Sifa za Mwanaume wa Ukweli Chini ya Jua !
SIFA YA MWANAUME WA UKWELI, SI KUWA NA VIBINTI, VIBICHI VIBICHI, BALI TUTAKUPIMA KATIKA MAMBO YAFUATAYO !
Ujanja wa mwanaume si kujua kutongoza wasichana.
Imekuwa kama kadesturi miongoni mwa vijana tuliowengi ,tulioibukia katika kizazi hiki kinachoifahamu computer kuliko kitu kingine.
Kizazi kichoifahamu Google kuliko mlango wa kanisa au msikiti inashangaza.Mithili ya watu tuamkao toka usingizini tumepigwa na butwaa na bumbuazi limetuenea mawazoni hatuna cha kusema mbele ya dunia ya mavumbuzi.
Tumeshindwa kujiongoza,tumeyakubali matakwa ya mwili pamoja na tamaa iongoze mstakabari wa maisha yetu.
Tumeona ni ni ujanja na ufahari kuwa na mademu wengi,kuliko kuhangaikia mambo ya msingi kwa ajili ya kesho inayo kuja mithili ya upepo wa kimbunga.
Tumekuwa washamba wa mapenzi na ulimbukeni usio na sababu ndio unao tuliza kila iitwapo Leo kwa sababu tumeingia kichwa kichwa katika mapenzi tukidhani ni kama kunywa chai, kumbe tumejipeleka vitanzini kwa hiari.
Amakweli si kila anayejiita”born town” ni kweli anamaanisha akisemacho La hasha ,unaweza kuwa MTU wa town lakini bado mambo yako yakaonekana kama MTU wa pori tu,ambaye umekuja mjini kama mkimbizi wa kuyakimbia mashamba kijini na kudhani mjini atapata nafuu kwa sababu utalima lami.
Je umewahi kusikia wapi mwanaume akasifiwa kwa kuwa na mwamke mzuri?Kama mzuri Huyo ni wako mwenyewe nyumbani kwako.Hata hivyo umewahi kusikia wapi mwanaume na akili zake akajisifia kwa kuwa na wapenzi wengi?
Kama MTU Huyo yupo basi ni sawa na mtu alisifiaye kaburi kama sehemu salama kwake kuishi.
Uanaume wako Utapimwa katika Mambo yafuatayo;
Je,Una mpango gani na kesho?
Kama mwanaume wa ukweli tunatazamia kuona ukiwa umejiwekeza katika vitega uchumi vitakavyo kuingizia kipato na kukunusuru kesho.Usizoelee kuwa omba omba kwa ndugu yumkini hata kama ni ndugu wa damu,IPO siku watakuchoka tu.Jijengee mazingira ya kujitegemea na kuepuka utegemezi usio na sababu.
Wewe ni mwanaume huna budi kujua kuwa,kuna Leo na kesho.Je,waijuaje kesho yako ikiwa wewe si MTU wa kujishughulisha?.
Je,wazitafuta chapaa au Wazitegemea ndoto za Alinacha?
Huenda ukawa miongoni mwa wale wanao tazamia kuokota embe jangwani,au watazamia kuokota chungwa chini ya mti wa mnazi?Maana hao wote wanao tazamia alinacha kuwa tatulia matatizo yao ndio tunao shuhudia kila Mara wakikamatwa katika nchi za ughaibuni kwa biashara halamu,wanao bakia mitaani ndio tunawashuhudia wakijiita kaka poa na wengine kuishia kula msoto wa kitaa,inaumiza na inashangaza.Kumbuka kesho yako IPO mikonkni mwako.
Misimamo yako ipoje?
Itashangaza mwanaume mzima unakosa misimamo yako binafsi,tunategemea kuona kama mwanaume wa kweli na unayejitambua,basi ni dhahiri utakuwa na taratibu zako.Kumbuka kinacho mtofautisha mwanaume na mwanamke ni uwezo wa kiyapambanua mambo,hatutegemei kuona mwanaume akishawishiwa na wenzake,kushawishiwa kwa mwanaume kuna utofauti gani na mwanamke atongozwaye?kama baba matarajiwa tutakupima katika kipengele cha upambanuzi wa mambo.
Kutozoelea anasa”Mwanaume mjanja si yule anayejua kila viwanja Vya starehe ,ambako uozo na ushenzi hufanyika.Kujua club,makasino na sehemu zingine za wala bata si kigezo cha kuwa wewe ni mjanja wa town,Bali ni kukudhihilishia kwa kiasi gani bado hujakuwa.Na kama unahitaji kuwa baba bora wa baadaye hunabudi kuogopa anasa kama ukoma.
Akili ya Maisha unayo ?
Tunategemea kuona vitu vikali kutoka kwako,kama kijana uliyestarabika na kupewa dhamana na taifa na hata familia yako,basi uwe ni MTU wa kujiongeza.Tumia utashi wako na kipawa cha ufahamu uliopewa na Mwenyezi Mungu kuhakikisha unatoka kimaisha.
Tuwe na kiu ya maendeleo na wawajibikaji pasipo kukaa tu vilingeni.Usiogope kufikiria,usiogope kuishughulisha akili yako kwasababu hiyo ndio kazi ya akili ishughulishe.Tafakari kwa makini,weka mikakati yako,ingia mzigoni.Kumbuka katika maisha yako usichague kazi, labda iwe ni kazi halamu au itakayo ghalimu uhai wako.
Mungu ni kinga yako ?
Mwanaume anaebeza maswala ya kiimani hana budi kubadilika.Tunategemea kumwona kijana mwenye kiu ya maendeleo,kwanza anajitambua,anajiamini,pia ni MTU wa kuthubutu na Kumtegemea Mungu.Mwenyezi Mungu akusaidi katika ujana wako uishi vema katika ujana wako, ili uje ufurahie maisha yako baadaye.
Waweza tembelea pia katika kurasa zetu,Facebook,Twitter,Instragram kwa makala mbalimbali .
Pia kama unaswali waweza kutuma kwa mwandishi wetu kwa email.....hekimailuvanda@gmail.com
BARIKIWA.
No comments