Breaking News

FACEBOOK CHATTING….5

 

Leo hii, vita vya chini chini vimeanza, vita ambavyo sitotaka kuwaambia marafiki zangu mpaka pale ambapo ningekamilisha ‘mission’ yangu na kuwa naye. Hebu jifikirie kwanza, Dorcas angetoka vipi? Angeweza kuanzia wapi kunikataa na wakati nilikuwa na maneno mengi ya kuandika? Sikuona angetokea wapi, ila kama atanikubali, siku ya kuonana sijui ingekuwaje kama atagundua kwamba ni mimi atafanyaje? Ila hiyo siyo ishu, ishu kubwa ni kumfanya aangukie kimapenzi kwenye mikono yangu iliyo salama juu ya maisha yake……thats all.

MIMI: (Nikalog out na kulala huku nikisubiri kesho nianze pale nilipoishia)
Siku iliyofuata, nakumbuka kabisa sikuwa na fedha kwenye line yangu ambayo nilikuwa naitumia sana kuunganisha na huduma ya internet. Siku hiyo nilikaa katika hali ya unyonge kupita kawaida, akili yangu ilikuwa ikimfikiria Dorcas tu. Sikujua ningepata vipi fedha ya kujiunga na internet kwani muda wa kifurushi nilichokuwa nimenunua muda wa kujiunga, ulikuwa umemalizika jana usiku.Kwa sababu nilikuwa mjanja nikaanza kuwasiliana na baba, mzee Chilongani na kisha kumwambia kwamba nilikuwa na shida ya kiasi cha shilingi elfu thelathini. Japokuwa alinihoji maswali mengi, nilimjibu kisomi mpaka akanitumia kiasi hicho ambacho nikaamua kuchukua kifurushi cha mwezi mzima cha Vodacom, sikutaka tena kupata usumbufu wa kutokuwa na huduma ya internet katika harakati zangu za kumtia mikononi Dorcas.
Nilijiunga na huduma ya mwezi mzima ya Internet ya Vodacom na kisha kuanza kufungua akaunti facebook. Kwa wakati huo, akili yangu ilikuwa ikifikiria maneno mengi matamu ambayo nilipaswa kumwambia Dorcas katika kipindi ambacho ningemkuta online. Baada ya kufungua mtandao wa facebook, nikaanza kuangalia listi ya marafiki zangu ambao walikuwa online, walikuwa nane tu kwani kipindi hicho nilikuwa na marafiki 102 tu.
Kati ya watu ambao walikuwa online, Dorcas hakuwepo kabisa, nilinyong’onyeaje. Ikabidi nizuge zuge na marafiki ambao walikuwa online kwa wakati huo kwa kupiga stori mbili tatu. Nakumbuka ilipofika saa 9:17 alasiri, Dorcas akaingia online. Kwanza nikashtuka sana, mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi ya ajabu, sikutakiwa kuhofia chochote kile, nikaamua kumpa hi.
MIMI: Mambo Dory! (Nilimsalimia huku nikitoa tabasamu kana kwamba alikuwa akiniona).DORCAS: Poa. Mzima Brother?MIMI: Nipo poa. Nimekusubiri sana online.DORCAS: Acha kunidanganya Brother.MIMI: Nikudanganye ili iweje? Kwani kunatolewa tuzo kwa atakayemdanganya mwenzake?DORCAS: Hahaha! Hujaacha tu maneno yako?MIMI: Maneno gani?DORCAS: Si hayo hapo unayoongea.MIMI: Mbona yapo kawaida tu. Hebu acha nikuulize kitu kimoja. Uliniota jana usiku?DORCAS: Hapana.MIMI: Dah! Kwa hiyo uliniacha nikuote wewe tu bila kuniota?DORCAS: kwani uliniota?MIMI: Yeah! Nilikuota sana. Nilikaa nawe sana tukipiga stori. Nilifurahi sana.DORCAS: Uliota tukipiga stori wapi? Humu facebook?MIMI: Hapana. Ulikuja nyumbani.DORCAS: Kwenu?MIMI: Yeah!DORCAS: Mmmh!MIMI: Mbona unaguna tena?DORCAS: Siamini.MIMI: Huamini nini?DORCAS: Kama nilikuja kwenu.MIMI: Je nikikwambia kwamba ulikuja nyumbani na kuingia chumbani kwangu na kuanza kupiga stori chumbani humo, utaamini?DORCAS: Acha utani bwana.MIMI: Kweli tena. Halafu nikwambie kitu?DORCAS: Niambie.MIMI: Asilimia mia moja za ndoto zangu huwa kweli.DORCAS: Hahaha! Kwa hiyo unamaanisha hata hiyo itakuwa kweli?MIMI: Wewe unaonaje?DORCAS: Haitoweza kuwa kweli.MIMI: Okey! Tufanye haitoweza kuwa kweli. Ila ukiulizwa kama ungependa iwe kweli, utakubali?DORCAS: Inategemea.MIMI: Inategemea na nini?DORCAS: (Kimyaa)
Dizaini nikaliona swali langu ambalo nilimuuliza lilikuwa gumu kujibika, nilikuwa nikimuona akilini akiwa anafikiria jibu la kunipa. Wala sikuwa na wasiwasi kabisa, nilikuwa najiamini sana, hivyo nikakaa kimya na kuanza kumsikilizia angejibu nini. Ghafla katika hali ambayo sikuitegemea, akatoka online.Nilionekana kuchukia sana, kwa nini Dorcas atoke online na wakati alijua fika kwamba nilikuwa online kwa ajili yake, nilinyong’onyea sana. Mara ghafla huku nikiwa simuoni online, nikashtukia napokea meseji kutoka kwake.
DORCAS: Samahani Brother.MIMI: Samahani ya nini tena Dory?DORCAS: Nilikuwa Intenet Cafe, nilichukua nusu saa kwani kuna kitu nilikuwa namtumia kaka kwenye email yake, muda uliniishia. Kwa sasa natumia simu yangu.MIMI: Usijali. Upo wapi now?DORCAS: Nipo kwenye daladala naelekea nyumbani.MIMI: Take care njiani.DORCAS: Usijali wangu. Nikifika home nitakushtua.Mimi: Poa.
Hiyo ndio hatua ambayo ilikuwa ikiendelea. Kutoka kuitwa Brother mpaka kuanza kuitwa ‘wangu’. Hapa ngoja nikwambie kitu. Kwangu mimi, hasa katika kipindi kile cha nyuma kabla sijazoea, nilikuwa nikiona kuitwa ‘wangu’ lilikuwa jina moja ambalo lilikuwa likinichanganya sana. Mtoto wa kike aniite ‘wangu’? Anamaanisha nini aisee? Kwa nini niwe wake? Kila nilipojiuliza, nikabaki na mshangao wenye furaha moyoni mwangu.
Siku hiyo sikutaka kutoka online. Japokuwa nilitakiwa nionane na Rich Carter Jr saa kumi jioni lakini siku hiyo nikaamua kumchunia. Nilichokifanya ni kuizima simu yangu. Katika kipindi hicho, Dorcas alionekana kuwa muhimu sana kuliko Rich Carter Jr. Rafiki alikuwepo tu, hata kama ningekataa kuonana naye siku hiyo wala asingekasirika sana kwa sababu yeye yupo maishani mwangu.Ila hali ilikuwa tofauti na Dorcas. Kama angekuta kwamba sipo online au amenitumia meseji halafu imekaa muda mrefu bila majibu ingekuwaje? Ningemkasirisha kitu ambacho sikutaka kitokee. Kwangu, hasa kwa wakati huo, Dorcas alionekana kuwa kama yai au sahani ya udongo ambayo ilitakiwa kushikwa kwa uangalifu mkubwa sana. Kama kawaida, mara baada ya kufika nyumbani kwao, nikakuta meseji ikiingia kutoka kwake, kwa haraka haraka nikaifungua.
DORCAS: Nimefika salama wangu.MIMI: Mungu amejibu maombi yangu.DORCAS: Maombi gani tena?MIMI: Nilikuwa namuomba akulinde njia nzima.DORCAS: Kwa hiyo wewe mwanamaombi siku hizi?MIMI: Yeah! Halafu dizaini kama Mungu anajibu kila ombi ninaloomba.DORCAS: Ahahaha! Kwani ulikwishawahi kumuomba maombi gani ambayo aliwahi kukujibu?MIMI: Kuna siku nilipiga goti na kumuomba kwamba anipe bahati ya kuchati na msichana mzuri. Jana amenipa.DORCAS: Hahahaha! Msichana gani huyo nimjue?MIMI: Wewe.DORCAS: Hahahaha!MIMI: Unanicheka?DORCAS: Hapana wangu. Nimefurahi tu. Endelea kuomba tu.MIMI: Yeah! Jana nilipiga tena goti.DORCAS: Uliomba nini?MIMI: Niweze kukutana na huyu msichana niliyeanza kuchati naye jana. Ila kwanza kabla ya kukutana tuwe wapenzi.DORCAS: Una utani sana Brother.MIMI: Kweli tena. Namsubiria ajibu maombi yangu. Natumaini atajibu hivi soon.DORCAS: Ombi lako hilo bila kufunga na kuomba sijui kama litajibiwa.MIMI: Kwa nini?DORCAS: Ni ombi moja ambalo linahitajika kuwa na nguvu sana.MIMI: Litafanikiwa tu. Au wewe hauamini hilo?DORCAS: (Kimyaa)MIMI: Swali gumu?DORCAS: Hapana. Omba sana.MIMI: Nikuulize swali?DORCAS: Uliza.MIMI: Unanipenda?DORCAS: Kama rafiki wa facebook tu.MIMI: Hebu chukua sekunde kumi za kuzungumza na moyo wako juu yangu.DORCAS: Hata nikichukua dakika kumi, bado wewe ni rafiki yangu tu.MIMI: Nikwambie kitu Dorcas.DORCAS: Niambie.MIMI: Ukweli ni kwamba unanipenda. Nadanganya?DORCAS: Hahaha!MIMI: Nimekwishazungumza na moyo wako. Unaonekana kuwa mnyonge sana, moyo wako ulihitaji furaha ya kipindi kirefu sana, unayapenda sana mapenzi japokuwa wakati mwingine unaona kwamba mapenzi hayakupenda, labda umekata tamaa na kujiona kwamba una bahati mbaya sana katika masuala yote ya mahusiano. Labda umelia sana, au umehuzunika sana moyoni mwako kwa sababu ya mapenzi. Moyo wako nauona una kidonda kikubwa sana, kidonda ambacho hauamini kama kuna siku kitakuja kupona. Ngoja nikwambie kitu leo, mimi ndiye ambaye nitakuwa dawa kubwa sana ya kukiponyesha kidonda chako moyoni, kidonda ambacho kinaweza kuoza na kuuharibu moyo wako wote. Nitakuwa na uwezo wa kuja na kufanya kazi kubwa ya kukurudishia furaha yako iliyopotea……ila yote yatawezekana kama utafanya kitu kimoja tu.DORCAS: Kitu gani?MIMI: Kunipa ruhusa ya kuingia moyoni mwako na kuufungua ukurasa mpya wa kimapenzi. Tunaweza kuufungua sasa?DORCAS: Naogopa.MIMI: Unaogopa nini?DORCAS: Utaendelea kuumiza.MIMI: Unaniamini?DORCAS: Nakuamini.MIMI: Basi fanya kama nilivyokwambia. Niruhusu sasa.DORCAS (Kimyaa)MIMI: Dorcas.DORCAS: Abee.MIMI: Nakupenda sana.DORCAS: Nafahamu sana. Najua kwamba unanipenda sana. Kila siku umekuwa ukiniambia neno hilo. Nakumbuka ulikuwa ukikaa sana uchochoroni kwa ajili yangu, wakati mwingine ukinisindikiza shuleni na hata dukani na kuniambia kwamba unanipenda. Nilikuwa nikikufikiria sana, sikuamini kama kweli ulikuwa ukinipenda ila mpaka nilipohama Tandale ndipo nilipoamini kwamba unanipenda. Yaani ilikuwa ni sawa na kitu ambacho unacho, huwezi kukiona thamani yake mpaka unapokipoteza. Najua unanipenda Nyemo, najua unanihitaji sana.MIMI: (Kimyaa)
Kwanza nikashtuka, kumbe nilikuwa nikizuga muda wote huo na wakati Dorcas alikuwa akijua kwamba mtu ambaye nilikuwa nikijiita Brother Prince nilikuwa mimi. Moyo wangu ukaanza kujisikia aibu, nilitamani niache kuchati naye muda huo huo. Nilijihukumu moyoni kwa kuona kwamba inawezekana Dorcas alianza kuniona mimi malaya kwa kuwadandia wasichana wa Facebook.
ITAENDELEA..

No comments