Breaking News

FACEBOOK CHATTING….1

 

Sehemu Ya Kwanza (1)

MSICHANA: Mambo Nyemo.MIMI: Poa. Mzima?MSICHANA: Mzima wa afya. Unafanya nini?MIMI: Nachati na friends pamoja na kuangalia muvi kwa kuibia.MSICHANA: Hata mimi nachati pia. Muvi gani hiyo unayoangalia kwa kuibia?MIMI: Message in the Bottle.MSICHANA: Mmmh!MIMI: Mbona mguno tena?MSICHANA: Hiyo muvi mpya?MIMI: hapana. Toka mwaka 1999.MSICHANA: Na mimi nataka nije kuangalia. Nakaribishwa?MIMI: Duh! Poa. Karibu.MSICHANA: Hahahaha! Inaelekea u kijana mcheshi sana.MIMI: Kitu gani kimekufanya kuhisi hivyo?MSICHANA: Basi tu. Nimejirubuni kusema hivyo.MIMI: Yeah! Hivyo ndivyo nilivyo.MSICHANA: Unaishi wapi?MIMI: Tanzania.MSICHANA: Yeah! Najua. Ila sehemu gani?MIMI: Dar es Salaam.MSICHANA: Nafahamu. Ila Dar es Salaam kubwa sana.MIMI: Naishi Tandale. Unapajua?MSICHANA: Huwa ninapita tu na gari mara chache chache.MIMI: Okey. Thats gud then.
Ukimya unatawala kati yangu na yake kwa dakika kama tano hivi, mara nasikia kamlio ka meseji kanalia, ninapoangalia, naona ni yeye. Naifungua na kuisoma.
MSICHANA: Samahani kwa kukaa kimya, nilikuwa nimekwenda kununua Chill souce dukani. Nimefurahi kuchati nawe kwa sasa. Nakwenda kupika mara moja. Tunaweza kuendelea kuchati baadae?MIMI: Usijali.MSICHANA: Utakuwa online?MIMI: Nafikiri kwa sababu sina pa kwenda.MSICHANA: Poa basi, baadae kidogo.MIMI: Poa.
Baada ya hapo anakwenda offline. Sikuonekana kujali, sikujua kwa nini msichana huyu alikuwa ameonekana kuwa karibu sana na mimi kwa kipindi hiki kichache, nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza, nikawa navuta subira mpaka katika kipindi ambacho atarudi tena online. Nikawa na hamu kumuona akirudi online na kumuuliza baadhi ya maswali ambayo yalianza kuja kwa haraka sana kichwani.
Nilikuwa na presha sana juu ya msichana huyu ambaye nilitoka kuchati muda uliopita. Niliporudi online, nikamkuta. Hata kabla sijamtumia meseji, akaniwahi.
MSICHANA: Naona umerudi.MIMI: Yeah.MSICHANA: Nimekumiss.MIMI: (Kimya)MSICHANA: Mbona haujibu chochote jamani?MIMI: Sasa ulitaka nijibu vipi hapo?MSICHANA: Kwamba na wewe pia umenimiss.MIMI: Sasa kama sijakumiss jamani?MSICHANA: Dah! Aya yaishe. Nilikuwa online muda mrefu kidogo, nilikuwa nakusubiria tu. Nilikuwa nimekwishaboreka, bora umerudi.MIMI: Usijali. Nipo hapa kwa sasa.MSICHANA: Kuna swali lolote ungependa kuniuliza?MIMI: Yeah! Tena mengi tu.MSICHANA: Kama yapi?MIMI: Unaishi wapi?MSICHANA: Mbezi.MIMI: Unajua kama zimegawanyika sehemu mbili?MSICHANA: Yeah! Nipo ya huku Beach.MIMI: Ok! Unasoma au unafanya kazi?MSICHANA: Nasoma sekondari.MIMI: Wapi?MSICHANA: St’ Mary.MIMI: Ok! Unaishi na nani?MSICHANA: Na wazazi wangu. Baba yangu mfanyabiashara na mama yangu ni mhasibu pale BoT.MIMI: Unasemaje?MSICHANA: Kwani haujanielewa jamani au unanifanyia makusudi tu.MIMI: Sawa. Nimekuelewa. Hivi ni kitu gani ambacho kimekupelekea kupenda kuchati nami na wakati ni jana tu ndio tulianza urafiki?MSICHANA: Kwa mara ya kwanza niliweza kukuona pale nilipoingizwa kwenye kundi lako la hadithi la SUSPENSE na rafiki yangu. Japokuwa sicomment wala kulike lakini nimependa sana hadithi zako. Huwa ninapenda sana kuzisoma huku nikiwa kitandani.MIMI: Sawa. Usijali.MSICHANA: Hivi itawezekana kuendelea kuchati hata kipindi ambacho hatupo online?MIMI: Kivipi? (Niliuliza japokuwa nilifahamu alimaanisha nini?)MSICHANA: Simuni.MIMI: Kwa hiyo unamaanisha unataka namba ya simu?MSICHANA: Ndio. Ila kama hautojali wangu.MIMI: Hapana. Hapa facebook kunatosha sana.MSICHANA: Ila ningependa kuisikia sauti yako wangu.MIMI: Usijali, tutaweza kutumia skype pale utakapohitaji kuisikia sauti yangu, tena hadi kuniona utaniona huko.MSICHANA: JamaniiiiiMIMI: Kweli tena.MSICHANA: Sawa.
Ghafla akakaa kimya, sikutaka kuchelewa, nilichokifanya ni kuanza kupitia picha zake. Mungu wangu! Kwanza nikajuta kwa nini nilimnyima namba ya simu, alikuwa msichana mzuri sana ambaye kwa mwanaume lijali kama mimi basi asingekubali kumuacha.
Mara nikaanza kupokea notification kwamba alikuwa akiLIKE picha zangu, yaani ilikuwa kama kero, kila wakati anaLIKE…analike.
MSICHANA: Nimevutiwa na picha zako. Na nimevutiwa na wewe pia.
Aliniambia maneno ambayo yalinichanganya.
Kwa kiasi fulani nikauhisi moyo wangu kuingia katika hali fulani hivi, najua wale ambao waliwahi kuwasiliana na wasichana kwa zaidi ya dakika themanini watakuwa wamekwishawahi kukutana na hali hii. Alikuwa msichana ambaye alikuwa wazi na wala hakutaka kujificha chochote kile. Aliniona kumvutia sana.
MIMI: Asante sana japokuwa najiona kuwa mtu wa kawaida sana.MSICHANA: Wa kawaida? Labda kwako mwenyewe. Hivi nikuulize swali la kizushi?MIMI: Uliza tu.MSICHANA: Una msichana?MIMI: Yeah! Ninao.MSICHANA: Unao?MIMI: Ndio.MSICHANA: Wangapi?MIMI: Wengi tu.MSICHANA: Kama wangapi?MIMI: Ngoja kwanza. 1, 2, 3, 4. Kwa sasa ninao hao tu japokuwa wa 5 na wa 6 nipo kwenye process za mwisho.MSICHANA: Sawa. Hongera.MIMI: Asante.MSICHANA: (Kimyaaaaa)
Kila wakati nilikuwa mtu wa kupenda sana utani pasipo kugundua kwamba wakati mwingine utani wangu unaweza kuniletea mambo mabaya. Nilikuwa nimeongea nae hayo yote kama sehemu ya utani, nikahisi tu kwamba alikuwa amekasirika japokuwa hakutaka kuongelea hilo. Hakunitumia meseji, alibaki kimya kwa muda wa dakika ishirini, nikashindwa kuvumilia, nikamtumia meseji.
MIMI: Mbona kimya tena?MSICHANA: Nipo bize.MIMI: Bize? Ubize wa nini tena?MSICHANA: Hautakiwi kujua.MIMI: Ok.
Tayari nilikwishaona kwamba nimeharibu, nilichokifanya, nami nikajidai kukaa kimya, si unajua mwanaume hautakiwi kuonyesha udhaifu kirahisi namna hiyo. Nilikuwa nikiumia sana kukaa kimya japokuwa nilikuwa nikijikaza kisabuni sana. Nikamtumia meseji.
MIMI: Nimechoka.MSICHANA: Eehh! Umechoka kufanya nini tena?MIMI: Kuwa…ok!MSICHANA: Kuwa muwazi bhana.MIMI: Nimechoka kuwa online. Nadhani natakiwa kusaign out mpaka wiki ipite ndio nirudi tena.MSICHANA: Kwa nini tena?MIMI: Sioni umuhimu wa kuwa online.MSICHANA: Kivipi?MIMI: Kwa sababu hautaki kuchati nami. Umekaa kimya sanaMSICHANA:Napenda amani Nyemo.MIMI: Nafahamu hilo. Ila unamaanisha nini?MSICHANA: Huwa sipendi kuchati na mtu mwenye wasichana wengi.MIMI: Hahaha! Nilikuwa nakuzingua bwana. Unadhani naweza kuwa na wanawake wote hao. Utani tu, naomba unizoee wangu.MSICHANA: PoaMIMI: Unafanya nini?MSICHANA: Nipo chumbani. Peke yangu huku kwa mbali wimbo wa Westlife ukisikika.MIMI: Wimbo gani?MSICHANA: As love as my witness. Unaujua.MIMI: Yeah.
Akakaa kimya tena. Kwa wakati huo kidogo nikaanza kujisikia amani. Muda wote nikawa bize kusikilizia meseji yake, ghafla meseji ikaingia, meseji hii ilikuwa imeambatana na picha moja nzuri, alikuwa amepiga akiwa kitandani huku juu akiwa wazi na nguo yake ya ndani ndio ambayo ilikuwa mwilini mwake.
MSICHANA: Umeionaje picha hiyo?MIMI: MmmhMSICHANA; Kuna tatizo.MIMI: Hapana. Ila……una nyingine tena unitumie?MSICHANA: Subiri
Akaanza kunitumia picha nyingi nyingi, picha zote zilikuwa zinanichanganya tu, nilikuwa nikiweweseka tu.
MSICHANA: Na wewe nitumie zako.MIMI: Poa.
Hapo ndipo nilipoanza kujipiga picha na simu yangu. Nilijipiga picha zaidi ya kumi huku na mimi nikiwa nimevaa boksa tu. Nilipomaliza, nikawasha bluetooth na kisha kuziweka kwenye kompyuta na kisha kumtumia.
MSICHANA: Unavutia sana. Naomba tufanye kitu kimoja.MIMI: Kitu gani?MSICHANA: Nitumie namba ya simu, nataka tufanye kitu fulani usiku.MIMI: Kitu gani?MSICHANA: Mapenzi kupitia maongezi simuni.MIMI: Mmmh!MSICHANA: Mbona unaguna? Haujawahi kufanya hivyo?MIMI: Nimewahi. Tena zaidi ya mara ishirini tena ikiwa zaidi ya masaa sita simuni.MIMI: basi naomba tufanye hivyo.
Hapo nikabaki kimya, nikaanza kujifikiria kama ilikuwa vizuri kumtumia namba ya simu au la. Alikuwa akitamani sana tufanye ngono simuni jambo ambalo nilijua lilikuwa na matatizo sana kisaikolojia. Hata kabla sijajua nifanye nini, meseji yake ikaingia, nikawa na shauku ya kuifungua. Nikaifungua haraka haraka.
Nikaifungua ile meseji, kwa wakati huu meseji ile ilikuwa imekusanya maneno mazuri ya mapenzi. Nilikuwa nikiziangalia kwa kuzisoma moja baada ya nyingine. Hazikuwa meseji ngeni kwangu, nilikwishawahi kuziona mara kibao.MIMI: Unaonekana unapenda sana mahusiano ya kimapenzi pamoja nami?MSICHANA: Ndio. Nimetokea kuvutiwa nawe.MIMI: Hahaha! Unataka nianze kuwindwa na bunduki mitaani.MSICHANA: Kwa nini?MIMI: Mvulana wako.MSICHANA: HahahahahaMIMI: Unacheka unaona mazuri?MSICHANA: Mbona unakuwa muoga hivyo? Yaani unamuogopa hadi mwanaume mwenzakoMIMI: Si kwamba namuogopa, hapana, naogopa bunduki.MSICHANA: Hahahaha! Hapana bwana. Siko kwenye mahusiano, nilikuwa na mpenzi ila tumeachana.MIMI: Chanzo nini?MSICHANA: Alikuwa anadate na rafiki yangu mmoja hivi.MIMI: Pole sana.MSICHANA: Asante sana. Vipi kuhusu wewe?
Hapo nikabaki kimya kwa muda. Kichwa changu kilikuwa kikifikiri kwa haraka sana. Hii ilimaanisha kwamba kama ningemwambia nina msichana, kwanza angeumia halafu ndio ingekuwa mwisho wangu nayeye kuchati. Huku nikiwa najifikiria nini cha kujibu, meseji yake ikaingia.
MSICHANA: Mbona kimya?MIMI: Unajua internet connection inazingua sana. Yaani mara ikate, mara irudi. Yaani tabu tupu.MSICHANA: Poleee. Naomba unijibu basi.MIMI: Ninae kwa sasa.MSICHANA: Unae?MIMI: Ndio. Ila hanionyeshei mapenzi ya dhati. Mara nyingi najitahidi kumtumia meseji, hanijibu, nikimpigia simu usiku, ipo bize tu. Tena si hivyo tu, hadi usiku wa manane ipo bize. Unahisi nini hapo?MSICHANA: Unaibiwa.MIMI: Kama naibiwa, nawe upo tayari kumuibia?MSICHANA: Una maana gani?MIMI: Hahahaha! Acha utani. Usitake nianze kutoa maana moja kwa moja hadi watu wa facebook washtukie.MSICHANA: Kama yeye mwizi, sina budi nami kuwa mwizi.MIMI: hauoni dhambi kuiba?MSICHANA: Kwenye mapenzi sidhani kama kuna dhambi kuiba. Anayeua kwa upanga nae atauawa kwa upanga.MIMI: Mmmhh! Sawa. Ila samahani kidogo. Kuna swali nataka kukuliza.MSICHANA: Kuwa huruMIMI: Unaonekana kuwa msichana wa tofauti sana. Yaani sio aina ya msichana ambaye amekulia hapa.MSICHANA: Yeah! Nimeishi sana nchini Marekani ambako huko nilikaa kwa muda mrefu sana na ndipo nikalilia kuja Tanzania.MIMI: Mmmh!MSICHANA: Mbona unaguna tena?MIMI: Hakuna bhana.MSICHANA: Vipi kuhusu namba ya simu.MIMI: Kwani unaitaka leo?MSICHANA: Ndio. Nataka tuongee leo kama nilivyokwambia.MIMI: Hivi unajua leo lini?MSICHANA: Jumatatu.MIMI: Hatutoweza kuongea kwa leo. Kesho inatakiwa niwe chuoni saa tatu.MSICHANA: Chuo gain?MIMI: Ninaposoma.MSICHANA: Kwa hiyo tutaongea lini?. Nina hamu sana ya kusikia sauti yako.MIMI: Labda Ijumaa.MSICHANA: Kuanzia saa ngapi?MIMI: Saa tano.MSICHANA: Ok! Kadri tunavyoendelea kuongea na ndivyo ambavyo ninazidi kufall inlove zaidi.MIMI: HahahahahaMSICHANA: Unazicheka hisia zangu?MIMI: Hapana. Umekuwa mwepesi sana kufall inlove.MSICHANA: Yeah! Sijui kwa sababu gani.MIMI: Labda kwa sababu una hamu ya kuniumiza hapo baadae.MSICHANA: Haiwezekani kabisa. Labda wewe ndio uniumize.MIMI: Kwangu haitowezekana kabisa. Niamini.MSICHANA: Sawa. Ila naomba unipe namba ya simu ili niwe na amani.MIMI: Usijali. Nipe yako ili nikupigie.MSICHANA: Yangu ni 0719 878 ……MIMI: Poa.
ITAENDELEA..

No comments