Breaking News

MAMBO AMBAYO NI VIKWAZO KATIKA MAISHA YETU

 

Katika maisha yetu ya kila siku kuna vitu ambavyo kimsingi tunakuwa tumevibeba ambavyo kimsing ukivitizama vitu hivyo havina msaada wowote katika maisha yetu.  Na vifutavyo ndivyo ndivyo vitu vinavosababisha maisha yetu yaendelee kuwa duni:
Kukimbia matatizo na kuogopa kushindwa
Je wajua? Ukikimbia matatizo yako, siku zote yatakimbia pamoja nawe. Usikimbie tatizo, likabili na kuamka haraka kila tunapoanguka. Na epuka Kuhisi kuna mtu mwingine anahusika na furaha yako.
Kuharibu Maisha ya Mwingine ili Ufanikiwe
Ukiharibu maisha ya mwingine, unaharibu ya kwako! Unaweza kuita Karma, Gundu, au majina mengine, lakini jua ya kwamba hii hutokea kweli. Pia ni ngumu kukaa na hayo mafanikio Maana hutakuwa na plani ya pili ya mafanikio zaidi ya kudhurumu, kuiba, kuua nk!
Kuamini kila kinachosemwa na “Wataalamu”
 Siku hizi kila sekta kuna watu wanaojiita wataalamu (mimi mmoja wapo!) Lakini nasikitika kukuambia kuwa, wengi wa wataalamu hawa, hawako sahihi kwani siku hizi watu wanapata kipato kutokana na kuyaelewa matatizo ya watu na si kujua suluhisho.
Usimuamini mtu eti tu kwa kuwa analielezea kwa uzuri na analielewa tatizo lako bali muamini anayeweza kutoa suluhisho linalokuwa msaada kwa tatizo lako.
Kujiweka wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe
Maisha yako yamejengwa kwa vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina nafasi yake, na kikikosekana basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na kuharibu maisha yote.
Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza na kuamua kujiweka sisi wa mwisho. Matokeo yake, unajinyima muda wa kupumzika, kula, kustarehe nk! Matokeo yake huwi na furaha na maisha yako!
Kukubali kuendeshwa na matukio mabaya yaliyopita
Kuishi kwa kuwa kuna kitu fulani kibaya kilikutokea kwenye maisha yako basi
Maisha hayatawezekana tena. Pengine ulifiwa, kufukuzwa kazi, shule, kuibiwa au kufilisika.
Kukubali kuzungukwa na watu wasiokufaa
Ni rahisi, Siku zote watu waliokubali kushindwa, huwa na sababu za kukupa kwa nini wameshindwa kimaisha, na ukikaa karibu nao watakupa sababu hizi na kukufanya uamini kwamba huu ndio ukweli, na hutakuwa tayari kupiga hatua zaidi.

No comments