FAIDA TATU ZA TENDO LA NDOA
“Watu wanaoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara, huwa hawa umwi umwi hovyo”, anasema Dkt.Yvonne K. Fullbright, mtaalam wa afya ya tendo la kujamiina. Baada ya nukuu hii kutoka kwa mtaalam, sio ajabu basi tukisikia kwamba faida kuu ya kwanza ni kuimarisha uwezo wa mwili wako kupambana na maradhi (strengthen your immune system). Uchunguzi uliofanyika Chuo Cha Wilkes huko jimbo la Pennsylvania, ulibaini kwamba kati ya wanafunzi waliojihusisha na vitendo vya kujamiiana mara moja au mbili kwa wiki, walikuwa na virutubisho zaidi vya kupambana na maradhi mwilini ukilinganisha na wale ambao walishiriki tendo hilo chini ya hapo. Pamoja na faida hiyo ya tendo la kujamiiana, wataalam walisisitiza kwamba ni muhimu kwa watu kuendelea kufanya vitu ambavyo pia ni muhimu kwa uimarishaji wa virutubisho vya kupambana na maradhi mwilini. Vitu hivyo ni kama ifuatavyo:
Kula vizuriKufanya mazoeziKupata usingizi wa kutoshaKuhakikisha umepata chanjo zote muhimu kwa ajili ya maradhi ambukiziTumia kinga (condom) kama hamfahamu hali zenu (Katika hili, thehabari tunashauri kama wewe ni mume, basi tafuta mke wa kuoa, na kama wewe ni mke, basi tafuta mume. Baada ya hapo, tulia katika ndoa yako, michepuko sio dili!!!)
Pamoja na kwamba kufanya mazoezi imetajwa kama nyongeza ya tendo la kujamiina kama vitu ambavyo vinaongeza vurutubisho vya kupambana na maradhi mwilini, tendo la kujamiina peke yake linahesabika kama mazoezi. Ndio maana, faida kuu ya pili ni kukufanya ufungue gym kitandani. Kwa maneno mengine, kujamiiana ni njia moja wapo ya mazoezi. Hapa ni muhimu kukumbuka kwamba hata mazoezi yanahitaji mapumziko, kwahiyo usije ukafanya tendo hilo kutwa nzima (kama unao ubavu) na kutegemea faida, badala yake utachuma hasara, ambazo sio mjadala wetu leo. Kama tendo hili litafanyika kwa umakini na utaratibu maalum, basi wataalam wanasema tendo hilo linachoma kalori (calories) tano kwa dakika, kalori nne zaidi zinachomwa ukilinganisha na mtu anayeangalia TV!
Wanandoa wakiwa katika miondoko kama walivyonaswa na kamera ya thehabari
Sababu kuu ya tatu, tendo la kujamiiana linapunguza uwezekano wa kuvamiwa na mshtuko wa moyo (heart attack!). Ukiachilia mbali kwamba tendo hili ni njia nzuri ya kuongeza mapigo yako ya moyo, pia ni njia nzuri ya kuhakikisha viwango vyako vya estrogen na testosterone vipo katika mizani sahihi kitu ambacho ni muhimu linapokuja suala la kuzuia uwezako wa kupatwa na mshtuko wa moyo, wataalam wanamalizia.
Hizi ni baadhi tu ya faida, bila shaka unazifaham faida nyingine lukuki, ambazo hazikutajwa hapa. Kama tulivyoonya hapo juu, kujamiiana ni tendo la kiungwana na lina faida nyingi kwa afya yako, hivyo basi, tafuta mke au mume, halafu dili nae! Michepuko sio diliii!
No comments