Breaking News

NJIA ZA KUMFANYA MWANAUME APAGAWE NA PENZI LAKO

 

Nataka niwape darasa bomba ambalo linaweza kukufanya ukafurahia penzi au ndoa yako na kumfanya mwanaume wako akupende zaidi na kumteka kimapenzi asitamani mwingine zaidi yako,nadhani hakuna anayeingia na aliyeko kwenye ndoa na anapenda kusalitiwa,kila mwanamke anapenda kuonekana bora hivyo unapaswa kufanya haya ili penzi au ndoa yako iwe bora na imara. Ikumbukwe pia hata wanaume wanapenda sana wapewe hisia kuwa wao ni wa muhimu katika maisha ya wanawake,ukichunguza utaona kuwa wanawake wanaoonyesha uchangamfu kwa wanaume mara nyingi wanajikuta wamependwa na kutongozwa katika muda mfupi.
RAHA YA KUGUSANA NA MWANAUME
Ni kweli kitendo cha mwanamke na mwanaume kugusana kinaibua msisimko mkali sana na mara nyingi huamsha mishipa butu iliyolala kwa uchovu wa kutwa nzima.
Wanasayansi wamethibitisha kuwa kushikana na kugusana ngozi huleta hisia kubwa katika mahusiano ya watu wawili,kile kitendo cha kugusana ,kukumbatiana,kufanya romance ni hatua kubwa ya ongezeko la kumpandisha umpendaye hisia zake kiasi cha kukufanya uwe na hamu ya kuingia ndani ya kuta nne. Hebu jiulize ,unapokumbatiana na umpendaye unahisi? Hakika utaniambia kwanza unapata hisia za mapenzi na unatamani kufanya kitendo hicho,na wengine hupata mabadiliko makubwa sana wanapokuwa wamekumbatiana na wapenzi wao. Kitendo chochote kinachoweza kukutanisha ngozi na ngozi kina uwezo wa kuleta mabadiliko ya kikemikali katika ubongo wa mwanadamu na pia kuboresha afya ya mwanadamu.
Ngozi ni kiungo cha ajabu katika mwili wa mwanadamu na kiungo kinachofanya kazi kubwa sana,ngozi ndio kiungo kikubwa kabisa katika mwili wa mwanadamu. Inafunika mwili wako wote wakati viungo vyako vingine kama macho,masikio na pua vipo sehemu moja ya mwili wako. Ngozi yako imejaa mishipa midogo midogo ya fahamu maelfu kwa maelfu ,mishipa hiyo ya fahamu hutuma taarifa mbalimbali za mwili kwenye ubongo na unaweza kufumba macho,funga masikio yako,ziba pua yako na kufunga mdomo wako ,lakini kamwe huwezi kuifunga ngozi yako inayofunika mwili wako. Zinapogusana ngozi kwa ngozi ubongo hutoa amri ili mwili uweze kutoa kichocheo (hormone) kinasababisha mtu na mpenzi wake waweze kuendelea kupata hamu ya kuwa pamoja na pia kumfanya mtu apate shida kuanzisha uhusiano na mtu usiyemzoea.
Yapo maeneo mengine muhimu sana unapokuwa na mpenz wako ,itakupasa uyaguse kwani ni muhimu sana kwako na umpendaye,unaweza kukumbatiana na mpenzi wako ukiwa mmelala,kwa ubavu na hata chali.
Naomba ufahamu kuwa katika hali ya kukumbatiana tumia mkono wako wa juu kupapasa papasa sehemu ya nyuma ya mwili wa mpenzi wako,anzia kwenye shingo endelea kuteremka chini,pole pole sana endelea hadi kwenye makalio yake na mwishowe mapaja yake ,fanya kitendo hicho mara kadhaa kama mara 10 na kuendelea.
Baada ya kutumia dakika kama 5 hivi kupapasa papasa maeneo ya shingo,mgongo,makalio yake hadi mapajani kwa upande wa nyuma,sasa hamia ubavuni mwake ,taratibu pitisha kiganja chako tokea kwapani hadi mapajani ,wakati wa kurudisha mkono papasa sehemu za ndani za mapaja yake. Fanya hivi huku ukipumua taratibu kiasi cha kumchanganya ,unaweza kumpumulia pumzi zako masikioni mwake. Pia unaweza kutoa sauti nzuri za mahabati ukimsifu umpendaye ,siyo jambo baya hata ukimuita majina mbalimbali ya kimahaba kama vile Darling,honey,swity, nk. Usiwe bubu wala usipende kujifanya una mawazo mengi wakati upo na umpendaye. Akili yako ihamishie eneo husika na onyesha ushirikiano wa kutosha kama mchwa wanavyojenga kichuguu kwa ushirikiano mzuri.
Baada ya wote wawili kufika kileleni ni vizuri kutamani kwenda raundi ya pili ,ili kwenda raundi ya pili ambayo kuna uwezekano mkubwa kuwa itachukua muda mrefu ni vyema kuanza tena kwa kushikana shika ila safari hii mpenzi wako alale chali

No comments