UJUMBE KWA DADA ZANGU
Unielewe dadangu... Ujue kuna wakati ambapo ninyi kama wasichana huwa na mvuto kuliko kawaida... yaan kwa lugha nyingine naweza kusema wakati ambao unakuwa katika kilele(peak). Huu ni wakati ambao utafuatwa na kila mwanaume maana unakuwa na nguvu ya mvuto na kila kijana hutamani kukupata... ni kipindi kile ambacho unavunja ungo na kuingia katika usichana wako.
_-_-_
Huwa una mvuto wa sura na umbo kutokana na kazi ya hormoni za uzazi kufanya kazi ya kukutoa katika utoto na kuwa mtu mzima. Utaanza kuona mabadiliko kama makalio hujengeka zaidi, matiti husimama vyema wenyewe wanaita "chuchu saa 6" n.k
_-_-_
Lakini dadangu wapaswa kutambua kwamba ni kipindi cha mpito na kwa bahati mbaya nasikitika wengine huwa mnakitumia kipindi hiki vibaya. Unakuta mabinti wengi wanapoteza usichana wao(ubikra) katika kipindi hiki kwa kujichanganya na kila mwanaume. Hii ni kufuatia kusifiwa kila kona na kujiona wazuri hivyo kuona fahari na kiburi kuibuka.
_-_-_
Unajua huwezi kuwakataa wote wanaokutongoza maana wanakuja matajiri, wasomi, vijana wa karibu jambo ambalo kama binti hajafundwa vyema lazima atanasa katika mtego ama mitego yao kwa kukosa hofu ya Mungu.
_-_-_
Nasema ni kipindi cha mpito kwani baada ya muda, ule mvuto wa kimapenzi ukoma, matiti huweza kulala kama ndala n.k.
_-_-_
Lakini wanaojitunza kipindi hicho huwa tayari wamepata waume wa kuwaoa na kuwa mama za familia. Maana ni kipindi cha kampeni ambapo wanaume wote huja kunadi sera zao na hivyo mabinti wanaojielewa na kuwa na hofu ya Mungu kufanya chaguo sahihi wakati viruka njia wakiwakataa wanaume sahihi kisa tamaa za mwili na fedha. Tamaa yao huwafanya kuwa jamvi la wageni ama mama huruma ambaye wengine wanamuita "cha wote". Mbaya zaidi madhara ya kushindwa kujitunza katika kipindi hiki ni makubwa mfano kupata ujauzito usitarajiwa,
magojwa ya zinaa, kutoa mimba, kupoteza mwelekeo wa maisha, kukumbana na mapepo ya ngono na wakati mwingine hata kupoteza kizazi. Kama ukikoswa na yote hayo ndipo linapokuja suala la kukosa wa kukuoa na hata kupata UKIMWI.
_-_-_
Mabinti wengi wanashindwa kupata waume wa kuwaoa kutokana na ukweli kwamba wakati wanaume wenye malengo ya kuwaoa wanakuja wao waliwakataa na kuwaona hawana sera nzuri za kampeni. Walijiona wana hadhi kubwa kumbe kipindi tu mfano wa maua saa 6 yanayochanua saa 4 hadi saa 6 kisha yananyauka.
_-_-_
Dadangu kama kwa sasa ndo uko katika kipindi hiki hatarishi, jaribu kutumia hekima zaidi kwani usipoangalia, waeza kwenda na maji.

No comments