakua na jinsi sababu amri hiyo ili toka kwa Mkuu wake Mzee Kira.,
Kila mchawi mmoja alikua akiingia kati kucheza ngoma hiyo ya mdundiko ambayo ilikua ikipigwa na misukule maalumu kwa ajili ya kazi izo, huku wengine wakiwa uchi wa mnyama.ivyo ndivyo ilivyokua, huku duniani wengine wakililia watoto wao wapendwa au ndugu zao siku ya arobaini huku kwao ilikua ni kama sherehe kubwa sana.

“R…..oshban”!
Donald aliita baada ya kumuona mwana mke Yule mbele baada ya kupakwa dawa ya kumrudisha kumbu kumbu zake za kibinadamu, ailjiangalia makucha yake na kujiona tofauti kabisa, walikua ndani ya chumba kidogo wamejificha.
“Donald”!
“hapa niiiiiipo wapi”?
“upo mbali sana”
“mbali wapi?, Mama , Pamela, wako wapi?”
Alionekana ni kama mtu aliye rejewa na kumbu kumbu tayari, watu wa kwanza kuwa kumbuka ni Pamela na mama yake mzazi, alijiangalia mara mbili mbili kisha kuchungulia nje na kuona watu wa ajabu sana huku wenginne wakiwa wana lima, mara ya mwisho alikumbuka kuwa alikua duniani ana zikwa alimkumbuka Pamela sana ambaye alizimia na kupoteza fahamu zake,

alimkumbuka Mzee Deuji ambaye alikua akimtesa mpaka umauti ulipo mkuta, vitu vingi mbali mbali alizidi kuvi kumbuka vilivyo pita katika maisha yake, alimtizama Roshban kwa umakini sana na kushindwa kuelewa ni nini hasa kilicho tokea katika maisha yake.
Roshban alimuonea sana huruma, lakini licha ya ivyo kadri siku zilivyozidi kwenda alijikuta anaanza kumpenda Donald kimapenzi, hakua ana mfanyisha kazi tena za misukule tena ilikua kila usiku ni lazima ampake dawa ya kumrudisha kumbu kumbu zake kisha kuongea mengi sana juu maisha ya kichawi, alimueleza jinsi alivyo muokoa kwa mara ya

kwanza alivyotaka kuuliwa, na mzee Deuji na kumuokoa akiwa ndani ya Shimo wakati yeye aliichukulia kama ndoto!.
Taratibu Roshban alijisogeza kwa Donald na kuanza kumshika mashavu huku akimwangalia machoni kulikua kuna kila aina ya dalili ya mapenzi tele ndani ya macho ya Roshban!
“Roshban kama una nipenda kweli nitoe huku”
“Donald kutoka huku sio rahisi kama unavyodhani, mimi nakupenda nataka tufunge uwe mume wangu!”
“kwanini, nitoe kwanza huku”!

“sio rahisi Donald kama unavyo dhani!,”

Hayo ndiyo yalikua maongezi yao kila siku ipitayo kwa Mungu , bado Roshban aligombana na wachawi wengine juu ya kumkata Donald Ulimi swala hilo hakutaka litokee kabisa alipanga kila njama ili asiweze kukatwa ulimi wake.
Siku iyo wakiwa usiku wanawa simamia misukule ghafla alimuona rafiki yake ambaye aliletwa siku chache zilizo pita, alimuendea moja kwa moja na kumuomba SANA Roshban aweze kumpaka dawa rafiki yake huyo kipenzi ili waweze kuzungumza.
“Hassan!”
Aliita Donald na kumsogelea rafiki yake huyo, alijua nini maana ya rafiki yake huyo kuwa huko.
“nyie ni akina nani”?
“Mimi Donald,”
“Donald. Donald yupi? Hapa ni wapi?”!
Taratibu ili bidi Donald aanze kumuelezea kila kitu na kila mtu kuanza kumshangaa mwenzake, walienda kwenye chumba kidogo ili waongee,
Donald aliambiwa mambo mengi tangu wajue kuwa amefiriki dunia ulimwenguni,
“Donald mimi sitaki kubaki huku , tutafute njia ya kutoka”
“huku hatuwezi kutoka kirahisi”
“mimi sitaki kukaa huku”
Hassan aliona gongo kubwa pembeni yake na kulishika vizuri baada ya kusikia parakacha za mtu zina kuja, alisimama nyuma ya mlango na kuwa tayari kabisa kumshushia yoyote atakae ingia.
“Don…”

Roshban kabla ya kumalizia sentensi yake alihisi kitu kizito kime tua kichwani kwake na kudondoka chini mzima mzima.
Haraka haraka Hassan alimshika mkono Donald na kuanza kutoka nje na kukimbia huku wakielekea wasipo pajua ndani yam situ mzito wenye kiza nene sasa!…


Shirika la ndege la Qatar airways lililobeba takribani abiria mia tano lili kua tayari juu ya ardhi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere nchini Tanzania jijini Dar es salaam, gari maalumu lililo kua na ngazi juu yake lilikua teyari lipo mlangoni na kuweka ngazi ili abiria washuke ndani ya ndege!,
Mmoja kati ya abiria waliokua ndani ya ndege hiyo alikua ni PHD Grayson Mallewo akiwa muda wote ameyakenua meno yake nje alitamani awe wa kwanza kushuka ndani ya ndege,
ilionekana kabisa alikua na kihoro cha kumuona mwanamke aliye mpenda katika maisha yake, alisumbuka kumpata na kumkosa lakini leo hii aliambiwa kuwa amekubaliwa, kwake alidhani kua ni ndoto lakini yeye alitamani isiwe ivyo,
Taratibu alishuka ngazi akiwa mwenye furaha kisha kuingia mpaka immigration na kugonga muhuri passpot yake wa kuingia na kupita taratibu kutoka nje,,hakuamini baada ya macho yake kutua juu ya uso wa binti mzuri aliye pendeza sana, moyo wake ulimlipuka sana na kutabasamu.
“Pamela”!
Aliita Phd Grayson Mallewo na Pamela kumkimbilia kisha kumrukia kwa furaha jambo lile lili mfurahisha sana mzee Deuji akiwa pembeni yao na Erick, walifurahi sana, walisalimiana kisha kuelekea kwenye maegesho ya magari.
Safari ya kuelekea Oysterbay ilianza na baada ya dakika chache walikua wamesha fika tayari kwenye moja ya maegesho ya magari ndani ya nyumba ya Deuji ambapo walikuta chakula kitamu kilichoandaliwa na mke wake.
Walifurahi sana siku iyo,

Kwa upande wa PHD Grayson aliona mambo sasa yana mnyookea aliona mambo yana mwendea vizuri sana, ila alisikitika sana baada ya kuambiwa kuwa Donald alifariki dunia, japo mwanaume huyo alikua kikwazo kwake lakini alionesha kuguswa sana moyoni mwake.

“pole Pamela”
“nishapoa”
Waliendelea kula na kunywa huku Pamela chini ya meza akiikanyaga miguu ya Grayson huku akimtizama machoni , PHD Grayson alivyomuangalia Pamela machoni alielewa nini maana yake,
Baada ya kula aliomba kutoka wakashangae mji na Pamela, hakukua na haja ya kuweka kipingamizi chochote kile waliruhuwiwa na kupewa HAMMER III waitumie na mzee Deuji, wakiwa wenye furaha mioyoni mwao walitoka nje na kuondoka na gari.

Ki ukweli ndani ya moyo wa Pamela hakua na mapenzi na Grayson hata kidogo alitaka kumtumia awe kama mwavuli wa kuzuia mimba ile ya Donald isije ikagundulika na wazazi wake na hayo ndiyo yalikua mahesabu yake kichwani aliamini kama mtoto wa kike kazi ile ilikua rahisi kama kuweka kibakuli cha supu mdomoni.!
Aliweza kumshawishi Grayson mpaka kuingia ndani ya Hotel hiyo na kuchukua moja ya chumba kizuri sana, walikunywa na kufurahi kisha kuongea mengi sana siku hiyo, waliongea mambo yao yaliyo pita hapo kipindi cha nyuma yake!
Baada ya PHD Grayson kuingia bafuni kuoga Pamela nayeye alivua nguo zake na kuzitupa chini kisha nayeye kuingia bafuni humo, kilicho fuata hapo walifanya tendo la ndoa.

*******

Hassan na Donald walizidi kukimbia huku nyuma wakisikia jeshi la wachawi liki wakimbiza wakiwa wenye hasira sana, misukule mingine pia ilipewa kazi ya kuwakimbiza, walizidi kukimbia wasipo pajua tena bila kuona hata mbele, kutokana na giza totoro lililo kua lime tanda mbele yao huku sauti za bundi na wanyama wengine wakali ziki sikika, hawa kuwa na hofu yoyote walicho fikiria wao kipindi hiko ni kunusuru maisha yao, hawa kutaka kurudi na kuendelea kuteseka tena,!
Walijua fika kukimbia ndio suluisho pekee, ilikua bora wafe kabisa kihalali kuliko kubaki huko kuteseka, hata wakifa walijua walikua wanaya okoa maisha yao!,
“Hassan nimechoka”
“twende Donald”
“mimi siwezi”

Hassan alimvuta mkono Donald na kuanza kukimbia huku wakikanyaga miiba na vitu vyenye ncha kali, ila hawa kujali walizidi kusonga mbele.
Jeshi la wachawi lilikua juu ya anga wengine wakiwa na nyungo na fisi, kuna wengine pia walikua chini wakiwatafuta kwa wudi na uvumba huku waki apia endapo wakiwa kamata wata wafanya kitu kibaya ili iwe mfano kwa yoyote atakaye kiuka masharti ya humo.

Mzee DEUJI akiwa na hasira zilizo mjaa moyoni alizidi kuwachapa viboko misukule ile wazidi kuwa tafuta Donald na Hassan ambapo mpaka sasa hawa kujua wapo sehemu gani ,lakini waliamini kuwa wapo ndani ya msitu huo mkubwa sana, hawakukata tamaa hata kidogo, walizidi kujigawa kila kona.
Donald na Hassan Walizidi kukimbia na baadae kuteleza na kuanza kubiringika kama mpira kuelekea chini na baadae kujikuta wametulia, walikua wapo ndani ya shimo refu futi kadhaa kwenda chini, kwa mbali sana walihisi wachawi wana kuja huku wakipiga kelele nyingi,
kulikua kuna kila aina ya dalili kwamba walisha onekana ,
Jambo lile lilikua la ukweli sababu wachawi walisha fika juu ya shimo na kuanza kuchungulia kwa chini, wakiwa wanashangilia sana, kwao walichukulia kama ushindi.
“baba baba baba bababa bababa!”
Aliongea msukule mmoja wao akiwa hana ulimi akisonta kidole chake ndani ya shimo akiwa taarifu wachawi wale kuwa watu waliotoroka teyari wamesha onekana,
Nyungo na fisi vilitua chini mithili ya helikopta na wachawi wale kuanza kulizunguka shimo lile ambapo ndani yake walikuwemo Hassan na Donald wakiwa wenye hofu nyingi,
Roshban aliye fahamika kama malkia wa wachawi alitokea na kumwangalia Donald huku akimuomba apande juu ili ajisalimishe, sababu watu aliokuja nao ambao ni wachawi walikua na hasira sana.

Bado walikua wana jishauri kupanda juu ili watoke sababu walijua teyari wameshakamatwa, lakini cha kushangaza walisikia ngoma ziki pigwa huku vilimbi yenye mlio mwembamba ikianza kusikika , walitulia kidogo na kuona wachawi hao wana anza kuondoka mmoja baada ya mwingine huku wakitoa mbio, kulikua kuna kila aina ya dalili kua muda wao wa kuwanga umekwisha,

Wote walisambaratika, taratibu Hassan alianza kupanda juu huku akishika kamba kamba za majani na kuchungulia nje , hakuona dalili yoyote ile ya kuwepo kwa mtu,alishusha kamba nyingine na kumvuta Donald aliye kua chini na kumpandisha juu, na baadae wote kutoka, wote walianza kukimbia tena wasipo pajua .!

Kwa mbali sana Donald alihisi kuna kitu kina mlamba lamba kichwani, ndani ya akili yake alijua kuwa ni mnyama mkali sana alicho fanya yeye ni kutulia kimnya bila kuji tingisha akiamini akiya fumbua macho

yake ndipo hapo utakua mwisho wa uhai wake,licha ya kulambwa na ulimi ule kwa mbali alihisi kelele za watu zikija upande wake, huku wakiongea Lugha za ajabu ajabu, taratibu alifumbua jicho lake moja kwa hofu sana huku mwili mzima uki mtetemeka sana na kujihami kwa lolote litakalo tokea lakini ndani ya Moyo wake aliomba Mungu wasiwe wakawa wale wachawi , sababu aliya kumbuka sana mateso yake,

Alikutana na pua ya mbwa mkubwa baada ya kufumbua jicho lake na kushusha pumzi ndefu ya uwoga na kufanya mbwa Yule aanze kubweka, kulikua tayari kume pambazuka jua lina waka, ilikua ni maajabu sana kwake sababu ya kutokuliona jua kwa kipindi kirefu cha nyuma!, watu waliokua mbele yake wamevaa vibwaya walizidi kumsogelea pale alipo kisha kuanza kumshangaa jinsi alivyo kua akitisha, nywele zake chafu na mwenye makucha marefu sana!.
“hapa tupo wapi”?
Alimuuliza Hassan ambaye alikua pembeni yake huku wakiwa wame zungukwa na watu wale waliokua wamevaa vibwaya mikononi wameshika mishale, kupitia picha ile ilionekana dhahiri kuwa walikua wakiwinda.
Pale pale walianza kunong’onezana kila mmoja wao na kuanza kuwatazama.
“kakaka kuku kaka kuku”!

Lugha hiyo iliwashangaza sana Donald na Hassan hawa kuelewa watu wale ni akina nani ila waliwa fuata na kuwainua kisha kuondoka nao mpaka kwenye kijiji chao ambapo walioneka wote walikua wamevalia mavazi hayo hayo.
waliwapelekwa mpaka kwa mwenyekiti wa kijjij hiko kisha kuwatambulisha tangu walipo wakuta, kwa bahati nzuri mwenyekiti huyo alikua akiongea Kiswahili ila kwa mbali sana.
“mume thokea wapi”?
“Dar es salaam , hapana hatujui tulipo tokea lakini tuna taka tufike Dar es salaam”
“thawa ila ithawabidi ninyi ninyi mbake hapa mupaka asabuhe yake ndipo muende, mule chakula kwanza alafu nifanye uaaratibu wa kuongea na ndugu yangu esho ana kwenda mujini”
Babu huyo alizidi kuhiaribu lugha ya taifa.
“kwani hapa tupo wapi babu”?
“mupo Nyaminya, huku Ni Musoma bhechukuru(wajukuu) zangu!”
Donald na Hassan walitazamana na kushangaa walifikaje mpaka huko Musoma, babu Yule alizidi kuwa hoji maswali mengi tofauti, !
Baadae waliletewa chakula na mwanamke mmoja aliye valia mavazi yaliyoficha kifua chake na chini sehemu za siri ila tumbo lake lilikua wazi,
Walikula haraka haraka kuonesha kuwa walikua na njaa sana ,Baada ya kula walishukuru sana na baadae kuoneshwa sehemu ya kulala na mwanamke huyo ambaye mpaka wakati huo hawa kujua jina lake,

*******

“NIMEWAONA WAPO KATIKA KIJIJI CHANGU NYAMINYA, TWENDENI TUKAWAFUATE”
Aliongea mzee huyo baada ya kutua tu na ungo wake usiku huo na kuwaambia kuwa Donald na Hassan wapo katika kijijji chake ki upande Fulani mzee Yule alikua ni mmoja wa wachawi , haraka haraka wachawi wale walianza kupanda nyungo zao wakiwa na hasira sana huku wengine wakipanda fisi na safari ya kuelekea kuwakamata Donald na Hassan kuanza walikua na hasira sana, na kupewa vitisho kwa mkuu wao kuwa endapo wakiwa kosa watapata adhabu kali sana..



Mwanamke aliyekua akiwapa huduma ya chakula mpaka vinywaji mchana na usiku sasa alijitambulisha kwa jina la Doto,hapo ndipo alipoamua kuwaambia ukweli Hassan na Donald juu ya uchawi wa mwenyekiti wa kijiji hiko aliyeitwa Wankuru, walistaajabu sana hasa baada ya mwanamke huyo kuongea Kiswahili fasaha kabisa,

Tayari ilisha fika saa sita na dakika mbili usiku bado walikua ndani ya kibanda hiko wakijishauri namna ya kutoka, walisha ingiwa na hofu mioyoni mwao, hawakujua kama wangetoka salama ndani ya kijiji hiko wakisaidiwa na mwanamke huyu Doto ambaye aliye amua kuokoa maisha yao yaliyokua hatarini sana.
“nendeni piteni kule, mtakuta barabara ya lami kulia kwenu mtakuta nyumba nyeupe ya mchungaji, mwambie kuwa mnahitaji kwenda mjini mna matatizo, fanyeni haraka ndiyo mida ya mzee Wankuru hii”
“asante Doto, sasa sasa sasa wewe hauji?”
“nyie nendeni nimeamua kuwakoa fanyeni upesi”
“sawa sawa”
Hassani na Donald walianza kutoka mbio mbio wakienda barabara waliyoelekezwa huku bado wakiwa na hofu nyingi kwenye mioyo yao, walinyoosha moja kwa moja na kukuta nyumba nyeupe waliyoambiwa ni ya mchungaji kisha kuingia na kukaribishwa ndani,
walikaribishwa na kueleza shida zao haraka haraka walisali usiku wakiomba ulinzi wa baba wa majeshi aliye juu mbinguni na kisha kuamua kuwasindikiza mpaka mjini kwa kutumia gari yake,
Jeshi la wachawi walisha kasirika tayari kitendo cha kuwakosa Donald na Hassani mahali pale walizidi kupiga patro wakiamini kuwa hawatokua mbali, mmoja wa wachawi aliyekua na nguvu alipiga filimbi yake nyembaba na kuangalia upande wa Magharibi kisha kuwaambia wenzake wamfuate ana poenda, wote walitii na safari ya kuwasaka Donald na Hassani kuanza mara moja, hawakutaka kurudi bila watu hao mikononi mwao, ivyo ndivyo ilikvyo kua,

Landrover lilizidi kusonga mbele kwa mwendo wa kinyonga usiku huo mnene, ndani yake kulikua kuna mchungaji Mlaki huku nyuma wakiwemo Donald na Hassan wakiamini kuwa wapo katika mikono salama,bila kujua tayari jeshi hilo la nguvu za giza lipo juu yao angani likiwafuatilia bila ya hata mchungaji kujua,
Kwa mbali kulikua kuna Basi kubwa la abiria lina kuja kwa mwendo wa kasi, ilikua ni lazima wachawi wale wafanye jambo ili kuwachukua Hassan na Donald wawarudishe walipotoka,wakiamini kuwa ,mchungaji Mlaki hakua na nguvu sana za kuwazuia asifanye ivyo sababu walishawahi kumlimisha usiku na kufanikiwa, dereva aliye kuwa katika mwendo wa kasi alikua sasa akishuka mlima kwenye daraja kubwa ambapo chini yake kuna mawe makubwa sana na maporomoko ya maji.!

Kazi ya wachawi hao ilikua ni ndogo tu kumpiga upofu dereva wa Basi kubwa lililobeba abiria, jambo hilo lilifanyika, ndani ya dakika mbili dereva huyo aliyumba akiwa kwenye mteremko wa mlima mkali sana mbele yake aliona jiwe kubwa na kulikwepa bila kujua kuwa yalikua ni mazingaombwe na aliokwepa jiwe.
alienda upande wa pili ambapo hakuliona landlover linalokuja, alijikuta akiligonga na kulipandia kwa juu yake ilikua ni ajali mbaya sana ya kusikitisha, magari hayo yalizidi kubiringika huku landrover lile likizidi kujisaga kwa chini,kilichosikika hapo zilikua ni kelele za abiria wakilia na kusali sara zao za mwisho sababu gari lilizidi kuserereka kuelekea chini kwenye mawe makubwa , damu nyingi sana zilitapakaa juu

ya lami, Landrover aliyokuwemo mchungaji Mlaki,Donald na Hassan haikutambulika jinsi ilivyo haribika na kusagika, iliserereka mpaka pembezoni mwa daraja , huku wachawi hao wakiwa wenye furaha na kusogea eneo lile la ajali wakiwa tafuta watu wao.

*******

Kichomi sasa kilishaanza kumsumbua tumboni mwake ilibidi tu Phd Grayson awashe gari lake la kifahari aina ya BMW X6 alilolinunua siku chache zilizo pita asubuhi hiyo na kuondoka na Pamela moja kwa moja mpaka hospitali, huko alipokea taarifa ambazo zilimfanya atoe meno yake yote nje, kitendo cha kuambiwa kuwa Pamela ni mjamzito kilizidisha furaha yake,

alijiona pengine ni kidume kuliko wengine wote duniani, alifurahi sana na kushangilia hospitalini hapo sababu moja ya ndoto zake zilikua teyari zinaanza kutimia, ivyo alitakiwa kufanya mambo haraka haraka weweze kufunga ndoa na pamela kisha warejee nchini ENGLAND wakajenge familia bila kujua kuwa mimba aliyokua nayo Pamela sio yake ni ya Donald ambaye sasa hivi anapigania kujinusuru na watu wabaya,!
Hakusita kumwambia Pamela siku hiyo wakiwa Kilimanjaro hotel ambpo hapo ndipo PHD Grayson Mallewo alipopanga chumba tangu afike,
“sijakueewa Grayson”
“nataka tufunge ndoa kabla ya huyu mtoto hajazaliwa, ninataka huyu mtoto achukue uraia wa kule,nafikiri umenielewa hapo mke wangu mtarajiwa”
Alizungumza Grayson huku akiwa chumbani na Pamela siku hiyo,
hata ivyo Pamela aliitikia kwa shingo upande huku akitabasamu kuashiria kuwa amekubaliana na maamuzi ya mwanaume huyo,waliwasha gari wakiwa wenye furaha sana wakielekea Oysterbay , nia ya Graysoni ilikua ni kumsalimia baba yake mkwe mzee Deuji, lakini alivyo fika nyumbani hapo akulika na hali ya utofauti kabisa,
mzee huyo walimkuta anaumwa sana, alishindwa hata kuongea chochote kile, jambo hilo lina washtua sana, ilibidi daktari wake aitwe mara moja ili amuangalie bosi wake.
“ana presha tu ya kawaida, lakini mpaka baadae atakua sawa, inabidi atumie hizi dawa zita msaidia”
Maneno aliyoongea daktari huyo hayakuendana kabisa na mgonjwa huyo aliyekua mahututi kitandani kwake, hali ya hofu ilizidi kumtanda mpaka kwa mke wake aliye kua akilia pembeni yake.

*****

Mama Donald tayari alishaanza kusikia fununu juu ya mtoto wake kuwa hakufa kama alivyodhani, maneno hayo yalisha vuruga akili yake alitamani sana kumuona mwanae tena alimkumbuka sana, watu mbali mbali walikuja na kumwambia maneno hayo,wengine walimwambia amuombe Mungu sana, ila kuna wale waliomwambia aende kwa Waganga wa kienyeji,

alikua na nafsi mbili zikibishana ndani ya mtima wake, hakuelewa aichukue ipi, japo aliamini ushauri wa pili haukuwa mzuri sana kwake ,yeye alimuamini sana Mungu wake mmoja tu aliye juu mbinguni, licha ya kumuamini lakini alijiuliza kama yupo sasa mbona alimuacha ateseke,
Imani ilisha mtoka mwanamke huyu akiwa na mama wa jirani yake, alimfuata na kumuomba ampeleke kwa waganga wa kienyeji ili aweze kumuona mwanae au amfufue ikibidi, Alisha sahau kuwa kuna Yesu Kristo,
“yaani huyu mimi nina kuhakikishia mwanao atarudi niamini mimi, mimi ndiyo Mama Mwanaidi nakwambia ivyo”
“kweli eeeh, sina cha kukupa lakini ipo siku Mungu atakulipa”

Tayari ibirisi Alisha muingia mwilini akiisukuma nafsi yake, walifika Buguruni na kutafuta Mabasi yaendayo Chanika na kupanda walivyofika Chanika walichukua gari za Msata na kuzidi kuingia ndani ndani ambapo kulikua na vijiji vingi tofauti, ilikua ni safari ndefu kidogo, baada ya kushuka walipanda baiskeli na kuzidi kutokomea maporini.
“samahani tuna muulizia Fundi NDUBUSA nahisi tumepotea”
“wala hamjapotea, nyoosheni na hii bara bara, kuna nguzo pale ,mbele sasa pale mkono wako wa kushoto kuna njia nyembamba mkitembea kidogo mtaona mto wa maji nyuma yake kuna mbuyu mkubwa sasa kwa pembeni hapo ndipo kibanda chake kilipo”
“ahsante Mama”!
“msijali”
Walizidi kusonga mbele baada ya kupewa maelezo hayo , baada ya mwendo wa kiasi walifika na kukuta moshi ukifuka, waligonga kisha kuingia ndani ya kibanda hiko,na kumkuta mganga huyo akiwa na vitu kama tunguli,, hakukua na haja ya kuweka vitu ndani ya moyo, moja kwa moja walianza kuelezea shida zao kwa mganga huyo,
“Mimi ndiye Dumbusa, walisha kuja hapa watu kutoka Bukoba, Singida, Malawi ndugu zao niliwatoa walioamini walikufa hiyo ni kazi ndogo sana Mama, njoo kesho usiku wa saa mbili, ukiwa umevalia nguo nyeusi, uje na shilingi mia mbili tu,”

Mganga Yule alizidi kujinadi na kuwahakikishia ushindi wa jambo lile, kweli walirudi makwao kisha kesho yake Mama Donald usiku alifunga safari akiwa mwenyewe mpaka Msata kwa ajili ya kumuona Mganga Dumbusa.
Baada ya kufika hapo mganga Yule alianza kuongea maneno yasiyo eleweka ila katika hali ya kushangaza alianza kutoa damu mdomoni na puani, kwa mara ya kwanza MAMA Donald alijua wenda ndiyo mizimu ina fanya kazi lakini hali ya mganga ilizidi kuwa mbaya sana,

Upepo ulizidi kupuliza na kupeperusha baadhi ya vitu huku mganga Yule akiwa ameshika shingo yake kama mtu anayekabwa na kitu kooni mwake, ghafla walitokea watu wanne mbele yake wakiwa na vibuyu alivyo muangalia mmoja wa Watu hao alikua ni mzee Deuji.
“ha ha ha ha ha,! Utaondoka na sisi”
Pale pale Mama Donald alipigwa na unyoya wa jogoo usoni na kilicho fuata hapo aliona kuna giza nene na kupoteza fahamu zake palepale



Magari ya kuchukua wagonjwa teyari yalishafika eneo la ajali usiku huo iliyosababishwa na basi la abiria kugonga landrover na kuanza kupakia maiti za watu waliokufa, kila mtu aliye kua pembeni hapo alishika kichwa chake sababu ya ajali mbaya iliyotokea, ila kuna wengine walijiuliza ni kivipi magari hayo ya wagonjwa kufika kwa haraka kiasi hiko jambo ambalo lilizua maswali vichwani mwao kutokana na umbali wa hospitali,
Katika upande wa pili wa nguvu za giza hakukua na gari hata moja la wagonjwa walikua ni wachawi wakiwasaka Donald na Hassan, ivyo walianza kuwatoa majeruhi wote na kuwaweka pembeni wakiwa

tafuta watu wao bila mafanikio wala dalili yoyote ile, walimuona Mchungaji akiwa ameumia vibaya kichwani na kufa pale pale walimsukuma pembeni na kuendelea na msako wao.
Wakiwa wenye hasira nyingi sana
“hawa watakua wapi sasa”?
“endelea kutafuta kabla hakuja pambazuka wapo humu humu”
“sasa wako wapi”?
“acha kelele”
Wachawi waliendelea kubishana huku wakizidi kuwa tafuta watu wao bila kuwaona, walizidi kupandwa na hasira sana.

No comments