Siri ya Mapenzi Yenye Kudumu !
Wapenzi hawana budi kuelewa hisia zao.
Mapenzi yanayodumu ni Yale ambayo wapenzi wanaishi kama marafiki.
Kama utabahatika kupata mpenzi ambaye ndiye aliye kuwa RAFIKI yako,utakuwa sehemu sahihi zaidi kupita wale tunaovamia mapenzi.
Jifunze kupenda,hata kama hujawahi kupenda.Hii inaweza kusaidia namna ya kujali hisia za mwenzi wako,pamoja na mihemko yake na namna ya kuendana nayo pasipo shida yoyote.
Ufundishe moyo wako namna ya kuitikia miali ya hisia zilizo ndani ya vilindi Vya moyo uliopenda.
Tambua kuwa mwenzi wako ni wa thamani na thamani yake hakuna awezaye kuifikia,hivyo ni budi thamani,uzuri na upekee huo udumishwe ili kutoihafifisha thamani hiyo.
Hakikisha tabasamu haliondoki machoni pa mpenzi wako,mfanye ajisikie mwenye bahati kuwa nawe.Waweza kumpatia ZAWADI,maneno matamu na kwa ukarimu wa dhati na kumfanya ahisi kana kwamba yupo katika jumba la kifalme.
Usifanye choyo,kwa kumbania mpenzi wako.Kaa karibu naye uakisi hisia zake na upendo toka kwake.
Epuka kuwa mzigo kwa mpenzi wako kwa kuiangalia nafsi yako.Ikimbie roho ya ubinafsi ambayo ni sumu katika mapenzi.
Zungumza na mwenzi wako kwa Uhuru,furahia na jisikie amani kuwa pamoja na mpenzi wako.Kwa moyo mnyofu pangeni pamoja mstakabali wa maisha yenu ya baadaye,mwaweza panga ni aina gani ya familia mngependa iwe?Watoto wenu mngelipenda muwalee katika mazingira ya namna gani?
Uwazi na umoja kati yenu ndicho kiini pekee kwa kustawi kwa penzi lenu motomoto la ujanani.
Hata hivyo hunabudi kuwa chachu ya mafanikio ya mpenzi wako.Kwa kuwepo kwako aone utofauti kati yako na watu wengine.Mtie moyo mpenzi wako na kumfanya ajisikie mshindi hata katika Hali ya kushindwa kwake,mfariji na kuambatana naye katika vipindi vigumu vya maisha.
Moyo wake na upandikizwe nafsini mwako.Kama mpenzi wako ataupandikiza moyo wake ndani yàko huu waweza kuwa mwanzo bora wa ndoa,maana hapo ndipo mwazo wa kila mmoja kidhihirisha hisia zake kwa mwenzake hata katika nyakati ngumu katika maisha,kwa kuhakikisha mwenzi wako anaumia kama wewe,anaguswa na tatizo ulilo nalo.Yupo tayari kuvaa kiatu chako? Huyo ndiyo shabaha pekee yenye manufaa katika maisha ya mapenzi.
Kuwa tayari kukosolewa na kuwa tayari kulekebishika,sikio lenye kusikiliza,upole na unyenyekevu pamoja na Hali ya kujishusha hivi ndivyo viungo vya siri ya mapenzi yenye kudumu.
Kuwa tayari kukabili madhaifu ya mwenzi wako,kama utafahamu fika madhaifu yake,mapendezi yake pamoja na vipaumbele vyenu wote WAWILI hii inaweza kuwa tija kwenu kusonga mbele.
Kumbuka unaweza kumfanya mpenzi wako vile utakavyo wewe ikitegemea jinsi wewe ulivyo.Utamu wa mapenzi unategemea ushiriki wenu.Yafanye mahusiano yenu kuwa mfano wa kuigwa katika jamii yenu
Je tumsahau Mungu? La hata kidogo,ni wajibu wetu kumshirikisha MUNGU maana yeye ndiye aliyetupatia mapenzi.Barikiwa unapoamua kuishi vema katika mahusiano yeko na mwenzi wako.
Kwa makala mbali mbali na za kuvutia pia waweza kupata katika Facebook,Twiter,Instragram .
kama una swali au maoni waweza TUMA kwa email:hekimailuvanda@gmil.com.
BARIKIWA.
No comments