Mdada Aliyekwambia Kujua Kuzungusha Kiuno ndo Tiketi ya Kupata Ndoa Kakudanganya..
Kila mwanamke anavitu vyake alivyojiwekea, ambavyo anataka mwanaume wa ndoto zake awe navyo. Ikitokea akampata Mwenye hivyo vitu basi huona kamaliza kila kitu, anajisahau, anafurahia vile anavyoviona kwa nje na kitandani, badala aanze kumsoma huyo Mwanaume. Kama ni husband material….
Wanawake ndio wanaongoza kwa kulizwa Sana kwenye mahusiano kuliko wanaume, kwasababu mwanamke akishampata mwanaume aliyekuwa anamtaka basi atampenda kwa kila kitu, moyo na mwili wake wote kwa haraka wakati yeye mwanaume hakupi vyote anakuangalia kwanza mpaka atakapoona kweli ndio kitu anachokitaka ndio ataanza kukupenda kwa ukweli sasa. Lakini akiona hakuna kitu atakuchukulia poa poa na baadaye anakupotezea, sasa wewe uliyekufa na kuoza lazima upate ugonjwa wa moyo.
Mwanamke usiende kwenye mahusiano kwa kuangalia picha ya nje, anza kwanza kumwangalia Kama anaweza kuwa Mume na je unampenda kweli, ukijihakikishia hapo anza kuwa wife material msaidie mwanaume hata kwa mawazo tu sio unakaa tu kazi yako wewe ni kuzungusha kiuno tu.
Inatakiwa ukiingia kwenye maisha ya mwanaume mwenyewe anakiri hakuna mwanamke Kama wewe. Unambadilisha hata Kama hakuwa muoaji ajue umuhimu wa mke na kutaka kukuoa.
No comments