FACEBOOK CHATTING….3
MSICHANA: *Usiku wa jana umekuwa usiku wa kukumbuka sana kwangu.*Nilikuwa nikilalamika mpaka mama akasikia na kuamua kuja chumbani kwangu. Sijui amejua nilichokuwa nimekifanya kwani asubuhi alikuwa akiniangalia kwa jicho la wasiwasi sana.* Kama mchezo wenyewe upo vile, sijui itakuwaje. Unaonekana kuwa mchezo mzuri lakini uliojaa hatari.* Ingawa niliwahi kuucheza mchezo ule lakini jana ilikuwa balaa. Yaani kama ni mpira basi nimekutana na timu inayokimbiza muda wote.* Mbona upo kimya mpenzi? Naomba ukizipokea meseji hizi nijibu chochote ili niwe na furaha. Leo sijaenda shule kabisa kwa kuogopa kutokuelewa darasani. Nimesingizia naumwa. Yote kwa ajili yako. Nakupenda mpenzi. Nakupenda My Only Nyemo.
Nilibaki nikicheka sana. Msichana ambaye ilikuwa imepita siku moja tu tangu tuanze uhusiano wa kimapenzi alikuwa amechanganyikiwa sana. Mahusiano yetu yakawa yamechangamka sana kana kwamba yalikuwa yameanza miezi sita iliyopita.MIMI: Usijali mpenzi. Mchezo ule unahitaji sana maandalizi. Wengi wanashindwa kuucheza kwa sababu tu huwa wanakurupuka. Mimi kama mimi huwa ninakwenda hatua kwa hatua mpaka mwisho. Najiamini, ninafanya kazi zangu kwa uhakika mpenzi.MSICHANA: Una tabia mbaya sana. Mbona haukunijibu toka asubuhi nilipokutumia meseji zile?MIMI: Nilikuwa darasani baby. Hadi hapa bado nipo darasani.MSICHANA: Umejifunza wapi mchezo ule?MIMI: Nyumbani.MSICHANA: Mmmh! Una hatari wewe!MIMI: Hatari ya nini tena?MSICHANA: Ungeweza kuniua last night. Yaani kuna kipindi nilikuwa naona viungo vyote vikiishiwa nguvu.MIMI: PoleeeeeMSICHANA: Asante mpenzi.MIMI: Naomba leo tucheze tena.MSICHANA: Sitaki. Sitaki tena kucheza, utaniua jamani. Jana nilikuwa nahema juu juu kama nakata roho vile.MIMI: Polee sana. Ila ndio ukubwa huo.MSICHANA: Au ulitaka kunitoa usichana wangu?MIMI: Kwani unao?MSICHANA: NdioMIMI: Mmmh! Kweli hatari. Unanishangaza sana.MSICHANA: Kwa nini?MIMI: Ulidumu na mpenzi wako kwa muda gani?MSICHANA: Kwa miaka miwili.MIMI: Hamkufanya kitu chochote kile?MSICHANA: Ndio.MIMI: Alikuwa na chembechembe za ushoga nini?MSICHANA: Hahahaha! Kwa nini unasema hivyo?MIMI: Inawezekana. Miaka miwili halafu kimya. Haiwezekani, kuna jambo hapo nyuma ya pazia.MSICHANA: Inawezekana.MIMI: Hivi una miaka mingapi?MSICHANA: Kumi na nane.MIMI: Hahahaha! Unafaa kuliwa wewe. Umeshaiva mpenzi. Inabidi nikutungue kutoka mtini. Umeiva vizuri kabisa.MSICHANA: Hahahaha! Una maneno weweMIMI: Hayo ndio maneno tunayopenda kuyatumia huku kwetu. Miaka kumi na nane mkubwa sana, tena sana. Kama ungekuwa huku kwetu ungekuwa unatafutiwa mume.MSICHANA: Ningekuwa natafutiwa mume?MIMI: Ndio. Tungekuwa tunakula pilau sasa hivi.MSICHANA: Hahahaha! Sawa bwana. Ila inakubidi uwe na shabaha ya kulitungua tunda lililoiva.MIMI: Shabaha ninayo tena kubwa sana. Nikiona kama nakukosa, nitakupandia uko uko mtini. Hahahaha!MSICHANA: Una visa sana Mpenzi.MIMI: Usijali. Lecturer anaingia. Kama vipi tutaendelea kuchati baadae.MSICHANA: Poa. Nakupenda mpenzi.MIMI: Nakupenda pia.
Msichana yule alionekana kuwa msumbufu sana, muda wote alikuwa akinitumia meseji za mapenzi lakini sikumjibu hata moja, muda wote nilikuwa nikimfuatilia lecturer alivyokuwa akifundisha. Muda wa kutoka ulipofika, sikutaka kumshtua, nikarudi nyumbani na kujilaza kitandani.
MIMI: Nipo nyumbani.MSICHANA: Namshukuru Mungu umerudi nyumbani salama. Kuna kitu nilikuwa nakifikiria mpenzi.MIMI: Kitu gani?MSICHANA: Unaonaje tukionana somewhere?MIMI: Lini?MSICHANA: kesho.MIMI: Haitowezekana kabisa.MSICHANA: Kwa nini mpenzi?MIMI: Labda tufanye weekend.MSICHANA: Okey! Ila naomba tuonane mpenzi.MIMI: Usijali.
Baada ya hapo, mawasiliano yalikuwa yakiendelea kila siku, alitamani sana kuonana nami lakini nilikuwa bize sana mpaka pale ilipofika weekeend ambapo tulipanga sehemu ya kukutania.
MIMI: Umesema wapi?MSICHANA: Slipway.MIMI: Du! Sipajui bwana.MSICHANA: Acha kunitania mpenzi. Ila usijali, nitakuelekeza.MIMI: Poa.
Baada ya hapo akaanza kunielekeza. Si kwamba nilikuwa sipajui kweli Slipway ila kwa wakati huu nilikuwa nikitaka kucheza na akili yake tu. Nilitaka afahamu kwamba mimi nilikuwa mtoto wa uswahilini na hata sehemu nyingi za kuenjoy hasa za watu waliokuwa na uwezo fulani nilikuwa sina uhitaji wa kupafahamu.Nikafikiria kwa haraka haraka, sehemu ile ilikuwa haiendeki kwa daladala hivyo kama ningependa daladala ya Msasani na kwenda huko, ungekuwa mwendo mrefu kidogo. Sikuonekana kujali, kukutana na msichana wangu ndicho kitu pekee ambacho nilikuwa nikikihitaji.Asubuhi ya Jumamosi tukaanza kuchati kwa sms hata kabla hatujaonana.
MSICHANA: Ndio najiandaa mpenzi. Unataka nivae mavazi gani?MIMI: Vyovyote tu. Ila sipendelei kukuona ukivaa suruali.MSICHANA: Kwa nini?MIMI: Sina sababu.MSICHANA: Basi usijali. Nitavaa gauni moja zuri sana ambazlo nilinunuliwa na baba katika moja ya maduka makubwa jijini New York. Nitakuja nalo huko.MIMI: Poa. Wewe njoo tu mpenzi.MSICHANA: Ili uwahi, naomba ufanye kitu kimoja.MIMI: Kipi?MSICHANA: Kodi bajaji na hela nitalipia mimi huku.MIMI: Poa. Ila usiniingize choo cha kike.MSICHANA: Usijali mpenzi.
Nikaanza kujiandaa kwa haraka sana, japokuwa toka nizaliwe sikuwahi kufika mapema sehemu ya appointment ila siku hiyo nilitaka kufika mapema sana. Nilipomaliza kujiandaa, nikaanza kwenda kwenye maegesho ya madereva wa mabajaji ambako nikamuita rafiki yangu ambaye alikuwa akiendesha bajaji moja.
MIMI: Sikiliza Moody, nataka unipeleke Slipway. Kiasi gani?MOODY: Du! Unakwenda kufanya nini tena?MIMI: Achana na hayo. Kiasi gani?MOODY: Elfu kumi.MIMI: Poa. Ila naomba tufanye kitu kimoja.MOODY: Kitu gani?MIMI: Tukifika kule, sema gharama ni shilingi elfu ishirini na tano. Umesikia?MOODY: Poa. Kwani kuna mtu anakulipia?MIMI: Yeah! Mtoto fulani wa kishua.MOODY: Poa jembe. Ingia twende.
Nikaingia ndani ya bajaji na safari ya kuelekea Slipway kuanza. Ndani ya bajaji bado nilikuwa nikiendelea kuchati nae huku akiniambia kwamba amekwishafika na ni mimi tu ndiye nilikuwa nikisubiriwa.
MIMI: Sasa hiyo elfu ishirini na tano, yako elfu kumi na yangu elfu kumi na tano. Nitaifuata baadae nikitoka kuonana nae. Umenielewa?MOODY: Du! Yaani hata hauniongezi kwa mchongo ninaoucheza?MIMI: Nikuongeze nini hapo? Kwanza bei yenyewe tu umenibamiza. Halafu kama ningetaka si ningechukua daladala kwa nauli ya shilingi mia tatu na ningefika Msasani ningepiga kwa mguu mpaka Slipway.MOODY: Dah! Poa bwana. Mara ya kwanza nilitaka kushangaa eti unakodi bajaji. Mtoto wa uswahilini akodi bajaji!MIMI: Ndio hivyo bwana. Yaani hapa najiona kupata zali sana.
Safari ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi mpaka tulipofika Slipway. Gari nzuri na ya kifahari ilikuwa imepaki nje. Mara msichana yule akateremka. Nikajikuta nikianza kutetemeka kupita kawaida, sikuamini, sikuamini kama duniani kulikuwa na msichana mzuri namna ile. Nilibaki kimya nikimwangalia kwa mshangao. SI mimi tu, hata Moody alikuwa akionekana kushangaa. Uzuri wa msichana yule ulinishtua kupita kawaida.
MSICHANA: Vipi mpenzi?MIMI: PoaMSICHANA: Ngoja nimlipe dereva.
Akaanza kuisogeea bajaji na kisha kumlipa Moody gharama zake. Sikutaka kuzubaa, nami nikaelekea pale pale kuona anamlipa kiasi gani ili baadae Moody asije akanigeuka. Nikaona wekundu wawili na elfu tano wakitoka kwenye pochi yake, nikaona kwa ushahidi ule Moody asingeweza kunizika.Tukatoka hapo na kuelekea ndani. Ingawa mule ndani kulikuwa na warembo wengi lakini mbele ya msichana yule wote walionekana kuwa si kitu. Tukatafuta sehemu na kukaa. Vinywaji na chakula vikaagizwa na kuanza kula.
MSICHANA: Tukitoka hapa nataka twende tukapumzike kwenye chumba chochote kile.MIMI: Sawa. Ila jina lako hasa ni nani manake naona kwenye facebook unatumia jina la Precious Angel.MSICHANA: Naitwa Angeline.MIMI: Ok!
Tukala na kuanza kwenda katika sehemu iliyokuwa na vyumba na kuchukua chumba kimoja. Tulipoingia ndani, akaanza kuvua nguo zake na mimi kuvua zangu. Akajilaza kitandani huku akiniangalia kwa macho ya kurembua. Nami sikutaka kuchelewa, ninaanza kumsogelea. Nikaanza kumwangalia usoni.
GIDEON: Nyemo….Nyemo…Nyemo…amka.
Ilikuwa ni sauti ya kaka yangu ambayo ilikuwa ikisikika kwa mbali huku akiugonga mlango wa chumbani kwangu. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo nilivyozidi kuisikia sauti ile. Ghafla nikaamka kutoka usingizini. Mungu wangu! Kumbe matukio yote yale ambayo yalikuwa yakiendelea ilikuwa ni ndoto. Nikaamka, nikabaki kimya kitandani, sikuamini.
MIMI: Ndoto! Mungu wangu! Kumbe ilikuwa ndoto! Damn!
Nikasimama na kwenda kuufungua mlango wa chumbani kwangu, kaka yangu, Gideon alikuwa amesimama mlangoni. Nilikuwa nimechukia kupita kawaida.
GIDEON: Rafiki yako amekuja kukuulizia.MIMI: Nani?GIDEON: Andrew CarlosMIMI: Aaaggghhh! Kwa nini usingengoja hata kwa dakika moja.GIDEON: Kuna nini?MIMI: Dah! Nilikuwa chumbani. Tena kila kitu kikiwa kwenye hatua ya mwisho kaka.GIDEON: Mbona sikuelewi.MIMI: Naomba modem yangu kwanza.
Gideon akanipa modem yangu na kisha kuanza kurudi chumbani. Nikachukua laptop ambayo ilikuwa juu ya dressing table, nikaiwasha na kisha kuchomeka modem ile, nikaoganisha na internet na kufungua mtandao wa Facebook.
MIMI: Anaitwa Angeline.
ITAENDELEA..
No comments