Breaking News

Vigezo 7 Vya Uchumba Wenye Mafanikio !

 


Je,Uhusiano wenu Unastahili kuitwa Uchumba?
  

Hakuna anayetazamia kuingia katika mahusiano ya kinafiki.

Kila mtu anatamani kuwa na mtu sahihi,mwenye upendo wa kweli.Hakuna mwanadamu hata mmoja asiyehitaji kupendwa.

kila kiumbe kinahitaji kupendwa,hii inaweza kushuhudiwa hata miongoni mwa wanyama tunao wafuga majumbani.

Kila kijana anaye tazamia kuingia katika ndoa Siku moja, hana budi kujifunza kwa uangalifu kuhusiana na uchumba,urafiki na ndoa.

Usifurahie kuambiwa neno nakupenda,maana si kila neno nakupenda linaashiria upendo wa kweli.

Hata hivyo si kila mwanaume au mwanamke anafaa kuwa mwenzi wako.Mahusiano ya kimapenzi ni zaidi ya mwonekano wa kijinsia.

Ni dhahiri tupo katika kizazi ,kijuaji,kikaidi na kisichopenda kusikiliza MASHAURI,omba usiwe wewe.

Kila MTU mbishi atavuna mavuno ya ukaidi wake, hasa majuto.Kama jambo hulielewi,tafuta kijifunza jambo hilo.Epuka kuishi kwa kiyabahatisha maisha.

Linapo kuja swala la mapenzi huna budi kujiuliza maswali,mengi kukuhusu.Jiulize kweli mpenzi wako anakupenda?

Je,ni dhahiri anataka muoane au anataka kukupotezea mda?
Jiepushe  usiwe miongoni mwao ,walio ruhusu gharika ya mapenzi iwagharikishe.

Mara zote ushauri tunao utoa kwa vijana wakati wa kutafuta wenzi wa maisha,ni vijana kutafuta marafiki kàbla hawajaingia katika uchumba.
Mahusiano ni sawa na ukuaji wa mtoto.Kama vile mtoto mchanga asivyoweza kuruka hatua ya kutambaa kadharika vijana hawapaswi kuruka hatua ya urafiki.

Usikimbilie uchumba na kuruka hatua muhimu ya urafiki.Na kama ikatokea umeruka hatua ya urafiki na kuingia katika uchumba au uhusiano huo ni mzigo, labda iwe ni uchumba wa kimiujiza.
Huwezi kusema una rafiki ambaye tayari umekwisha mweleza hisia zako.

Rafiki yako ni  yule ambaye bado hajafahamu hisia zako za mapenzi,Bali anafahamu ukaribu wako kwake,amefahamu kujali kwako, na kwa namna unavyo husiana naye katika mambo ya kila siku.
Mara nyingi urafiki ulio bora ni ule ambao unawafanya wote WAWILI kuwa wawazi kila mmoja kwa mwenzake.MTU uliye mfungukia kihisia ,kwa kudai unampenda Huyo si rafik ni mpenzi tu!

Kosa kubwa tunalo lifanya wengi wetu Leo ni pupa na papara.
Kama kuna mtu umetokea kumwelewa ,hebu usiwe na haraka naye ,kuwa mvumilivu,jenga ukaribu Naye wa kawaida kabisa,mfahamu yeye ni nani, na ni MTU wa namna gani,anatokea wapi,anafanya nini,wazazi wake ,uhusiano wake na watu wanao mzunguka.Tumia mda mwingi kumfahamu kwa utafiti wako,kwa MSAADA kutoka kwa watu wake wa karibu na kwa uongozi wa Roho mtakatifu.

Ongea naye,Msalimie kila mara unapo mwona,husiana naye katika mambo ya jimuia.Mfano katika mazingira ya CHUONI,angalia ni wapi huwa anapendelea kwenda.

Sehemu za ibada kama in MTU wa ibada,katika matamasha ya uimbaji,katika mikutano na semina  mbalimbali,sehemu kama hizo kama mtazitumia zinaweza kuwaweka pamoja na kuwa Fanya muwe shirika moja katika mambo chanya yanayo husiana na maisha yenu kwa ujumla wake.

Katika urafiki huo,pia waweza kumwalika katika matamasha na makongamano kwa kumnunulia tiketi,na kuwafanya mhudhurie pamoja,hii itakuwa ni fursa yenye manufaa kwenu.

Mhusishe katika kazi unazo zifanya,afahamu wewe ni nani, unafanya nini ,usisite wala usione shaka kumweleza Ili afahamu ukweli kukuhusu.
Usikimbilie kumweleza hisia zako kabla hujahesabu gharama.
Baada ya kujiridhisha jiulize je unadhani anafaa kuwa mwenzi wako?

Je,Unadhani anaweza kuwa mtu sahihi kwako?
Je,Unadhani huu ni mda mwafaka kwako kuingia katika uchumba?

Kama utajiridhisha mweleze ukweli na nia yako.

Kumbuka uchumba ni hatua ya mwisho,inayokupeleka katika ndoa.Usiingie katika uchumba ikiwa  bado huna uhakika juu ya kesho yako.

Usikimbilie kumweleza rafiki yako unampenda na unatamani muwe wachumba ,ikiwa kabisa unajua hujajipanga,hujajiandaa na huna unachokitegemea kukuingizia kipato.

Tamko la uchumba Liwe na uhakika wa wewe kuingia katika ndoa,si chini ya miezi sita na si zaidi ya miaka miwili .Tokea pale tamko hili linapokuwa likitolewa na makubaliano yenu kufikiwa baina yenu.

Vigezo 7 Vya Uchumba;

Uanze kwa Nguvu ya maombi na uongozi wa Roho Mtakatifu.

Uchumba wenu hauna budi kufahamika(Mkatambulishane kwa wazazi au viongozi wenu wa dini).

Msijihusishe katika vitendo Vya ngono kabla hamjaoana.

Mfahamiane vema kila mmoja,amfahamu mwenzake kwa madhaifu yake na mazuri yake na kukubali kwa hiari kuandama ndoa.

Usiwe katika Uchumba na vijana zaidi ya mmoja huo si uchumba bali ubatili.

Usiingie katika Uchumba na mtu asiye amini.Usifungiwe nira na asiye amini .

Usiingie katika uchumba kama unajua hujakomaa Kiakili,Kimwili na Kiroho pia.Tunatazamia uwe ni mtu unayejitambua.

Mungu akusaidie katika harakati zako za kutafuta mwenzi wa maisha.Kamwe usikate tamaa,ingoje ahadi yako kwa saburi ukidumu kwa sala na kwa bidii pia.Wewe ndiye kichocheo kikubwa kupata mwenzi haraka au kuchelewa na kukosa kabisa.Kuwa makini na mienendo yako.


Waweza tembelea pia Facebook na twitter na instagram kwa makala mbali mbali.

Pia kama una swali waweza kutuma kwa mwandishi wetu kwa email....hekimailuvanda@gmail.com


BARIKIWA.

No comments