ANAOMBA USHAURI; NIMESHINDWA KUACHA KUJIUZA NA BADO NASOMA
Nilianza kidato cha kwanza Mwaka 2016 ikiwa ni siku chache au miezi michache baada ya kumaliza elimu ya msingi yaani darasa la saba.
Wazazi wangu ni wakulima walioishi kijiji kimoja huko fyentanyina Mkoa Rukwa Sumbawanga kijiji chetu ni jirani sana na Manisipaa ya SUMBAWANGA kwani nilibahatika sana kuchaguliwa kidato cha kwanza katika moja ya shule za serikali kubwa zilizopo Sumbawanga Mjini.
Nilipofika kuyaanza maisha ya shule nilifika kwa shangazi yangu alikua akiishi mjini hapo nilianza vyema sana bila yakujua kua mjini shule pia, nilipata marafiki wengi wakiwa toka mjini wachache tu walikua vijiji jirani na wengine walikua wa wakutoka katika kijiji cha Fyentanyina.
Mwaka ulipita nikafika kidato cha pili nikafanya mitihani ya kidato cha pili hatimaye nikafanikiwa kuingia kidato cha tatu ambacho mpaka sasa nilipo ingia kidato cha tatu alikuja dada yangu tulianza ishi naye nikahamisha makazi toka kwa shangazi yangu hapo sasa ndipo nilipo anza kujihusisha na mapenzi.
Sikujali masomo yangu ilimradi nipate pesa niishi na dada yangu, ilihali hata dada yangu alikua akifanya hivyo na nilipiga pesa (Kuwachuna Mabuzi) hadi dada yangu mwenyewe akanivulia kofia kuwa nimemzidi hata yeye aliekubuhu.
Hali hii imeshika hatamu sana kwa upande wangu hadi imetokea natembea na watu wenye umri zaidi yangu yote hii inakuja kisa harufu ya pesa Nashindwa kujizuia kani wakati mwingine nawaza vipi nimudu masomo yangu hata sijui nifanyenini.
Naombeni Ushauri wenu
Kwani nahisi rafiki zangu shuleni wameshaanza kunitenga kwa kuogopa kwa tabia Zangu pia mtaani napoishi naona aibu hata kutembea.
Kwani nahisi rafiki zangu shuleni wameshaanza kunitenga kwa kuogopa kwa tabia Zangu pia mtaani napoishi naona aibu hata kutembea.
No comments