Breaking News

FACEBOOK CHATTING…..7

 

DORCAS: Vibaya.MIMI: Hao ndio vidudumtu kwenye mapenzi. Huwa mara kwa mara hawapendi wakuone kwenye furaha, unapojaribu kufanya hivi, wao watataka kufanya kile, utakapojaribu kufanya kile, wao watataka kufanya hiki. Waepuke sana watu hawa, huwa si wema sana, huwa ni wabaya ambao wanaweza kuharibu kila kitu.DORCAS: Mmmh! Una maneno mengi sana Nyemo. Ila ulichosema kuhusu watu hao, ni cha ukweli kabisa.MIMI: nawajua sana. Ninaposema kwamba leo nataka kukaa na mpenzi wangu niyafurahie mapenzi, wao watakasirika tu huku wakihoji kwa nini nikae na mpenzi wangu.DORCAS: Nimekuelewa. Hebu kwanza tuachane na hilo. Nikuulize swali?MIMI: Uliza.DORCAS: Unanipenda?MIMI: Sawa na kuulizia makofi polisi.DORCAS: hahaha!MIMI: Sawa na kuulizia ushungi Pemba.DORCAS: hahahah!MIMI: Ni sawa na kuulizia bunduki jeshini.DORCAS: hahaha! Acha kunichekesha Nyemo. Hebu nijibu kwanza.MIMI: kwani si tayari nishakujibu.DORCAS: bado.MIMI: Swali lako ni sawa na kuulizia mapenzi juu ya Dorcas moyoni mwa Nyemo. Nakupenda, nakupenda sana, nakupenda zaidi ya unavyofikiria, nakupenda zaidi ya unavyojipenda, ninakupenda zaidi ya marafiki zako wanavyokupenda.DORCAS: Huo umekuwa kama wimbo Nyemo. Sound nyingi.MIMI: Huu ni kama wimbo, naamini hilo. Kila siku umekuwa ukiambiwa kwamba unapendwa na watu wengi kiasi ambacho umeona kwamba neno ‘nakupenda’ kuwa kama wimbo masikioni mwako. Ila nataka kukwambia kitu kimoja. Neno hili limekuwa wimbo kwako, lakini leo huu wimbo umekuwa remix masikioni mwako.DORCAS: Unamaanisha nini?MIMI: Msanii anapotoa wimbo na kisha kutoa remix yake ina maana kwamba kuna vitu alikuwa amevisahau hakuviweka sasa anataka kuviweka katika remix yake. Hiyo ni sawa na mimi. Wengi wamekwambia kwamba wanakupenda ila kuna vitu hawajavisema kwako.DORCAS: kama vipi?MIMI: Kupendwa zaidi ya unavyojipenda. (Nilijibu, akatoa tabasamu ambalo likanifanya nimpende zaidi)
Ukinisikiliza, nilikuwa naongea kiutani sana ila kumbuka kwamba ndio nilikuwa nazidi kupiga hatua zaidi na zaidi. Nilikwishamsoma Dorcas kwa kipindi kirefu sana, hakuwa msichana wa kumwendea sana siriasi, unamuwekea utani, unamchombeza kwa maneno haya, unamfurahisha hapa, unamchekesha kule. Hiyo ndio hatua ambayo nilikuwa nikiifanya kwani nilijua kwamba kama ningekuwa naongea huku nikiwa siriasi, kumpata kwangu ingekuwa ndoto ya mchana.DORCAS: maneno yako matamu sana, yanafanana na post zako unazoziandikaga kwa facebook.MIMI: Tabasamu lako zuri Dorcas, linafanana na maneo uliyoniandikia jana kwamba unanitakia ‘FURAHA YA SIKU YANGU YA KUZALIWA’.
Siku hiyo ikaonekana kuwa siku ya furaha katika maisha yetu wote wawili, tulikula na kunywa huku tukipiga stori za kizushi mahali pale. Dorcas alionekana kuwa mwenye furaha kubwa sana kiasi ambacho hakutana nitoweke mbele yake. Tulitumia muda wa saa moja na nusu kukaa pale na ndipo tukahitaji kuondoka mahali hapo. Kwa mara ya kwanza, nikambusu Dorcas shavuni mwake jambo ambalo lilionekana kunifurahisha kupita kawaida. Ukurasa mpya wa mahusiano ya kimapenzi ulikuwa umefunguliwa mahali hapo.
DORCAS: Usiniumize.MIMI: Nami natakiwa kukwambia maneno hayo hayo.DORCAS: Naijua facebook. Japo una marafiki mia moja na kadhaa lakini unaweza kupata marafiki wengi zaidi kutokana na uandishi wako. Kuwa makini na watoto wa kike.MIMI: Usijali Dorcas. Siwezi kufanya jambo lolote baya, hasa kukusaliti wewe (Nilimwambia huku nikitoa tabasamu pana ambalo lilimfanya kuniamini zaidi).
Kiukweli tofauti na watu wengine, Dorcas sikutaka kumchezea na kumuacha, hapana, nilikuwa nikimaanisha mapenzi yale ambayo nilikuwa nimemwambia, hata kama ingewezekana, basi haikuwa budi kumuoa. Siku hiyo tukaongea mengi na hatimae kuagana. Sikutaka kuondoka nyumbani, nilichokifanya ni kumng’ang’ania kwenda naye huko alipokuwa akiishi, tukaenda na kupaona na ndipo nilipoondoka kuelekea nyumbani.
MIMI: Nitakupenda mpaka nakufa (Nilijisemea ndani ya daladala katika kipindi naelekea nyumbani kana kwamba Dorcas alikuwa pembeni yangu)
Mahusiano yale yaliendelea zaidi na zaidi, sikuachana na uandishi wa hadithi humu facebook, bado nilikuwa nikiendelea nao kama kawaida. Watu walinipenda, watu walipenda kusoma simulizi zangu ambazo nilikuwa nikiziandika katika staili ambayo ilikuwa ikinishangaza hata mimi mwenyewe. Nikazidi kupata marafiki zaidi mpaka ndani ya wiki moja kupata marafiki zaidi ya 500. Kazi ya uandishi ilikuwa ngumu sana lakini sikutaka kuiacha, bado nilikuwa nikiendelea nayo kama kawaida jambo ambalo lilikuwa likinipa marafiki wengi.
JULIET: Unajua sana Nyemo. Nafurahi sana kila ninaposoma simulizi zako, yaani kama naangalia muvi Mlimani City.MIMI: Asante. Ila kawaida tu, namshukuru Mungu kwa hiki kipaji.JULIET: Yaani kama na mimi ningekuwa najua kuandika kama wewe, ningefurahi sana.MIMI: Tofauti na kipaji, wakati mwingine ukijifunza unaweza.JULIET: Sasa mimi nitajifunza wapi?MIMI: Kupitia hadithi nyingi. Jitahidi kusoma hadithi mbalimbali. Ukiona kwamba unataka kuandika hadithi kama za Nyemo, basi penda kusoma hadithi za Nyemo, ukiona kwamba unapenda kuandika hadithi kama za Sultan Tamba, pendelea sana kusoma hadithi zake.JULIET: Na kama nikisoma hadithi za wote?MIMI: Utachanganyikiwa. Katika maisha ya mwandishi, wengi hushindwa kuandika hadithi za aina tofauti. Mungu amegawa vipaji ila kavitofautisha tu.JULIET: Kivipi?MIMI: Kuna mwingine anaweza kuandika hadithi kuhusiana na mambo ambayo huwezi kuyafikiria kabisa, mfano ninavyoandika, huwezi kujua ni staili gani ninayotumia, naweza kukuandikia vitu ambavyo havipo katika jamii ya Kitanzania, huwa ninafurahi kuandika kuhusiana na mambo ya nje, huo ndio uandishi, nazunguka duniani kote. Ila katika hili, kuna mwingine anaweza kuandika hadithi ambayo inahusu jamii inayomzunguka tu, kutoka nje ya jamii inayomzunguka inakuwa ngumu sana kwani kuandika kuhusu jamii tofauti na hizi za Kiafrika, basi inabidi Mungu awe amkupa kitu kingine cha ziada sana.JULIET: Mmmh! Umetoa maelezo marefu sana.MIMI: Hiyo ni kwa sababu unataka kujifunza.JULIET: Na mbona hauandiki hadithi kuhusiana na jamii inayotuzunguka, hadithi zako nyingi zinakwenda nje ya Afrika?MIMI: Nilikwishawahi kuandika hadithi kama Maria, mwanzo mwisho ilizungumzia maisha halisi ya Mtanzania, ila baadae nikajuta.JULIET: Kwa nini?MIMI: Huwa sipendi kuziandika hadithi hizo humu Facebook japokuwa ninazo nyingi. Humu facebook, ngoja niwe naziandika hizi hizi za kwenda nje, zile zinazohusu jamii husika ya Mtanzania, ningependa kuzifanyia muvi na si kuzirusha hewani, ndio maana nafanya hivyo. Watu wabaya wanaweza kukopi na kupaste, ili kuwachanganya, acha niwaandikie mpaka za nje, kama wana uwezo, waigize huku wakisafiri kwenda nchi mbalimbali.JULIET: Hahaha! Mtoto mjanja wewe.MIMI: Kawaida tu.JULIET: Asante kwa muda wako.MIMI: usijali.
Huyu msichana ndiye alikuwa wa kwanza kabisa ambaye alikileta kitu fulani moyoni mwangu, kitu ambacho kilionekana kuwa doa katika mahusiano yangu na Dorcas. Kwangu mimi, nilikuwa nachukulia kila kitu kuwa kawaida sana lakini kumbe mwenzangu alikuwa tofauti na mawazo yangu. Mawasiliano yangu na Juliet yalikuwa yakiendelea kama kawaida kwa njia ya inbox. Kitu ambacho kila siku alikuwa akikifanya ni kuniomba namba ya simu, sikuwa mwepesi, nilikuwa nikimyima sana ila kutokana na wadau wengi kunisumbua kwamba walikuwa wakitaka kunipongeza kupitia simuni, nikaiweka namba yangu hadharani jambo ambalo likaonekana kuwa kosa kubwa. Usumbufu ukaanza rasmi kutoka kwa Juliet,
MIMI: Unasemaje?JULIET: Sauti yako nzuri. Naweweseka kila ninapoisikia.MIMI: Ok! Usijali. Kawaida tu.JULIET: Kwani yangu sio nzuri Nyemo?MIMI: Nzuri.JULIET: Hauweweseki?MIMI: Ndio…siwewesekiJULIET: Naomba kitu kimoja kutoka kwako.MIMI: Kitu gani?JULIET: Naomba tuonane.MIMI: Haiwezekani. Nipo bize sana kwa sasa.JULIET: Hata kwa dakika kumi tu.MIMI: Hapana Juliet, nafikiri kuwasiliana simuni na facebook kunatosha.JULIET: Hapana bwana, nataka kumuona mtu ambaye kila siku anaufanya moyo wangu kufurahia. Naomba tuonane…nakuomba.MIMI: Haiwezekani. Sipo Dar, au uje huku mkoani Kagera ninapoishi (Nilidanganya)JULIET: Upo Kagera?MIMI: Ndio.JULIET: Mbona umeandika unaishi Dar?MIMI: Niliamua kuandika hivyo ili watu wengi waone nilikuwa nikiishi katika jiji hilo.JULIET: Nahisi unanidanganya.MIMI: Kweli tena. Sioni haja ya kukudanganya.JULIET: Sawa. Naweza kuja huko Kagera kesho kuonana nawe?MIMI: Kuja Kagera? Kesho? Mvua zinasumbua sana huku, barabara mbovu.JULIET: Usijali. Nitakuja na ndege.MIMI: Mmmh!JULIET: Nini tena?MIMI: Hakuna kitu. Usijali. Unaweza kuja.JULIET: Sawa. Nitakuja na ndege ya saa nne asubuhi. Ngoja nimwambie baba anikatie tiketi kabisa.MIMI: Poa. (Simu ikakatwa).
Dizaini sikuwa sawa katika hali hiyo, nikaanza kujiuliza kuhusiana na Juliet, mpaka kufika hapo, kuna kitu ambacho nilikuwa nimekifikiria kwa kuona kwamba juliet alikuwa ametoka katika familia ambayo ilikuwa ikijiweza sana kuhusiana na mambo ya fedha.
Ila, sikutaka kuamini, nilikuwa naona kwamba msichana yule alikuwa muongo, nilitaka kuona kama kweli ingewezekana kusafiri mpaka Kagera kwa ajili ya kuniona. Usiku wa siku hiyo, niliiona post yake akiwa ameandika ‘Nakwenda Kagera kesho, nahitaji maombi yenu’. Nilishtuka sana, nikaona kwamba Juliet alikuwa akimaanisha kile ambacho alikuwa ameniambia, nilichokifanya, nikaLIKE na kisha kuendelea na mambo yangu.
Kutokana na usiku uliopita kuchelewa kulala, asubuhi ya siku hiyo niliamshwa na mlio wa simu yangu ambayo ilikuwa ikiita, nikaamka na kisha kuangalia kioo cha simu ile, namba haikuwa imehifadhiwa simuni lakini kwa kuiangalia tu, nilikuwa nikiijua, ilikuwa ni namba ya Juliet. Huku nikionekana kuwa katika uchofu, nikabonyeza kitufe cha kijani na kisha kuipeleka sikioni.

****************************************ITAENDELEA

No comments