Vyuo vikuu, msingi wa ndoa mbovu
Nikiwaangalia wanafunzi wengi wa vyuo vikuu napatwa na walakini juu ya maisha ya mbeleni pindi watakapokuwa na familia; sijajua shida iko wapi, Je wanaingia chuoni wakiwa wadogo sana kiumri au ni hulka tu kwamba mtu akifika chuo lazima "ale bata"?
Wavulana wengi chuo kikuu huishi kwa kufuata mkumbo rika yaani inatokea tabia yake awali ilikuwa njema ila baada ya kuchangamana na aina fulana ya watu anajihisi unyonge kutofuata yale wenzao "wajanja" wanayofanya.
Wavulana wa chuoni huona kipindi ambacho wao wako chuo ndio kipindi ambacho ngono inabidi iwatambue wao ni akina nani (SIO WOTE) N a hili suala hupelekea wengi kutokuwa wavumbuzi wa masuala ya msingi ya kimaisha.
Mvulana akiwa chuo anapolalamika kuhusu boom kuwa halitoshi mawazo yake yote ni kutaka kufidia kwenye anasa hasa uzinzi
mimi nawaambiaga mtoto wa kiume ukipokea laki tano na sitini kila baada ya miezi miwili na ukalialia utakapoajiriwa wewe ni KILAZA MSHENZI
No comments