Breaking News

JINSI YA KUSAFISHA UKE

 

Kama kuna kitu kinachomkera mwanamme katika uwanja wa sita kwa sita basi ni harufu chafu katika mwili wa mwanamke hasa uke. Na mimi hapa nitazungumzia usafi wa uke peke yake kwani hii ndo sehemu muhimu sana katika mahusiano na inayohitaji usafi wa hali ya juu sana pengine kuliko sehemu nyingine yoyote ya mwili wa mwanamke.
Jinsi ya kusafisha uke
Njia bora ya kusafisha uke ni yakutumia maji safi bila kutumia sabuni ya aina yoyote. Mara nyingi wanawake hutumia sabuni kusafisha si vibaya lakini ni vizuri ukatambua kuwa iwapo utatumia sabuni hakikisha kuwa haiingii sehemu ya ndani ya uke iishie sehemu za juu ya uke pekee, iwapo sabuni itaingia ndani ya uke huleta bacteria wabaya ambao baada ya muda mfupi huleta madhara makubwa ikiwemo na harufu mbaya. sabuni ni muhimu katika usafishaji wa miili yetu lakini si sehemu ya ndani ya uke bali sehemu nyingine za mwili najua wanawake wengi hutumia sabuni kujisafisha uke watashangaa kusikia kutumia sabuni kusafisha uke kuna hatari lakini sabuni huondoa mafuta ya asili ya ndani ya kum* na kusababisha ukavu ukeni kitu ambacho si kizuri hasa ukizingatia kuwa aina nyingi za sabuni zina dawa iitwayo chlorophenol ambayo huondoa aina zote za bacteria katika uke wakiwemo bacteria wazuri kitu ambacho hutoa nafasi ya bacteria wabaya kumea kwa kasi hivyo baada ya muda mfupi harufu mbaya au uchafu mzito sehemu za uke hivyo unapoosha uke hakikisha unaeepuka kuingiza maji yenye sabuni ndani ya uke, chukua maji safi osha uke bila kuingiza ndani ya mpasuko.
HATUA TATU ZA KUOSHA UKE
Hatua ya kwanza-ingia bafuni hakikisha kuwa bafu ni safi ikiwezekana lifanyie bafu usafi kiasi ambacho utalizika nacho wewe kwani bafuni pia ni sehemu ambayo imekuwa ukiwaletea magonjwa mbalimbali wanawake hasa ikiwa chafu magonjwa ambayo huambatana na harufu mbaya ukeni, wakati wa usafi unaweza kujisafisha ukiwa umesimama wima au umechuchumaa.
Hatua ya pili-polepole anza kusafisha uke wako kwa kidole cha pili toka dole gumba, kidole cha kati au chanda(kidole kiwekwacho pete ya ndoa) fanya hivyo kwa maji safi.Hii itakusaidia kuondoa uchafu wote mzito uliopo ukeni
Hatua ya tatu na ya mwisho – Suuza uke kwa kumwagia maji uke wako kuanzia mbele kurudi nyuma unaweza kutumia kikombe au kopo la plastiki hii pia itazui kupata ugonjwa na njia ya mkojo yaani UTI.

No comments