KUNA LUGHA TANO ZA MAPENZI, UNAIJUA YA MPENZI WAKO
Kwanini uliachana na ‘ingiza jina’?”…
“Ah tulikuwa hatuendani tu”
“Ah tulikuwa hatuendani tu”
Ushawahi kujikuta kwenye scenario hiyo?
Unaweza kumfanyia mpenzi wako kila jambo uonalo ni jema kwake na bado akakuacha au akatoka nje ya penzi lenu(cheating). Unabaki kusema “Nilikuwa nampa pesa, zawadi, na kumhakikishia nampenda na nataka tuje kuwa pamoja maishani lakini aliniacha.
Haya matatizo yote yanaweza kumalizwa au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa na kujua LUGHA YA MAPENZI anayoielewa mpenzi wako.
Lugha ya mapenzi ya mwenzi wako ni ile namna mtu anaona amethaminika zaidi na ukideal nae namna hiyo anaona hewaa, hapa napendwa.
Hujawahi ona mtu ashawahi kuwa na wapenzi kibao ila akipata mtu wake mmoja anatulia tuliiiiii?(am sure umewahi) Ni sababu anakuwa ameongea nae ile language yake anayoitaka yeye.
Kuna lugha tano maarufu za mapenzi. Naamini kuna nyingine; zinaweza kuongezeka hapa maana najua Tanzania ndo Eden kwenyewe.
1. Maneno ya kumhakikishia penzi
Mpenzi anayezungumza lugha hii ukimwambia I love you zake 10 kwa siku anatosheka. Ukimwambia Uko peke yako kwenye sakafu ya moyo wangu anafurahiiii. Ukimsifia kuwa kapendeza sana umemmaliza.
Onyo: Watu wa lugha hii wako sensitive na maneno. Kama ambavyo ukimwambia neno zuri anawasha penzi kama moto, ndivyo ukimtusi au kumwambia neno la kuumiza utakiona cha mtema kuni.
2. Muda wa kuwa pamoja bila bugudha
Wapo wapenzi wanaothamini muda wa kuwa pamoja na mwenzie kuliko chochote. Hata njaa hasikii, yeye awe tu na mpenzi wake aidha ndani au nje.
Ukiwa nae hataki mara umepigiwa simu na shogaako Mary, mara umeingia goal.com unaangalia kama Chelsea wamerudisha goli; anakutaka wewe na macho yako na masikio na kila kitu.
Onyo: Kuahirisha mipango na mpenzi huyu = Sikupendi!
Kuwa makini.
Kuwa makini.
3. Matendo ya kimahaba
Wapo ndugu zetu wengine wanathamini matendo ya kimahaba. Mara nyingi hivi ni vitu vidogodogo tu vya kuonesha unajali; mfano kumsaidia mpenzio kuosha vyombo, kumsaidia kubeba pochi, kumsaidia kufunga tai au vifungo vya shati, kumlisha mpenzi wako, kumsindikiza mpenzio kwenye gari aendapo kazini, kumpitia kazini mkapate wote lunch, kumshika mkono mbele za watu…ni vingi mnooo.
Onyo: Hawa watu wanaangalia sana matendo na huyahusisha na commitment; kama huwa unamfungulia mlango wa gari kila siku na siku moja ukaacha = Umepata mwingine!
Kama huwa unampakulia chakula mezani kila siku, siku ukaacha apakue mwenyewe = Una anayekutia kiburi!
4. Kupokea zawadi
Najua wanaume watasema “wanawake Tanzania wanaongea lugha moja tu, nayo ndo hii”
Najua wanaume watasema “wanawake Tanzania wanaongea lugha moja tu, nayo ndo hii”
Hakuna asiyependa zawadi jamani hasa ya mpenzi lakini hapa tunawazungumzia ambao haoni kama anapendwa kama hapewi vitu/pesa kila mara.
Hapa siongelei wachunaji au wanaouza nanii maana hao huwa hawapo kimapenzi. Nazungumzia mpenzi ambaye hakupi pressure ya kwamba anahitaji kiasi fulani au nataka hiki na hiki, yeye anahitaji uwe unampa zawadi kila mara kulingana na uwezo wako na usipompa anaona hakuna mapenzi hapo.
Onyo: Wapenzi hawa huwa sensitive sana na aina ya zawadi unayompa na kuilinganisha na uwezo wako. Yani ubora wa zawadi ndo ubora wa mapenzi.
Mfano birthday ya kwanza unampa perfume na kadi, ya pili unampa lollipop na kadi wakati anajua uwezo wa kuupgrade ulikuwa nao…sina la kukwambia.
5. Mguso wa kimwili
Actually, hii ndo lugha yangu mimi. Watu wa hivi tunapenda kugusana na wapenzi wetu. Kugusana haimaanishi tu katika ngono; hata katika mazingira mengine.
Tunapenda hugs, kisses, kushikwa mkono, kugusanisha miguu chini ya meza, kuegemewa, cuddling…name all physical contacts. Mpenzi akifanya hivi = Nakupenda Kinoma.
Onyo: Kama ambavyo watu hawa wanapenda mguso chanya, miguso hasi inawavuruga.
Kupigwa, kusukumwa, kutolewa mkono anapomshika mpenzi wake vinahit hard so do not try it; mwenzio atakachotafsiri hata hutotegemea.
=====
Baada ya kupitia hizi lugha ni muda wa kutafakari je wewe lugha yako ni ipi? Na ya mpenzi wako ni ipi?
Njia bora zaidi ya kujua lugha ya mwenzi wako ni kuangalia anaonesha vipi mapenzi. Mtu anayeelewa zaidi lugha ya zawadi believe me atakupa zawadi mara kwa mara sababau ndo anaona best way ya kuonesha penzi.
Anayeelewa lugha ya matendo ya kimahaba atakufanyia vitendo mbalimbali vya mapenzi. Wa maneno atakuambia maneno ya kukuaminisha penzi kila mara.
Anayeelewa ya muda atataka mara nyingi awe na wewe na anayeelewa lugha ya mguso utakoma kwa kuguswaguswa kila mara.
Kama wapenzi probability kubwa mtakuwa na lugha tofauti za mapenzi, ni wajibu wenu kujuana na kutendeana ipasavyo.
No comments