Breaking News

LIMBWATA BORA KWA MUMEO AU MPENZI WAKO WA KIUME

 



1.Muite jina lake la utani,,jina lile analolipenda sana.
2.Muache atumie mamlaka yake kama kichwa cha familia.
3.Usimcheke akiwa ameumizwa na jambo fulani.
4.kaa kimya pale anapokuwa na hasira,,unaweza ukaenda kumuomba msamaha na kumuelezea kwanini ulimkosea pale hasira zinapokuwa zimemuisha.
5.kuwa na haraka ya kuomba msamaha pale UNAPOMKOSEA,,sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe.
6.ongelea mazuri yake na yeye kabla ya ndugu,jamaa na marafiki hawajafanya hivyo.
7.waheshimu wazazi wake
8.msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kupeleka chochote na afanye hivyo hivyo HATA kwa wazazi wako.
9.msuprise kwa chakula anachokipenda,,hasa kipindi anapokuwa na msingi wa mawazo na kamwe usimcheleweshee chakula chake.
10.usimruhusu dada wa kazi amhudumie chakula ukiwa wewe upo nyumbani.
11.mkaribishe kwa kumkumbatia anapokuwa Ametoka kwenye mihangaiko yake,msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.
12.tabasamu pale unapomtazama,,vaa vizuri na ujipendeshe pale mnapotaka kutoka.
13.mpigie simu na umwambie unampenda na umemkumbuka.
14.muamshe asubuhi na umpe romance kiasi kwamba ifike hatua awe anaihitaji,,mpe na hatajishughulisha na wanawake wengine siku hiyo.
15.kamwe usithubutu kutamka kuwa hakuridhishi kwenye tendo la ndoa,,tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.
16.mwambie ni kiasi gani una bahati ya kuwa nae kama mume wako.
17.mkumbatie tu bila sababu yoyote ile
18.mshukuru Mungu KWA kukupa adamu katika maisha yako.
19.kumbuka kumuombea na kumkabidhi mikononi mwa Mungu.
20.Tengenezeni utaratibu mzuri wa kumshukuru Mungu kama familia kila asubuhi na usiku kabla ya kulala.

No comments