Breaking News

FACEBOOK CHATTING….4

 Nikaanza kuwaangalia marafiki zangu wote huku nikimtafuta huyo msichana mwenye jina la Angeline. Sikuwa na rafiki huyo kabisa kitu kilichonipelekea kuanza kulitafuta. Majina yote yalikuja lakini hakukuwa na msichana yule, sura zao zilionekana kuwa tofauti kabisa na msichana yule mrembo. Sikutaka kuishia hapo, nikaanza kwenda kwenye akaunti zangu zote, twitter, myspace, beareshare, yahoo messenger lakini kote huko hakukuwa na msichana huyo.

MIMI: Mungu wangu! Kumbe alikuwa msichana wa ndoto! Kumbe nilikuwa nikiota. Ndoto….Ndoto! Kumbe ilikuwa ni ndoto! Nazichukia ndoto.
Nilijisemea huku nikionekana kukata tamaa. Sura ya msichana huyo bado itaendelea kubaki katika akili yangu, alikuwa ni msichana mzuri ambaye kila ninapowaangalia wasichana wote, hakukuwa na msichana ambaye alikuwa mzuri kama yeye. Miaka miwili imepita tangu niote ndoto hiyo lakini kamwe sura ya msichana huyo haikuweza kuondoka kichwani mwangu, nilikuwa namkumbuka kwa kila kitu. Nimejaribu kwa muda mrefu sana kumtafuta kwenye mtandao wa facebook lakini wala sijafanikiwa kumuona. Angeline….Angeline ataendelea kubaki kwenye akili yangu, nitaendelea kumkumbuka kila siku.
MWISHO WA SEASON 1
Unaikumbuka ile Season One niliyoandika kuhusiana mimi na msichana yule wa kishua? Leo hii nakuja na Season two ambayo itakuwa kali zaidi ya ile season one iliyopita. TWENDE PAMOJA.

Najisikia nimechoka sana huku laptop ikiwa mapajani mwangu na nimeunganisha na internet nikicheki updates za facebook, macho yangu yanakuwa mazito, natamani kulala lakini ghafla naliona jina, jina zuri la msichana mmoja hivi, jina la msichana ambaye nilikuwa namtaka kila siku toka kipindi kile alichokuwa akikaa mtaani kwetu. Ghafla uchovu wote ukanitoka, naanza kumwangalia, ndiye yeye, ndiye yeye kabisa kwani nilikuwa nimemtumia friend request jana tu, leo kanikubali kuwa rafiki yake, halafu yupo online.
Kwanza nasita kumpa hi, hii ni kwa sababu katika kipindi ambacho alikuwa akiishi mtaani kwetu, alikuwa akiringa sana kutokana na urembo wake, nilikuwa nimemtaka mahusiano ya kimapenzi zaidi ya mara saba, zote alinipiga mbavuni. Leo hii, huyu msichana Dorcas kanikubalia urafiki, lazima nianze upya mpaka anikubalie bila kujua mimi ndiye yule yule ambaye alikuwa akinikataa sana. Kwa kuwa katika kipindi hicho nilikuwa ninatumia a.k.a ya jina langu kama BROTHER PRINCE, hakuweza kunitambua. Ninamfuata na kumpa hi
MIMI: Mambo mrembo! (Nilimsalimia kwa kujiamini)DORCAS: Poa. Mzima Brother?MIMI: Nipo poa sana. Asante sana.DORCAS: Asante ya nini tena? (Aliuliza huku nikiona kabisa swali lake dizaini kama lilikuja na tabasamu pana)MIMI: Kwa kunikubalia urafiki. Nimefurahi sana.DORCAS: Usijali Brother.
Kwanza hapo nikakaa kimya, sikujua ilitakiwa niendelee vipi na mawasiliano naye, kwa dakika kadhaa, vidole vyangu vikabaki kwenye keyboard ya laptop bila kuandika chochote kile. Kuna kitu nikatokea kukikumbuka, nikaona ngoja kwanza niende kuangalia picha zake.Asikwambie mtu, alikuwa Dorcas yule yule, msichana ambaye alinifanya niwe kama chizi mtaani kwetu, msichana ambaye alinifanya niumwe na mbu sana vichochoroni, msichana ambaye alinifanya niwe namsubiria sana kumsindikiza shuleni kwao huku nikiwa radhi nichelewe shuleni kwetu.
MIMI: Dorcas……! (Niliita kwa mwandiko wa kioga)DORCAS (Baada ya dakika mbili): Abeeee.MIMI: Upo bize sana?DORCAS: Sio sana. Ila kwa nini umeuliza hivyo?MIMI: Nimeona nimekuandikia meseji halafu unanijibu baada ya dakika mbili kupita. Kweli haki hii jamani?DORCAS:Samahani. Unajua ninachati na watu wengi ndio maana.MIMI: Au kwa sababu mimi ni mgeni kwako?DORCAS: Hapana jamaniiiii. Nisamehe basi.MIMI: Usijali. Naweza kukuuliza swali moja la kizushi?DORCAS: Swali gani?MIMI: Lakini haujanijibu.DORCAS: Sawa. Uliza.MIMI: Unaishi wapi?DORCAS: Jamani ndio swali gani tena hilo. Si kila kitu nimeandika kwenye profile langu uangalie.MIMI: Ninatamani sana kufanya hivyo. Mtu anapouliza swali hili si kwamba siwezi kuangalia, hapana. Internet zetu kwa sisi tunaotumia simu huwa hazina kasi kabisa na ndio maana nimeona bora nikuulize tu.DORCAS: Kwa hiyo hapo unatumia simu?MIMI: Yeah! (Nilidanganya)DORCAS: Mmmh!MIMI: Mbona unaguna?DORCAS:Nakuona online.MIMI: Hilo si tatizo. Natumia Opera Min mpya. Naomba unijibu.DORCAS: Naishi Magomeni.MIMI: Ila si unafahamu kama ni kubwa sana.DORCAS: Nipo Mapipa.MIMI: Sawa. Nashukuru kwa kukufahamu. Naomba tuwe tunachati kila tunapokutana online.DORCAS: Usijali. Karibu sana.MIMI: Poa.DORCAS: Na wewe unaishi wapi?MIMI: Naishi Manzese Midizini (Nilidanganya kwani ningesema kweli, angehisi kitu).DORCAS: Owkey. Unasoma?MIMI: Nimekwishamaliza kidato cha sita (Nilidanganya tena)DORCAS: Shule gani?”MIMI: Makongo.DORCAS: Hongera.MIMI: Asante. Wewe unasoma?DORCAS: Nasoma kidato cha tano ila mwezi wa pili mwishoni naingia kidato cha sita.MIMI: Nawe hongera sana.DORCAS: Asante. Naomba nikuulize swali jingine.MIMI: Uliza tu.DORCAS: Mbona haujaweka picha yoyote ile?
Swali hilo likanifanya kukaa kimya kwa muda fulani, halikuwa swali gumu kabisa na pia nilikuwa na picha nyingi sana kwenye mashine yangu ila yeye ndiye alikuwa miongoni mwa watu ambao sikutaka waone picha yangu yoyote ile. Kumbuka kwamba Dorcas nilikuwa nikimtaka toka alipokuwa akiishi mtaani kwetu Tandale, tena katika mara zote ambazo nilikuwa nikimtaka, alinikataa sana kiasi ambacho mpaka nikachoka. Leo hii Dorcas alikuwa hapa, ninachati naye moja kwa moja kupitia inbox. Sikuwa tayari kwa kipindi hicho kuweka picha zangu, nilitaka zibaki zile zile za wasanii wa Wamarekani.
DORCAS: Mbona kimya Brother?MIMI: Sina picha. Ninatamani sana niweke picha ila tatizo simu yangu haina kamera. Ila usijali, ndani ya siku mbili, utaziona picha zangu.DORCAS: Sawa. Nakwenda kulala. Tutachati kesho Brother Mungu akipenda.MIMI: Mungu anapenda labda wewe usipende tu.DORCAS: Hahaha!MIMI: Huo ndio ukweli.DORCAS: Basi sawa mimi nakwenda kulala.MIMI: Usijali. Wape hi wote.DORCAS: Wa kina nani?MIMI: Utakaowaota.DORCAS: Na kama nikikuota wewe?MIMI: Nipe Hi tu. Ila kumbuka kwamba ukiniota, nami nitakuota, na kama tukiotana basi hiyo inamaanisha tumemisiana.DORCAS: Hahaha! Una maneno Brother.MIMI: Napenda kuongea tu. Ila usijali. Usiku mwema Dory.DORCAS: Nawe pia (Akaenda offline)
Kuanzia hapo nikawa na amani. Muda wote nilikuwa nikishukuru sana kwa Mungu kwa sababu alikuwa amenipa uwezo mkubwa sana wa kuandika kiasi ambacho uwezo ule nilikuwa nautumia kwenye chatting kiasi ambacho ulionekana kuwa mzuri sana.Huyu Dorcas nilikuwa namtaka sana, tena nilikuwa namtaka kuliko wasichana wote. Japokuwa zamani alikuwa akinikataa lakini nilikuwa nimekwishaapa kwa marafiki zangu kwamba ilikuwa ni lazima nimpate. Wengi walinicheka kidharau kwa kuniona najisumbua, hata alipohama nilichekwa sana kwa kuonwa kwamba sikuwa nimekamilisha lengo langu.

*** Unavyodhani atafanikiwa kumpata Dorcas..??
ITAENDELEA

No comments