Breaking News

FAHAMU LUGHA NZURI YA MAPENZI ILI UWEZE KUPATA MAHUSIANO SAHIHI

 

Moja ya tatizo la kawaida ambalo watu huhangaika nalo kwenye mahusiano ni jinsi ya kujielezea upendo Walionao kwa watu wanaowapenda.

Wengi wa watu hupenda mtu , lakini jinsi ya kujieleza ili kufikia matarajio yao ni ngumu sana katika mahusiano yote.Na wote wanaweza kuishia kutopenda na kupendwa.

Ingawa haya hutokea katika mahusiano 

ya kimapenzi, hayana limit; watu mara nyingi huhangaika sana kuelezea upendo wao kwa marafiki, familia na hata wafanyakazi wenzao pia!
Kama una tatizo hili la kushindwa kujiexpress, usihofu. kuna hizi mbinu 5 za lugha ya mapenzi itakayokusaidia jinsi ya kuelezea hisia zako na mapenzi ulionayo kwa mtu. kila mtu anaweza kuchukua mbinu ya jaribu hili la lugha ya mapenzi ili kufahamu namna ya kuonyesha watu kuwa wanawapenda.

Unahitaji kutambua jinsi unavyoweza kuwasiliana na hisia zako? Soma na ufahamu jinsi hio.

1.Fanya Kitu.

Kwa watu wengine , kwa jinsi ya kuonyesha mapenzi au kuonyesha kuwa anampenda mtu, ni kufanya kitu kwa ajili yao. Unaweza kusaidia kazi alizonazo, kumbebea mzigo alionao hata kama sio mzito, kumpikia na hata kufanya mazoezi kwa pamoja.

Na kama huyu ni mwenza wako wa msingi kwenye lugha hii ya mapenzi, wataelewa kuwa unamaanisha kitu kizuri kwao. unaweza kumwambia maneno ya wema pia, lakini yasiwe kama ya mapenzi. kwao vitendo huongea zaidi ya maneno. hupenda kusikia ukisema , ” acha hiki nitafanya mimi kwa ajili yako”, au” acha nikusaidie hiki. na kile.”

2.Mguso Wa Kimwili.

Watu wengine huwa na mguso wa kimwili kama ndio primary love language yao. ingawa hii huwa inahusisha sex, haizuiwi kuwa nayo. Hii pia inahusu kushikana mikono, kutoka pamoja, kissing and massaging. watu wa aina hii hupenda zaidi kuguswa kuliko kusaidiwa kazi au chochote. Labda iwe wamepokea habari mbaya, huhitaji kukumbatiwa na kusaidiwa na hata kupewa ushauri.

Kama unahitaji kuwa bora katika kugusa. anza kidogo, mkumbatie rafiki yako kila unapokutana nae, na kumkiss kila anapokuaga. fanya juhudi kushika mikono yao wakati ukiwa nao karibu. inaweza isiwe na maana kwako, lakini kwa mwenza wako ina maana kubwa. kwao.physical contact inavuta mapenzi na kujali.

3.QUALITY TIME

Kama primary language yako ni kwenye muda , ina maana uthamini kuwepo muda mwingi. weka usikivu. Hii haina maana kwamba ukae kwenye TV pamoja au kupigiana simu muda wote. Ina maana kuweka kila kitu standby wakati unapohitaji kukaa pamoja na kuongea.

Wakati huu munaweza kuongelea kazi zenu, matumaini na hata ndoto zenu; kwa muda wote huo kutakuwa na kitu cha maana kwenye kujihisi kuthaminiwa na kupendwa. kusudi kubwa la hapo ni kuwepo pamoja, na kama hupati muda wa kuwa pamoja utaanza kuhisi hupendwi na kukosa furaha. na kuona kuwa hauhitajiki.

4.Maneno Ya Kukubali.

Kwa watu wengi , kitu cha muhimu kwao ni lugha ya mapenzi ya neno la affirmation. Kwa mtu huyu vitendo huwa haviongei bali ni maneno yanakuwa na maana sana kwake, na bila ya mawazo positive, wanaweza wakaanza kuhisi kukosa furaha.

Watu hawa hukubaliana na comments za moto moto, kama vile,” Nakupenda” na ” kufanya hiki” maneno ya aina hio yanaweza kufanya siku yao kuwa nzuri , na hujisikia vibaya wasiposikia maneno hayo kutoka kwa wenza wao

Lakini pia huchukia kudharauliwa. kitu kimoja cha dharau kinaweza kuharibu week yao. kwa hio inabidi kuwa makini na maneno yako.

5.Kupokea Zawadi.

Kupokea zawadi ni lugha ya upendo ya mwisho , lakini inabidi ichukuliwe kwa ajili ya vitu vya maana. Mtu huyu hujali sana wazo na nguvu ya kwenye zawadi. wanaweza kupenda kupokea zawadi ya kadi iliotengenezwa hata kwa mikono kuliko ile ya kutoka dukani.

Kwa kadri anavyopokea hio zawadi, huhisi kujaliwa na kupendwa. ukikosa siku ya kuzaliwa kwao au kutofikiria zawadi yake, hujisikia kama kudharauliwa sana. kwao, zawadi huwafanya kuona kuwa ni kielelezo cha upendo. kwa hio kusahau kitu hicho ni maumivu sana kwao.

Kumbuka kuwa huyu mtu hakuvutiwa na pesa; huvutiwa na watu ambao ni wabunifu na wenye mawazo mazuri na wanaofanya mambo yasiotegemewa.

“If a long distance relationship survives, it’ll only grow stronger. So I’m going to make it work.”

No comments